# Nawaza kijinga na mawzo ya kijinga.

Mzururaji

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,559
1,272
Nawaza kijinga katika ubora wa ujinga wangu!

Mimi si nabii ila nahisi neno MAKONDA litaingia katika orodha ya misamiati mipya ya Kiswahili japo mpaka sasa sijui wanazuoni wa kitaa watalipa neno hilo maana ipi.

Hili li dhahiri sasa na linatiwa nakshi na historia ya baadhi ya misamiati iliyotokana na majina ya watu fulani kutokana na matukio yaliyowazunguka. Hii ni baadhi tu

1. Kilaaza:
Hivi sasa neno Kilaaza linamaanisha mtu asiye na uwezo (kiakili) yaani mbumbumbu. Lakini Kilaaza ni neno lililotokana na Juma Kilaaza aliyejinasibu anauwezo wa kupiga gitaa miaka ya 1970 kumzidi Mbaraka Mwinshehe. Kumaliza ubishi, likaandaliwa shindano Kati yao na Juma Kilaaza akaonekana hana uwezo.....Kilaaza

2. KIHIYO
Ni neno linalomaanisha mtu aliyeghushi vyeti vya taaluma ilhali hajasoma. Mwaka 1995 bwana Kihiyo alishinda ubunge jimbo la Temeke lakini ikabainika alighushi vyeti, katika kesi ya uchaguzi hatua iliyopelekea kuvuliwa ubunge. Kihiyo likawa msamiati wa kiswahili

3. Changudoa
Miaka ya mwanzo ya 1990 kigogo mmoja alikubwa na kashfa iliyogonga vichwa vya Habari ya kuwa na mahusiano na kahaba Maarufu mitaa ya Ohio jijini DSM aliyekuwa akijiita changudoa! Tokea wakati huo makahaba wakawa wanaitwa machangudoa!

4. Masaburi
Hili ni ingizo la hivi karibuni baada ya aliyekuwa meya wa jiji la DSM kusema wabunge wa DSM wanafikiri kwa kutumia Makalio........tokea wakati huo wote tunajua kilichofuata ni nini

5. Babu Seya
Hili ni neno linalomaanisha mwanaume mwenye tabia za kulawiti (watoto), Mara baada ya mwanamuziki gwiji Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha kutoa kibao Chao kilichotamba sana cha "Seya". Baada ya wanamuziki hao kufungwa kifungo cha maisha kutokana na tuhuma za ulawiti maneno babu seya yakawa moja ya misamiati mipya ya kiswahili.

Orodha ni ndefu sana, ila kwa kiwango cha MWENDOKASI naona kaka yangu Makonda anataka kuingiza jina lake katika orodha hiyo ya misamiati kutokana na matamko yake anayoyatoa kila kukicha;

1. Kupiga rangi Nyumba zote DSM
2. Ondoa ombaomba na makahaba
3. Marufuku shisha na sigara
4. Marufuku kuwafollow mashoga instagram
5. Msako wa wasio na kazi Nyumba kwa Nyumba, viongozi wasiotoa ushirikiano kushtakiwa

Kila siku ni amri na ahadi ambazo hazitekelezeki ukiacha alizotoa awali akiwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuwa walimu watasafiri bure na vijana wasio na ajira wapeleke vyeti na sijui iliishia wapi bila kusahau ile plan ya mtaa wa BAR, mtaa wa guest houses...yaani kila kitu mtaa wake. Ukitaka kunyoa utoke Tegeta uende Sinza au utoke Bunju ufuate bia Magomeni.

Kwa kasi hii tujiandae kwa msamiati mpya uitwao MAKONDA......Sijui wanazuoni wa kitaa wataupa maana gani.

#MawazoYaKijinga
 
Ngoja nisubiri tamko lake la wiki hii.kisha nitarudi ku comment
 
Umenikumbusha mbali sana, nilifanya interviewe mambo yakajiseti alaf nikapigwa LOWASA, - walikata jina langu...

Makondakta ni mzee wa unfinished business
 
We upo wap mbona huku kwetu tumeshaanza kulitumia huku kwetu ukiwa mbwatukaji basi tunakuita MAKOND.
 
Back
Top Bottom