Ijue nchi ya Madagascar

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
597
2,225
Jamhuri ya Madagascar ni nchi ya visiwa (island country) vidogo na vikubwa vinavyopatikana katika bahari ya Hindi vikiwa na ukubwa wa square mita 228,900.

Madagascar ni nchi ya kisiwa namba mbili kwa ukubwa duniani ikitanguliwa na Indonesia.

Huku kisiwa cha Madagascar pekee kikishika namba nne kwa ukubwa duniani ikitanguliwa na visiwa vya Greenland, New Guinea na Borneo.

Naomba hapa niwaeleze kitu kimoja kisiwachanganye.

JAMHURI YA MADAGASCAR ni muunganiko wa visiwa vya Madagascar na visiwa vyengine (kwahyo kuna visiwa vidogo vidogo na kisiwa cha Madagascar ambavyo kwa pamoja ndio inaitwa JAMHURI YA MADAGASCAR) jamhuri ya Madagascar kama Nchi ya kisiwa inashika namba mbili kwa ukubwa duniani ikitanguliwa na Indonesia.

Lakin Madagascar kama miongoni mwa visiwa vinavyounda nchi ya Madagascar ndio inashika namba nne kwa ukubwa duniani.

Mji mkuu wa Nchi ya Jamhuri ya Madagascar ni Antananarivo ambao hadi kufikia mwaka 2015 ilikuwa na zaidi ya watu Million 2.

Kwa ujumla Jamhuri ya Madagascar ina zaidi ya watu Million 26.

Raisi wa nchi hiyo anaitwa Andry Rajoelina
Lugha yao ni kimalagarasy na kifaransa.

1) Zaidi ya Miaka Milion 160 ndio kisiwa cha Madagascar kilijitenga na bara la Africa

2) Wamalagalasi wana asilimia kubwa la chimbuko kutoka nchi za kusini mashariki mwa bara la Asia. Hata tamaduni zao zinaendana kwa kiasi Fulani

3)Madagascar ni miongoni mwah nchi masikini duniani

4) Madagascar ilianza kukaliwa na watu tokea miaka 300000 iliyopita

5) Licha ya kuwa Madagascar ni nchi ya kisiwa lakini ina idadi kubwa ya watu kuliko nchi za uholanzi, ugiriki, Sri Lanka, Australia

6)Madagascar kuna wanyama na ndege aina nyingi ambazo huwez kuzikuta sehemu nyengine duniani, karibia asilimia 70 wanaopatikana Madagascar hawapatikani sehemu nyengine

7) Nchi ya Madagascar ilianza kukaliwa na watu kutoka asia kabla ya waafrika

8)Kabla ya uvamizi wa wafaransa, Madagascar ilikuwa ikitawaliwa na Mwanamke.

Malkia Ranavalona III ndio alikuwa mtawala wa mwisho wa kifalme alianza kutawala kuanzia mwaka 1883 -1897 baadae akaondolewa na wafaransa

9) Mimea mingi ya Madagascar inatumika kwa tiba mbali mbali ipo hadi mimea inayotumika kutengenezea dawa za kutibu Aina fulani ya kansa

10) Katika miaka ya 1700 eneo la Madagascar lilikuwa kitumiwa na maharamia yalikuwa yanapendelewa kukaliwa name maharamia kutoka Ulaya na Asia ambapo waalifikia hatua ya kujitangaza kama nchi waliyoipa jina la Libertalia (nchi huru ya maharamia)

11) Vyakula vinavyoliwa katika nchi ya Madagascar ni mchanganyiko wa mapishi kutoka kusini mashariki mwa bara la asia, ulaya, China, afrika na India.

Hii imesababishwa na kuwa watu hao waliishi katika nchi hiyo

12) Lamba ndio vazi la asili la Madagascar ambalo huvaliwa na wanawake na wanaume

13) Asilimia kubwa ya Wamalagasy ni wakristo lakin bado wanaimani na dini zao za kale. Bado wanaamini katika mungu wao wanaoamini ndio aliyeumba dunia. Mungu huyo anaitwa Zanahary

14) Moraingy ndio mchezo wa wamalagasy ...moraingy ni kama boxer ila sema kwenye mchezo huu watu wanapigana bila kuvaa gloves

15) Kwa sasa dunia ina mabara 7 lakini wengi huita Madagascar kuwa ni bara la 8 duniani

16) Karibia nusu ya vinyonga wanaweza kupatikana Katika nchi ya Madagascar pia wanapatika wanyama aina ya lemurs

17) Madagascar ni miongoni mwa nchi maskin duniani
 
Back
Top Bottom