*************************
SEHEMU YA NNE
*************************
NGUVU YA SOULTIE (si wawili tena)
Mke na mume wakiwa sawa mbele za Mungu, muunganiko wao hutengeneza nafsi moja. Kwa hiyo mbele za Mungu kila jambo linalofanywa na mkono wa kushoto ni lilelile linalokubalika na mkono wa kulia. Huwezi kusema mkono wa kushoto unataka kufungua mlango huku mkono wa kulia unapinga. Sababu ni kuwa viungo vyote source yake ni moja tu, ila tofauti ni uwezo wa majukumu. Mwingine atasema mkono wake wa kushoto una nguvu, mwingine atasema mkono wa kulia, lakini mwili ni mmoja.
Anayeamrisha mkono wa kulia ndiye huyo huyo anayeamrisha mkono wa kushoto. Kwa hiyo, nafsi inayomwongoza mke ndio hiyo hiyo inayomwongoza mume. Tofauti na aina ya majukumu na si kukinzana kwa amri. Sasa kama ndivyo, wawezaje mkono kupeleka maombi yake kwa siri kwenye ubongo pasipo mkono wa kulia kufahamu? Ndivyo ilivyo kwa mke na mume. Mke awezaje kumlilia Mwenyezi Mungu pasipo mume kujua? Mume naye awezaje ikiwa nafsi yao ni moja? Ndio maana tunaongelea KUWA NA NIA MOJA ili kuweza kupeleka hoja za nguvu.
Mke na mume wakishibana mmoja akipata tatizo, wote wanaumia, mmoja akiugua wote huwa wagonjwa, mke akipata mimba mume anapata kichefuchefu nk. Hiyo ndio nguvu ya soul tie.
Nguvu ya tendo la ndoa
Tendo la ndoa ni muunganiko wa mwili na roho kati ya mke na mume ambao tayari ni nafsi moja. Hili ni tendo la kukumbuka tukio la uumbaji ambapo Mungu aliumba mtu mume akampulizia roho moja ambayo ilikuwa ni Adam na Hawa. Baada ya kuwatenganisha ndipo tukawa mwanamke na mwanamume tofauti. Sasa roho ya mke hutafuta kuirudia roho ya mwanamke ili kukamilisha nafsi. Hili ni somo zuri sana ambalo huweka wazi namna Mungu alivyofanya uumbaji wake na kujua asili ya mvutano wa kimapenzi. Tuendelee na mada....
Umewahi kujiuliza ni kwa vipi binti akampenda mvulana kiasi hata wazazi wakiingilia kati kuwatenganisha hutishia kujidhuru? Wengi wanasema binti ama mvulana kachanganywa na mapenzi. Ukweli ni kuwa kuna jambo lililofanyika katika ulimwengu wa roho. Kama sio ushirikina umetumika kuiteka nafsi, basi ni soul tie. Ndipo wanaume wengine hutamba kabisa, huyu binti hata akija kuolewa hana ujanja juu yangu, nitalala naye kila ninapotaka, halafu kweli inakuwa hivyo!! Hawa wanaweza kutengana kadri wanavyozidi kuingiza nafsi nyingine ndani, kisha mahaba haya hubaki kama kumbukumbu nzuri akilini mwao (wanajenga hali ya emotional blur).
Je umewahi kuona mwanamume, kwa sababu ya wingi wa mali zake akaamua kupora mpenzi wa mtu mwingine na kumfanya mke? Huyu ni mjinga kabisa asiyeelewa ni jinsi gani utajiri wake utatumika kumlea huyu kijana mwenye soul tie!! Kile kivuli kilichomo ndani ya mwanamke huyu kitakuwa kikiamka mara kwa mara na kumwamuru asimzuie kitu mwenza wake (aliye rohoni). Mume bandia hugeuka mshika mapembe huku maziwa akifaidi mwingine. Nguvu ya soul tie hupofusha hata mke yuko tayari kuvunja ndoa yake na kuharibu maisha mazuri anayoishi na mume bandia kwa sababu ya msela mmoja!! Hiyo ndiyo soul tie, jihadhari usijeingia kwenye mtego huo hatari!!
Hatari ya soul tie
Sasa hakuna jema lisilo na madhara. Tayari tushaona jinsi gani muunganiko huu unaweza kupelekea hata ndoa kuyumba. Lakini si hayo tu, soul tie ni nguvu ya hatari pia kama wapenzi wawili hawatakuwa na kujizuia.
Mwanamke ndiye aliyebeba sura yote ya mwanamume ndani yake, hivyo aweza kutumia mwanya huo kumuumiza mwanamume. Mfano mwanamke aweza kujiapiza kuwa, kama umeingiza tupu yako ndani yangu, ukakojoa humu, basi hutokuwa na amani hata ukipata mwanamke mwingine yeyote. Mwanamke huyu kama kweli ulimkuta katika ujana wake akakushiba, basi mwanamume utaishi kwa kutangatanga bila malengo. Utashangaa haudumu na mwanamke yeyote yule.
Au umewahi kusikia wazazi hulaani? Basi jambo hili wengine huliona kama masimulizi lakini lipo kabisa!! Mama anapokubeba tumboni mwake miezi tisa akakuzaa, basi ujue kivuli chako hubaki ndani yake. Ndio maana mtoto hata awe mvuta bangi, jambazi sugu, teja nk kwa mama atabaki kuwa MTOTO BORA kabisa. Akiwekwa ndani mama atampigania atoke, akiwa na shida yoyote mama aweza kugombana na ndugu wengine ili wamsaidie. Ndio maana ni kutokuwa na maarifa kuanzisha biashara changa halafu ukaweka ndugu zako wa damu waisimamie, kwani siku wakiihujumu, ukawapeleka polisi ili warejeshe walichoiba, mama huapa kutembea uchi kama hujawatoa. SOUL TIE!!!
“Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
”
— Mithali 10:1
Baba husimama na mwana mwenye hekima, kwa sababu ndio sifa yake. Hana mambo ya soul tie na watoto, lakini mtoto akiwa mpumbavu tu, baba hajishughulishi naye katu. Mama ndio ataanza kuhangaika mara polisi, mara kwa mjumbe nk.
Sasa mama ili amlaani mwanae huvua nguo na kubaki utupu, kisha humwonyesha uchi wake huku akimwapia, mfano, kama nilikubeba tumboni mwangu miezi tisa, nikashikwa uchungu nikakunya, ukapitia hapa kwenye uchi wangu,....... Hapo mama anaamuru kivuli cha mtoto kilichobaki tumboni mwake ambacho ndicho huleta muunganiko na mwanaye. Jambo hili hutimilika kabisa, hasa kama umemtendea jambo baya na kumsononesha.
Itoshe sasa kusema kuwa, iko sababu kwa nini sio vema hata kidogo kuoa/kuolewa kwenye familia ambayo mama ndio kila kitu. Watoto huwa na muunganiko wa hatari na mama yao, kiasi kwamba lazima atayumbisha ndoa za wanaye vibaya sana!
Kwa upande wa wanaume, hicho kitu ni nadra sana, kwani mtoto wa kike akiwa karibu mno na baba, hata jamii hutilia shaka kwamba huenda ni wapenzi. Lakini hata wakiwa karibu sana basi sio rahisi baba kuingilia ndoa za wanaye, hii ni sekta ya wamama. Mara nyingi ukiona baba anaingilia kati ugomvi wa kawaida tu baina ya binti na mumewe huwa kuna shaka huenda aliwahi kumwingilia akaweka nafsi yake humo. Yaani mpaka binti anageuka agent wa baba kwamba kila mkipishana kauli kidogo tu anampigia simu, na baba naye anakuja kufoka na kutoa vitisho vingi kwa mume. Vinginevyo itakuwa ni kiburi cha nje kama utajiri, kazi nzuri aliyonayo, nafasi yaje serikalini nk.
Kwa upande wa watoto wa kiume, mara baba huwa anasimama upande wa muolewaji, na hii ndio hekima. Ni aibu kubwa kukuta baba na mwana wanamchangia binti mwolewaji kumshambulia kwa matusi. Lakini ni jambo la kawaida mama na Mwana kumvaa binti kwa na sababu kubwa ni mama kuwa rubani wa familia na hivyo watoto wamelelewa hivyo. Mtoto aliyelelewa vyema, hata kama mke amekosea vipi hawezi kamwe kusimama na mama yake wakimtukana na kumpiga. Mwanamume huyu atafanya kila linalowezekana kumtuliza mama kisha atatafuta jinsi ya kusuluhisha mambo. Soul tie inamfanya mama aamini kuwa ana haki ya kuendesha maisha ya wanaye pia na watoto nao wanaamini mama ana wajibu huo!!
Kuishi kama mapepo
Kwa kawaida mapepo huzunguka huku na kule na kukivaa chochote kilichotoa nafasi. Ndivyo alivyo mwanamume ambaye anatembea na wanawake mbalimbali na kuwatenda na kuondoka. Atajiona anaishi sawa lakini kwa sababu ya laana ya wadada aliowaumiza, mambo mengi yatakuwa yanavurugika yakikaribia kufanikiwa. Atakuwa hana kituo maalum, hata wakati akiona mambo yanakaribia kuwa safi ghafla yanaharibika.
Mbaya zaidi ni pale mtu anapofungamana na pepo (spirit). Mfano jini mahaba, haya humvaa mtu mzinzi ama aliyeacha roho yake isiwe na kinga yoyote na kisha kufunga naye soul tie kiasi kwamba hakuna jambo atakalofanya litafanikiwa bila kuliomba na kulitolea kafara. Mwanamke ama mwanamume mwenye pepo wa ngono hawawezi kuwa na ndoa imara. Hata wakifunga ndoa hazidumu, ama waweza kufunga ndoa ikawa kila mimba inaharibika, maana yake yanachukua hizo mimba. Soul tie na mapepo ni hatari zaidi.
Itaendelea........ [/B][/B]