Ijumaa ya tarehe hizi shosti!!!

Ijumaa ya tarehe hizi shosti!!!

maisha ni vile unavyoishi maisha,inakubidi uwe mbishi maisha.
Nalog off
 
hahahaa mkuu chama unamfananisha Bishanga na mrisho ngassa ile vidoe yake umeiona nini LOL

Mkuu Kaizer
Hapo ni mambo ya viwango Bishanga kiwango chake kidogo sana yaani kujua kupiga dana dana amejiona mchezaji kwenye ligi yangu hata kazi ya kurudisha mipira uwanjani kwenye mazoezi hapati hana sifa hiyo!!
 
Last edited by a moderator:
Japo sio shosti naomba nitie neno.......


Ilikuwa ni miaka minne baada ya kumaliza chuo, Miaka minne kazini na miezi miwili ktk ndoa.

....... Nilipigwa chini kazini ghafla, baada ya mkataba kwisha. Sababu ni matatizo binafsi na manager.

...... Wakati huo huo mke wangu kipenzi akaanza kusumbuliwa tumbo.

Nilihangaika sana hospital wakati huo huo nahangaika kutafuta kazi.

..... Yalikuwa ni maisha mapya kwangu na magumu sana.

........ Maisha yana changamoto nyingi sana.
 
asee we acha tu siku amini hiyo siku duh!!nilivyo fika nyumbani usingizi siku pata kabisa afu ndo tarehe za kulipa kodi dah!!after week marafiki walivyo jua niko juu ya mawe wakaanza kunikwepa kabisa nikawa alosto apeche ila nashukuru kibanda niliweza kulipia gafla mwili nao ukaaza kupungua kwa mawazo.aaah staki kukumbuka huo msoto now nimerudi hewani eti marafiki ndo wanarudi nimesema bora peke yangu
 
Mkuu Washawasha.
Kuna mambo mengine hayahitaji ubishi.
Kweli kabisa kiongozi wangu Mzee,ujue unatakiwa uwe unaijua hii miti miwili,kuna mkwaju na mnazi.Mnazi unapopigwa na upepo unakuwa mbishi mwishowe upepo unaung'olea mbali mnazi lakini mkwaju ukipigwa na upepo unakubali kupelekwa na unajikunja upepo ukiisha mkwaju unarudi tena kusimama na maisha yanakwenda.Kwahiyo katika maisha inatubidi tujifunze kupitia hii miti,hali ikiwa mbaya inakubidi ukubaliane nayo tu usilazimishe kuishi matawi ya juu wakati ukiwa umechoka ila ukizikamata RUKHSA kujiachia.
Nalog off
 
Back
Top Bottom