Ijue sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyopiganwa Sudan kwa sasa

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,007
Tokea mwaka 1958 sudan yameshatokea majaribio almost 36 ya kupindua serekali kwa lugha nyepesi sudan ni moja ya nchi ngumu sana kuiongoza afrika

Mwanzon wa miaka ya 2000 kulikua na vuguvugu la waasi darfur rais wa wakati huo omar al bashir alianzisha janjaweed ambao ni kama kikosi maalumu kwa ajili ya kupigana na waasi wa darfur kumbuka janjaweed ni sehemu iliyotolewa kwenye jeshi la sudan na ilikua ikiongozwa na hemedti

Janjaweed ambao baade ndo ikaja badilisha jina na kuitwa rapid support force walikua na kazi ya kuwadhibiti waasi wa darfur na kulinda mipaka ila baadae walianza kufanya biashara zenye ela kama kuuza silah, gold na kushiriki kama mamluki kutoka na hii ilipelekea kiongozi wao hemedti kuwa na ukwasi wa kutosha vyanzo vingine vinasema ni billionaire

Vuguvugu la sudan kusin lilishika hatama na mwaka 2011 wakapata uhuru hii ilikuwa pigo kubwa kwa sudan sababu asilimia 75 ya visima vya mafuta vilienda sudan kusin ambayo ni nchi mpya huku sudan imibakiwa tu na asilimia 25 ya visima vya mafuta

Hali ya uchumi sudan haikua nzuri tena ilikua mbaya na mnamo mwaka 2019 kiongozi wa janjaweed ambayo baade ilijulikana kama rapid support force aliungana na kiongozi wa jeshi wa sudan al burhan wakampindua al bashiri

Baada ya kumpindua al bashiri ikabid hao makanda wawil wahandover madaraka kwa kiongozi wa kiraia, tatizo lilianza pale al burhan alipotaka rapid support force iwe integrate na jeshi la sudan mapendekezo haya yalipingwa vikali sana na hemedti sababu uwepo wa rapid support force ulimfanya kuuza silaha, gold na kupeleka wanajeshi kupigana kama mamluki kwenye nchi kama yemen, libaya n.k kote huko alikua anapata ela nyingi kwa hiyo ilimfanya kuwa tajiri sana sasa kuja kumwambia rapid support force ife ni sawa na kumwagia kitumbua mchanga

Baada ya hiyo sintofahamu ndo ilapelekea power struggle kati ya al burhan na hemedti na matokeo yake vita ambavyo tunaviona leo matokeo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni matoke ya legacy ya al bashiri
 
Attachments

  • 94DB962C-1CAF-4153-8773-177519045D52.jpeg
    94DB962C-1CAF-4153-8773-177519045D52.jpeg
    112.2 KB · Views: 12
Umeeleza sahihi ila umezunguruka sana mwana JF mwingine hatokuelewa kwa kifupi serikali ya sudani ni mshirika Wa Russia na wakakubaliana Russia aweke navy base baharini kitendo ambacho USA hapendi akachomeka mamruki wakipewa supported na CIA . vita imekuwa ngumu sana kwa kuwa upande Wa serikali kuna Wagner military (RUSSIA) upande Wa waasi wapo CIA (USA)
 
Al burhan ni kiongozi wa jeshi la serekali huku henedti ni kiongozi wa jeshi la rapid support force
Sasa nikuulize swali muasi ni nani hapo
 
Umeeleza sahihi ila umezunguruka sana mwana JF mwingine hatokuelewa kwa kifupi serikali ya sudani ni mshirika Wa Russia na wakakubaliana Russia aweke navy base baharini kitendo ambacho USA hapendi akachomeka mamruki wakipewa supported na CIA . vita imekuwa ngumu sana kwa kuwa upande Wa serikali kuna Wagner military (RUSSIA) upande Wa waasi wapo CIA (USA)
umekosea kuelezea...

RSF sio waasi, ni sehemu ya Taasisi za Serikali na ipo kwa mujibu wa Sheria na katiba ya Sudan... na ni sehemu ya vyombo vya ulinzi na usalama.

RSF ndio wanaushirikiano na Wagner, Marekani kwa upande wake amekuwa mpatanishi mkuu bila kujali Jeshi kuu au RSF sababu anamini anaweza kuleta democracy.

RSF wanasuportiwa na Qatar, Saudia, Libya na Wagner kwa sababu ya kutoa Askari na kusafirisha magendo ya dhahabu.

Wote Al Burhan na Hemedti wana nguvu za kipesa na kijeshi na wanatumia majeshi yao kukwepa kuwajibika kwa makosa yao huko nyuma...

Kama Janjaweed ina makosa basi wakati wote huo walikuwa wanashirikiana na Jeshi la nchi
na wakuu wake wote walikuwa wanafanya operation zao pamoja.

Al Burhan na Hemedti wana marengo na ndoto za Kisiasa... na wote wanajua kuwepo kwa majeshi haya mawili kinamuondolea mmoja wapo nguvu zote kama akiwa mkuu wa nchi...

Mwisho hakuna nchi inaweza kuwa na majeshi mawili yenye nguvu sawa alafu isije kupigana.

Iran, Russia is loading...
 
Back
Top Bottom