moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,900
- 4,865
Kifungu cha 61(1)(v) Cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002, kinampa mamlaka waziri wa Elimu kutunga kanuni za masuala mbalimbali zitakayokidhi utekelezaji wa masuala ya sheria hiyo.
Mojawapo ya kanuni zilizotungwa ni The Education (Corporal Punishmemt ) Regulation G.N.294 ya mwaka 2002.
Kanuni hizi zinatoa mwongozo ni wakati gani adhabu ya viboko inatakiwa kutolewa na kwa kiwango gani kanuni ya 3(1) inasema athabu ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhabu au kosa kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule amabalo litailetea litaishushia shule heshima.
Kanuni ndogo ya (2) inasema adhabu ya viboko itolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya mwanafunzi na isizidi viboko 4 kwa tukio lolote.
Nani Ana mamlaka ya kumchapa mwafunzi.
Sheria inamtaka mwalimu mkuu wa shule husika kutoa adhabu ya viboko au kukasimisha mamlaka yake kwa umakini mkubwa kwa mwalimu yeyote kutoa adhabu hiyo.Mwalimu anayechaguliwa kutoa adhabu atakuwa na mamlaka ya kutoa adhabu pale tu atakapopata idhini ya mwalimu mkuu katika tukio husika.
Kanuni ya (5) inataka kila adhabu ya viboko inapotolewa kwa mwanafunzi kumbukumbu ya kutolewa kwa adhabu hiyo sharti iwekwe kwenye kitabu, ikitaja jina la mwanafunzi,kosa alilolifanya,idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu. Na kumbukumbu hizo lazima zisainiwe na Mkuu wa shule.
MY TAKE :
Walimu tusiongozwe na hasira katika kuadhibu watoto kwa makosa ambayo pengine hayahitaji adhabu ya viboko.