Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Siku za hivi karibuni neno KILAZA limepata umaarufu na kutumika kwa kasi kubwa hapa nchini. Neno KILAZA limepata umaarufu baada ya Rais Magufuli kuwaita VILAZA wanafunzi 7802 (special diploma) waliofukuzwa chuo kikuu cha Dodoma na kuwataka wakatafute vyuo vya saizi yao ya UKILAZA.
Kama lilivyo neno la KIHIYO, nalo KILAZA lina historia yake. Juzi nimeskiliza Honi Sigara wa Baraza la Kiswahili Tanzania akifafanua kuhusu KILAZA, japokuwa alizunguka sana kulitolea ufafanuzi lakini kwa ufahamu wa kawaida alimaanisha ni ''Uwezo mdogo wa kufanya jambo''.
Sigara aliendelea kuelezea kuwa halina maana moja kwa moja na uwezo wa akili, akadai pia kuwa asili ya neno KILAZA ni kwenye Tasnia ya Muziki.
Nikafuatilia kwenye tasnia ya muziki na ndipo nikajua kwamba, hapo kale kwenye muziki wa Dansi kulikuwa na mwanamuziki maarufu aliyejulikana kwa Jina la Juma KILAZA, Mwanamuziki huyo alikuwa na tambo na majigambo kuwa yeye ni bora kuliko gwiji la muziki Mbaraka Mwinshehe na ana uwezo mkubwa wa kutumia vyombo vya muziki kuliko Mbaraka Mwinshehe.
Ili kuondoa doubt, liliandaliwa Pambano kati ya KILAZA na Mwinshehe lakini tofauti na tambo za KILAZA, Mwinshehe alamgaragaza vibaya sana mpinzani wake na KILAZA alionesha UWEZO MDOGO SANA.
Kuanzia hapo neno KILAZA likaanza kukua kwa kasi na kutumika kwa watu wanaoonesha uwezo mdogo wa kufanya jambo.
* Honi Sigara amesema kuwa hili sio neno RASMI la Kiswahili, lakini watalifanyia mchakato na Utafiti na kama wataona linafaa basi watalifanya kuwa neno rasmi.
Asanteni sana.