Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,427
- 154,271
Gari hii inapatikana ikiwa na aina za injini zilezile za matoleo ya machaguo ya model zilizopita ambazo ni 3B,13B,14B,15B-T,1HZ,1HZ-T na 1HD-T.
Coaster ni gari ya kwanza kufanyiwa mabadiliko mazima ya muundo wa bodi ( full redesign ) chini ya shirika jipya la Toyota's Commercial Vehicle (CV) kampuni ambayo Ni mahsusi kwa ajili ya kubuni na kuendeleza magari ya BIASHARA.
The fourth generation Coaster imefungwa vifaa vingi vya teknolojia ya juu vya kiusalama kama standard air-bags kwa ajili ya dereva na abiria wa kiti cha mbele.
Pia gari inakuja na Vehicle Stability Control (VSC), a ringed frame body kwa ajili ya kudhibiti gari isianguke ikikata Kona ikiwa kwenye mwendokasi, pre-tensioners kwa ajili yamikanda kwenye viti na pia zimewekwa force limiters inayopunguza pressure kwenye vifua kwenye vifua vya abiria iwapo itatokea magari kugongana uso kwa uso.
Pia ngazi za mlangoni zilirefushwa kwa 65 mm (2.6 in) ili kufanya wepesi wakati wa kuingia na wakati wa kutoka.
Viti ndani vimeongezewa shepu na upana wa sehemu ya kukalia na ile sehemu ya kuegemeza mgongo.
Kioo cha mbele kimepanuliwa ili kumuwezesha dereva kuona kwa uzuri.
Coaster imetolewa katika configurations tatu;
- Standard wheelbase configuration ambayo inabeba abiria 25,
- The long wheelbase configuration inayokuja na viti vya abiria 24 au 29
- School BUS configuration ambayo ina seat 3 za watu wazima na 49 vya watoto. The school bus configuration haina kiti Cha mbele cha abiria.