G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Wakati wa utawala wa JK, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje ndugu Benard Membe alikuwa akipinga waziwazi hatua za aliyekuwa waziri mwenzake ambaye sasa ni rais ndugu John Pombe Magufuli dhidi ya makampuni mbalimbali ya kimataifa. Miongoni mwa hatua hizo zilikuwa zikiangaliwa na bwana Membe kama kichocheo cha uhasama kati ya Tanzania na mataifa mengine.
Hali hiyo ilifanya mawaziri hao kuwa na tofauti za waziwazi kwani Membe alikuwa akipinga kuharibiwa kwa diplomasia ya nchi kutokana na hatua hizo ikiwemo kusitisha mikataba ya kazi kienyeji. Hali hiyo ilifanya wawili hao kutokuwa na uhusiano mzuri na hadi sasa wako hivyo. Katu hakuna ushirikiano wowote anaotoa ndugu Membe kwa utawala huu wa Magufuli ingawa anaelewa vyema mambo mengi ya nchi yetu dhidi ya mataifa ya nje.
Je Membe alikuwa sahihi? Vipi matokeo yake kwa sasa?