Ijumaa Kuu ya Pasaka nimeona jamaa wanatafuna nyama, tena 'mdudu'

Nipe andiko acha kuzunguka. Wewe hiyo authority ya ni bible tu umeitoa kwenye mstari upi?
Hujui ukristo. Kama jambo dogo kama hilo hulijui basi hujui kitu dogo. Nyama inaliwa Ijumaa bila shida na hamna dhambi mapokeo ya dini hayatusumbui sisi.
 
Mungu akusaidie ukutane na kweli. Ninakuombea uanze utafiti huru kwa muongozo wa Roho Mtakatifu. Tuombeane ndugu.
Kula nyama Ijumaa ya pasaka si dhambi na haijawahi kuwa dhambi. Huna kifungu katika Biblia dogo. Unaleta Blaah blaah tu
 
Nipe andiko kuwa Ukristo muongozo wake ni bible tu! Bible yenyewe inajikataa kuwa muongozo pekee
emoji41.png

Biblia yenyewe ni sehemu ya mapokeo soma hapa ....

15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
2 Wathesalonike 2:15
Biblia yenyewe ni sehemu ya mapokeo soma hapa ....

15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
2 Wathesalonike 2:15
Pole sana ndugu Neno la Mungu alisomwi hivyo lazima uwe mtafiti, lazima ufanye referance ya Biblia zaidi ya Moja na kuagalia muktadha wake, Biblia zongine zilichapwa kukudhi mafundisho ya Ibada ya dhehebu fluni, ndiyo maana tunatakiwa kusoma biblia hasa iliyotafsiriwa toka kwenye maandiko ya awali ya Kigiriki ndiyo maana Biblia habari njeme inasomeka "Mafundisho" Nimeweka hapo chini.

Screenshot_20210402-220650.png

Screenshot_20210402-220759.png
 
Biblia yenyewe ni sehemu ya mapokeo soma hapa ....

15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
2 Wathesalonike 2:15

Kuhusu Kula nyama Kwa kukuongezea maarifa soma hapa attachment

Screenshot_20210402-222442.png
 
Tatizo lako ni kufikiri biblia ndio muongozo pekee. Hadi karibia karne ya 4 Wakristo hawakuwa na biblia! Hivyo heshimu maelekezo ya Kanisa na kama huyaelewi tafuta facts!

Hiyo biblia unayoitaja ni sehemu ya kazi za Kanisa kama ilivyo hiyo amri iliyowekwa na Kanisa! Mwenye kusoma hili na afahamu!
Ipo siku utajikuta una-compromise Ukristo na mapokeo. Mapokeo ni mila na desturi zilizorithishwa au kurithiwa kutoka vizazi vilivyopita.

Mathayo 15: 2-6
2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.

3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?

4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.

5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,

6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

Vv
 
Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu, Ijumaa Kuu ya Pasaka ni mwiko /marufuku watu kula nyama kwani ni siku maalum ambayo Bwana wetu YESU Kristo aliteswa msalabani kwa dhambi zetu sisi wanadamu.

Ni ujinga fulani wa Yuda Eskalioti aliyerubuniwa na vipande vya sarafu (pesa).

Ijumaa Kuu ni siku ambayo Bwana Yesu alimwaga damu msalabani, na umauti ukamkuta...

Nyama hairuhusiwi kuliwa siku ya Ijumaa Kuu. Ni mwiko yaani.

Nimeshangaa sana nimeona jamaa wanakunywa beer , wanakula na minyama wamejaza kwenye masinia makubwa (mlima) kabisa bila haya. Na mbaya zaidi wanakula kitimoto yaani nguruwe. Ni hapa Moshi, Kilimanjaro.

Hiyo nguruwe ilikuwa imekaushwa vizuri sana , mikachumbari mingi sana, ndizi za kutosha na pilipili na kukata ile...

Tuache dharau mbele ya Mwenyezi Mungu. Haifai.

Anyway kila mtu ataubeba msalaba wake.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Hao uliwauliza au walikwambia wao NI dini gani au madhehebu gani?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Unasema hiyo kitimoto ilikuwa imekaushwa vizuri sana, maana yake haina damu.....biblia inachokataza ni kula damu kwa sababu damu ndo inabeba uhai wa kiumbe. Kukoleza uzi wako ungetupia kapicha tuone namna hayo majamaa yalivyokuwa yamepania kula vinono siku ya ijumaa kuu siku ambayo watu wanakuwa wanahitimisha mfungo...
 
Ipo siku utajikuta una-compromise Ukristo na mapokeo. Mapokeo ni mila na desturi zilizorithishwa au kurithiwa kutoka vizazi vilivyopita.

Mathayo 15: 2-6
2 Mbona wanafunzi wako huyahalifu mapokeo ya wazee, kwa maana hawanawi mikono walapo chakula.

3 Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?

4 Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.

5 Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,

6 basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

Vv
Yesu hakuja kutengua torati bali kutimiliza. Nimekupa nukuu za agano jipya hujaelewa? Mapokeo tunayosema hapa ni ya mitume na mahalifa wao soma haya maelekezo sio yangu ......15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
2 Wathesalonike 2:15
 
Halafu asilimia kubwa ya Viongozi wa dini Masheikh na Mapadri ndiyo watenda dhambi wakubwa.
Lete ushahidi Kama kweli viongozi wengi wa dini ndo watenda dhambi wakubwa.
Taja mkoa unaoishi una viongozi wa dini wangapi na watenda dhambi wakubwa wangapi.

Mapadre,.......
Mashehe......,.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Akili za walokole hizi.

Lete kifungu kinachozuia hilo sio unatoa hoja Mihemko mzee.

Taja fungu watu warejelee wajifunze usilete habari za kusadikika
 
Yesu hakuja kutengua torati bali kutimiliza. Nimekupa nukuu za agano jipya hujaelewa? Mapokeo tunayosema hapa ni ya mitume na mahalifa wao soma haya maelekezo sio yangu ......15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.
2 Wathesalonike 2:15
Torati sio mapokeo, torati ni sheria za Mungu, hizo ndio Yesu hakuja kuzitangua. Kula au kutokula nyama Ijumaa ni mojawapo ya mapokeo ambayo Yesu anawaambia watu wa dini kuwa wanashika mapokeo na kuacha maagizo ya torati.

Vv
 
Si lazima kila kitu kiandikwe kwenye biblia. Kanisa si kazi ya kitabu "bible" bali Bible ni moja ya kazi za Kanisa! Ni Kanisa liloamua Bible kuwa mafundisho rasmi ya Kanisa!

Ni hilo hilo Kanisa lililoamua ijumaa kuu usile nyama! Kama huelewi logic ya kanisa ya kutokula nyama ijumaa kuu uliza! Ila kama bado una akili ya kila kitu kiwe na nukuu ya Bible basi ujue bado una safari ndefu hata kama una nena kwa lugha
Hizi biblia za kawaida hazina baadhi ya vitabu ambavyo vinatumika na kanisa katoliki, mfano kitabu cha hekima ya Suleimani na kitabu cha makabayo....sasa akisubiri kila nukuu aipate kwenye hizi biblia za kisasa atapotea...
 
Kitabu cha hekima ya Suleiman, makabayo, yoshua bin sira, Daniel kuanzia 13, vingine ulivyo visema hakuna kitabu kinachosema watu wasile nyama siku flan ili kukumbuka mateso ya Yesu na pia hivyo vitabu vimeandikwa kabla ya yesu kuja duniani
 
Mengine ni mafundisho, mapokeo au tuseme ni amri za kanisa....
 
Back
Top Bottom