Ijue Historia ya Kabila la Wapare

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,289
2,000
Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare Mkoa wa Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania. Lugha yao ni Kipare au Chasu).

Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni,Himo,Mabungo,Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka hapa nchini,Afrika na dunia nzima kwa ujumla kutokana na suala la utandawazi wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali kwa mfano jamii kubwa ya wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi na hali imekuwa katika mikoa yote hapa nchini na kwingineko. Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita,Taveta,Ukamba.

Ni kabila la watu wachache lakini wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania. Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).Ndio maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi,bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.Utawasikia watu wengine wakidai kuwa mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.

Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa.

Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi anaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.

Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisherani wa Kikiristo waliingia maeneo mengi ya Upare.

Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru,Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisla la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisala la Kiluteri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Waluteri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.

Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga manake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baade na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale.

Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mvungi,Msuya,Mgonja etc, wana asili ya maeneo yao kama Bwambo,Mjema,Usangi,Vungi,Suya,Gonja etc.

Mifano ya majina ya watoto wakipare.

Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)

Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Mwajuma Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Namangi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.

Majina ya kiume:

Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli,Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibariki,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo ,Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio,Lukungu, Lusingu, Macha (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (Jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (Jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni Ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (Jina hili lipo pia kwa wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha mtafuta mali), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (Jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (Jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Tenshigha, Teri,Twazihirwa,Warema,Zihirwa, Zihirwani.

Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.

Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikwepoa hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa mapumziko na matukio fulani.Hali hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima madiwa Jacob Steven( JB ) ,Sinta,Sara Mvungi,Roma Mkatoliki na wengineo wengi.

Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,kirutu n.k ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika.Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.

Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande(mchanganyiko wa mahindi na maharage).Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze kupumzika vizuri mwisho wa wiki bilaa kuwaza masuala ya upishi.Samaki pia ni kipenzi cha wapare wengi na ndio maana utawasikia watani wao wakuu yaani wachaga wakiwatainia kuwa wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki wakimaanisha kuwa ni wabahili.Wakati mwingine utawasikia wapare wenyewe wakisema "ipere ethi kindu,kindu ni mshombe"kuwa samaki si kitu kitu ni mchuzi kuonesha ubahili wao kuwa samaki anayebaki atumike tena wakati mwingine bqaada ya mchuzi kuisha.

Maeneo ya wapare yamekuwa na mvuto wake mfano katika milima ya upareni kwenye maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari ya kijani kibichi yanavutia japo shughuli za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu mazingira ya upareni kadhalika.Kuna maeneo yanayovutia kama milimani(Usangi,ugweno,misitu ya shengena n.k.Pia skimu ya umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga.Pia kuna mwamba wa kuvutia Same unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama ikamba la fua.

Kama ilivyo kwa makabila mengine wapare nao wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya ya elimu,siasa na uchumi.Zipo shule nyingi za zamani na mpya katika maeneo ya wapare.Mazao ya chakula na biashara kama mpunga,katani,mahindi n.k zimeinua maendeleo ya uchumi.Pia Miundo mbimu kwa kiasi chake imeboreshwa,kuna mabasi ya Kilenga yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro,pia magari yafanyayo safari za mikoani kama Ngorika Kwa upande wa siasa wapo pia wapare ambao wamepiga hatua kubwa katika nyanja ya siasa kama Mh.Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu,Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe na pia Waziri,na wengineo wengi kama Anna kilango Malechela,Pro.Jumanne Maghembe,Michael Kadeghe n.k Pia Mheshimiwa Chediel Yohane Mgonja aliyewahi kuwa mwnasiasa maarufu hapa nchini(waweza ongeza).
 
Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,077
2,000
[h=1]Wapare
[/h]

Wapare ni kabila kutoka milima ya
Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini ya nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kipare (au Chasu).

[h=2] [/h] Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni, Himo, Mabungo,Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka hapa nchini,Afrika na dunia nzima kwa ujumla kutokana na suala la utandawazi wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali kwa mfano jamii kubwa ya wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi na hali imekuwa katika mikoa yote hapa nchini na kwingineko. Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita, Taveta na Ukamba. Ni kabila la watu wachache lakini wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania[SUP][/SUP]. Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).Ndio maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi,bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.Utawasikia watu wengine wakidai kuwa mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.

Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa.Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi anaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.

Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisherani wa Kikiristo waliingia maeneo mengi ya Upare.

Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru,Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisla la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisala la Kiluteri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Waluteri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.

Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga manake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baade na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale

Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mvungi,Msuya,Mgonja etc, wana asili ya maeneo yao kama Bwambo,Mjema,Usangi,Vungi,Suya,Gonja etc.

[h=2] Mifano ya majina ya watoto wakipare[/h] Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)

Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Mwajuma Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Namangi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli,Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibariki,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo ,Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio,Lukungu, Lusingu, Macha (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (Jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (Jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni Ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (Jina hili lipo pia kwa wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha mtafuta mali), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (Jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (Jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Tenshigha, Teri,Twazihirwa,Warema,Zihirwa, Zihirwani.

Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.
Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikwepoa hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa mapumziko na matukio fulani.Hali hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima madiwa Jacob Steven(JB),Sinta,Sara Mvungi,Roma Mkatoliki na wengineo wengi
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,kirutu n.k ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika.Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande(mchanganyiko wa mahindi na maharage).Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze kupumzika vizuri mwisho wa wiki bilaa kuwaza masuala ya upishi.Samaki pia ni kipenzi cha wapare wengi na ndio maana utawasikia watani wao wakuu yaani wachaga wakiwatainia kuwa wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki wakimaanisha kuwa ni wabahili.Wakati mwingine utawasikia wapare wenyewe wakisema "ipere ethi kindu,kindu ni mshombe"kuwa samaki si kitu kitu ni mchuzi kuonesha ubahili wao kuwa samaki anayebaki atumike tena wakati mwingine bqaada ya mchuzi kuisha.
Maeneo ya wapare yamekuwa na mvuto wake mfano katika milima ya upareni kwenye maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari ya kijani kibichi yanavutia japo shughuli za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu mazingira ya upareni kadhalika.Kuna maeneo yanayovutia kama milimani(Usangi,ugweno,misitu ya shengena n.k.Pia skimu ya umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga.Pia kuna mwamba wa kuvutia Same unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama ikamba la fua.Kama ilivyo kwa makabila mengine wapare nao wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya ya elimu,siasa na uchumi.Zipo shule nyingi za zamani na mpya katika maeneo ya wapare.Mazao ya chakula na biashara kama mpunga,katani,mahindi n.k zimeinua maendeleo ya uchumi.Pia Miundo mbimu kwa kiasi chake imeboreshwa,kuna mabasi ya Kilenga yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro,pia magari yafanyayo safari za mikoani kama Ngorika Kwa upande wa siasa wapo pia wapare ambao wamepiga hatua kubwa katika nyanja ya siasa kama Mh.Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu,Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe na pia Waziri,na wengineo wengi kama Anna KIlango Malechela,Pro.Jumanne Maghembe,Michael Kadeghe n.k Pia Mheshimiwa Chediel Yohane Mgonja aliyewahi kuwa mwnasiasa maarufu hapa nchini(waweza ongeza).

Waweza ongeza kuiedit ili kuiweka historia ya wapare vyema na kujua tulipotoka na sasa Wapare wapo wapi kwani vitu vingi vimebadilika.Edit na kuongeza historia unayoifaham ukiwa na uhakika ili ikae mtandaoni wikipedia

Ni historia nzuri sana, naamini kila mpare atampa na mwanae asome angalau aelewe asili yake.

Tafadhali kati ya viongozi wakuu ktk nchi hii kutoka kabila hili la wapare usimsahau mzee MSANGI NARUNDU ELANGWA SHAIDI yeye alikuwa ni Inspector General wa Police (IGP) wa kwanza Tanzania, akitokea Vudee na Chome kule Same. Pia kulikuwa na mzee Elifadhili Shaidi Mchome, huyu alikuwa kati ya makamishna wa kwanza wa Magereza na alianzisha Chuo cha Magereza Kiwira 1980's.

Bless you.

Queen Esther
 
Askari wa miguu

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
333
0
Ni historia nzuri sana, naamini kila mpare atampa na mwanae asome angalau aelewe asili yake.

Tafadhali kati ya viongozi wakuu ktk nchi hii kutoka kabila hili la wapare usimsahau mzee MSANGI NARUNDU ELANGWA SHAIDI yeye alikuwa ni Inspector General wa Police (IGP) wa kwanza Tanzania, akitokea Vudee na Chome kule Same. Pia kulikuwa na mzee Elifadhili Mchome, huyu alikuwa kati ya makamishna wa kwanza wa Magereza na alianzisha Chuo cha Magereza Kiwira 1980's.

Bless you.

Queen Esther

Bila Kumsahau Gray Mgonja aliyekuwa katibu mkuu Wizara ya Fedha. Aliekaribia kuibadilisha Hazina kuwa 'Hazimo'
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,556
2,000
Askofu Elinaza Sendoro, Balozi Ombeni Semfue.

Wapare wanapenda majina yao.

Kwa nini majina ya kike mengi yanaanza na Na- ? Is that some significant prefix?
 
MasaiSupai

Senior Member
Jan 18, 2013
109
0
isisahau Msuya, Waziri Mkuu aliefanya Party ya hali ya Juu baada ya Hayati Sokoine kupata ajali na Kufa, kisha kawahamisha Wamasai kinyama Kilimanjaro pale alipoanzisha kwa Makusudi Mkomazi National Park. wamama walibakwa, miji kuchomwa, ng'ombe kufukuzwa kwa Helikopta. ndio wamasai unaowaona Mbeya hadi Zanzibar. njama ya Msuya Mkoa Kilimanjaro wasiwepo Wamasai
 
mathabane

JF-Expert Member
Jan 27, 2013
2,227
2,000
Wapare
Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini ya nchi ya Tanzania. Lugha yao ni Kipare (au Chasu).

Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni, Himo, Mabungo,Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka hapa nchini,Afrika na dunia nzima kwa ujumla kutokana na suala la utandawazi wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali kwa mfano jamii kubwa ya wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi na hali imekuwa katika mikoa yote hapa nchini na kwingineko. Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita, Taveta na Ukamba. Ni kabila la watu wachache lakini wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania. Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana. Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu).Ndio maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi,bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii.Utawasikia watu wengine wakidai kuwa mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.

Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe,mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga,na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa.Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya Wafugaji na Wakulima. Wakati Wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, Wakulima wao waliishi milimani na wafuaji wa vyuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma. Kwa asili Wapare hupeleka vijana wakiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia,japo siku hizi tamaduni za kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache. Hata hivyo wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati wasangi anaongea kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyika wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni uchagani japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya uchaga wala upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na wapare,pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya wapare pamoja na wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za wapare wengine.

Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndio maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania. Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti,kwa kila koo na eneo lao la tambiko, katika karne ya 19 hadi 20 wamisherani wa Kikiristo waliingia maeneo mengi ya Upare.

Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo, walio Kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu,Kihurio,Bendera,Hedaru,Makanya,Suji,Chome,Tae,Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisla la Sabato wengi sana,maeneo kama Chome,Mbaga,Gonja, Vudee yana waumini wengi wa kanisala la Kiluteri, Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Waluteri na Waislamu. Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara juu, Vumari, na Mbaga.

Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile hata majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila kama vile Wasambaa na Wanguu. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.

Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga manake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baade na walipotaka kuishi na wachagga ndipo vita ikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au watu wanaotumia mishale

Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao,mfano Mbwambo,Mjema,Msangi,Mgweno,Mvungi,Msuya,Mgonja etc, wana asili ya maeneo yao kama Bwambo,Mjema,Usangi,Vungi,Suya,Gonja etc.

Mifano ya majina ya watoto wakipare

Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)

Ingiahedi, Itikija, Kafue,Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha,Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Mwajuma Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa,Namkunda,Nabera,Namangi,Nangasu,Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa,Shode, Yunesi.Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli,Chuma, Elieseri, Eliesikia,Elinighenja,Elibariki,Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa),Kalutu, Kambaita (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (Jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (Wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo ,Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio,Lukungu, Lusingu, Macha (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (Jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (Jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni Ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (Jina hili lipo pia kwa wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha mtafuta mali), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (Jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (Jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (Jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (Jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni Ukoo), Tenshigha, Teri,Twazihirwa,Warema,Zihirwa, Zihirwani.

Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofauti tofauti.

Tamaduni,mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote.Hapo kale wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi jambo ambalo wapo baadhi ya wapare ambao mpaka leo wanaweza.Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga maarufuku utawala wa jadi.Kiongozi huyu aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.Pia walikwepoa hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo.Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama siyo kuisha kabisa.Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalum kama kwenye jando au unyago,pia nyimbo za kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika.Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali,hadithi,maigizo n.k wakati wa mapumziko na matukio fulani.Hali hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima madiwa Jacob Steven(JB),Sinta,Sara Mvungi,Roma Mkatoliki na wengineo wengi
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu,kirutu n.k ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika.Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande(mchanganyiko wa mahindi na maharage).Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze kupumzika vizuri mwisho wa wiki bilaa kuwaza masuala ya upishi.Samaki pia ni kipenzi cha wapare wengi na ndio maana utawasikia watani wao wakuu yaani wachaga wakiwatainia kuwa wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki wakimaanisha kuwa ni wabahili.Wakati mwingine utawasikia wapare wenyewe wakisema "ipere ethi kindu,kindu ni mshombe"kuwa samaki si kitu kitu ni mchuzi kuonesha ubahili wao kuwa samaki anayebaki atumike tena wakati mwingine bqaada ya mchuzi kuisha.
Maeneo ya wapare yamekuwa na mvuto wake mfano katika milima ya upareni kwenye maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari ya kijani kibichi yanavutia japo shughuli za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu mazingira ya upareni kadhalika.Kuna maeneo yanayovutia kama milimani(Usangi,ugweno,misitu ya shengena n.k.Pia skimu ya umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga.Pia kuna mwamba wa kuvutia Same unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama ikamba la fua.Kama ilivyo kwa makabila mengine wapare nao wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya ya elimu,siasa na uchumi.Zipo shule nyingi za zamani na mpya katika maeneo ya wapare.Mazao ya chakula na biashara kama mpunga,katani,mahindi n.k zimeinua maendeleo ya uchumi.Pia Miundo mbimu kwa kiasi chake imeboreshwa,kuna mabasi ya Kilenga yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro,pia magari yafanyayo safari za mikoani kama Ngorika Kwa upande wa siasa wapo pia wapare ambao wamepiga hatua kubwa katika nyanja ya siasa kama Mh.Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu,Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe na pia Waziri,na wengineo wengi kama Anna KIlango Malechela,Pro.Jumanne Maghembe,Michael Kadeghe n.k Pia Mheshimiwa Chediel Yohane Mgonja aliyewahi kuwa mwnasiasa maarufu hapa nchini(waweza ongeza).

Waweza ongeza kuiedit ili kuiweka historia ya wapare vyema na kujua tulipotoka na sasa Wapare wapo wapi kwani vitu vingi vimebadilika.Edit na kuongeza historia unayoifaham ukiwa na uhakika ili ikae mtandaoni wikipedia

Huu utumbo hauna tija kwa watanzania. Nakushauri uhamishie PAREFORUMS .
 
Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,077
2,000
Huu utumbo hauna tija kwa watanzania. Nakushauri uhamishie PAREFORUMS .

Mathabane, mbona unahasira hivyo mpendwa? Una maana somo la HISTORIA liondolewe kwenye mitaala ya elimu? Historia ya wapare ni sehemu tu ya historia ya TZ.

Uwe na amani na usiharibu siku yako kwa mambo madogo kama haya. Au kuna mpare alikukwaza umeamua kukasirikia wote? Kama ndio hivyo basi samehe Saba mara sabini.

Queen Esther
 
Dr. Wansegamila

Verified Member
Feb 3, 2012
2,228
2,000
That is very nice............ i like it, wapare ni wakwe zangu, hivyo its interesting for me
 
Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,077
2,000
Askofu Elinaza Sendoro, Balozi Ombeni Semfue.

Wapare wanapenda majina yao.
Kwa nini majina ya kike mengi yanaanza na Na- ? Is that some significant prefix?

Kirang, Itabidi the Hammer aje aeleze vizuri maana hata mimi nimeshangaa.
Queen Esther
 
MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,471
2,000
Ni kwanini majina ya ukoo ya kipare yote yanaanza na herufi M halafu herufi inayofuata haiwi ktk (a,e,i,o,u)?

Mfano: Msuya, Msangi, Mmbaga, Mchome, Mjema, Mdee, Mgonja, Mfinanga, Msofe, Mzava, Mbwambo, na mengine mengi.

Na kwanini Wapare hupenda kuishi sehemu zenye asili ya jangwa (mahali pakame) penye shida ya maji?

kama mwanga, same, rundugai, chereni, kahe, uchira na kwingineko kwenye hali kama hiyo.
 
zitafute

Member
Jan 13, 2013
23
0
maeneo mengine ya kuvutia ni kama ziwa Jipe na msitu 'unaolia' Usangi
By The Way, sidhani kama hii thread imekaa kikabila, hakuna ubaya kujifunza historia ya makabila ya TANZANIA ilimradi hakuna mtu aliyekashifiwa.
 
MAGUNJA

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
1,006
1,500
Nimeipenda Hii Historia. Niliwahi kuona kitabu kimoja kimeandikwa MILA NA DESTURI ZA WAPARE. Kina mengi sana japo sikukisoma chote. Mweka thread na wachangiaji hebu wekeni methali au nahau za kipare mnazozikumbuka! Nami najaribuu kuzitafuta.
 
mdoe

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
434
170
Hua nawatania wapare kua, Hawawezi kuishi maeneo ambayo ni Tambarare na yenye maji ya kutosha na rutuba. wana aleji na mazingira kama hayo. ndio maana utawakuta milimani na kama ni tambarare basi pana hali ya Jangwa. Ila kiasili ni wacheshi na wana utani mwingi sana hasa wakiongea kipare. Ni wachapa kazi sana, Japo nyingi ni zile zisizotumia akili nyingi. Wengi ni wafupi nadhani ni kutokana na mazingira magumu wanayoishi. mfano, angalia viumbe wote wanaoishi kwenye harsh enviroment, wengi sio warefu. Miti ya same na maeneo ya mwanga ni mifupi, hivyo wangekua warefu kivuli kwao ingekua big issue. Nawapenda sana wapare na mimi Mama mpare na Baba Mchagga.
 
kilio changu

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
408
0
Baadhi ya maeneo ya Wapare ni makame lakini pamoja na ukame huo wanafurukuata, yaani pamoja na ukame wao bado wanaendelea. Wapare ni wachapa kazi sana, kuanzia kilimo mpaka kufuga,kusoma na biashara.

Wanaakili sana japo wengine ni wanakashfa za ufisadi kama Gray Mgonja, Daniel Yona, lakini wapo wapambanani na watetei wa haki za wengi mfano Dr Hellen Kijo Bisimba (HLRC), John Mnyika (CHADEMA) Halima Mdee (CHADEMA).

Ni vema pawepo na historia ya makabila ya Tanzania ili watu wafahamu asili yao na utamaduni wao na kujifunza jinsi gani waliweza kuishi na makabila tofauti na wao ili wadumishe udugu ambao umekuwa miongoni mwetu

Na hichi ndio kilio changu
 
MR. ABLE

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,471
2,000
Nimebahatika kuishi na wapare kwa muda mrefu kiasi kwamba ninaijua vizuri sana lugha yao (hawawezi kunisema).

Ninachotaka kujua ni kwanini hupenda kutumia lugha yao kumsengenya mtu? Yaani ukibahatika kukaa mahali wapare wanazungumza kipare utagundua wanamsema mtu.
 
kilio changu

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
408
0
Nilisoma na vijana wa Kipare, walikuwa na akili sana, walikuwa na miili midogo na weupe weupe hivi. Walikuwa na akili sana darasani lakini pia walikuwa wabahili sana, kuna mmoja walisema baba yake ni tajiri lakini jamaa alikuwa bahili sana na anaishi maisha ya mwanafunzi wa kawaida sana.

Lakini kingine ni wabishi, wakiamini kitu chao ni wabishi kubadilika.
 
ngaranumbe

Senior Member
Apr 16, 2012
148
0
kwa umbea, wivu na ushirikina ni kiboko. Usipange karibu na mpare hata nguo za ndani huzishughulikia. Wapare hufunga mvua zisinyeshe ili mazao yakauke ng'ombe wao wapate chakula, ovyo tu. Thi, thi,thi,thi,thi ila ni wazuri kwa sura 70-70%, tabia 1-2%
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom