Ijue Historia ya Kabila la Wapare

Ni historia nzuri sana, naamini kila mpare atampa na mwanae asome angalau aelewe asili yake.

Tafadhali kati ya viongozi wakuu ktk nchi hii kutoka kabila hili la wapare usimsahau mzee MSANGI NARUNDU ELANGWA SHAIDI yeye alikuwa ni Inspector General wa Police (IGP) wa kwanza Tanzania, akitokea Vudee na Chome kule Same. Pia kulikuwa na mzee Elifadhili Mchome, huyu alikuwa kati ya makamishna wa kwanza wa Magereza na alianzisha Chuo cha Magereza Kiwira 1980's.

Bless you.

Queen Esther
Ok yote na mengine yatakayapatikana yataunganishwa.
thnx
 
Askofu Elinaza Sendoro, Balozi Ombeni Semfue.

Wapare wanapenda majina yao.

Kwa nini majina ya kike mengi yanaanza na Na- ? Is that some significant prefix?
Hayo majina ni maneno ya kawaida kama ilivyo masumbuko,Tabu,shida...n.k
mfano jina nakunda=nimependa,pia nakundwa=nimependwa,namkunda=nimempenda......
So yanaendana kulingana na maneno ya kipare yanavyoandikwa na kutamkwa yakiwa na maana ilele ya kiswahili
 
Na kwanini Wapare hupenda kuishi sehemu zenye asili ya jangwa (mahali pakame) penye shida ya maji?

Kama mwanga, same, rundugai, chereni, kahe, uchira na kwingineko kwenye hali kama hiyo.
Hii kama ilivyokuwa ktk historia fupi hapo juu,ni kuwa wachaga na wapare wote ni wahamiaji kutoka sehemu za Kenya ila wote walihamia ktk vipindi tofauti. Wachaga walitangulia na kuchukua sehemu zote zilizokuwa na hali nzuri ya hewa na zenye rutuba hii ikiwa sehemu zote zinazunguka mlima kilimanjaro nk. Hivyo Wapare walivyofika walikuta sehemu zenye hali ya hewa na rutuba nzuri zilishachukuliwa na Wachaga wakajaribu kuchukua kwa mabavu wakashindwa hivyo wakakimbilia milimani na sehemu kame.
 
kwa umbea, wivu na ushirikina ni kiboko. Usipange karibu na mpare hata nguo za ndani huzishughulikia. Wapare hufunga mvua zisinyeshe ili mazao yakauke ng'ombe wao wapate chakula, ovyo tu. Thi, thi,thi,thi,thi ila ni wazuri kwa sura 70-70%, tabia 1-2%

Labda ungesema maeneo gani hayo,sidhani sana kwa ulichosema labda kwa sababu sifaham maeneo yote (vijiji vyote vya huko)ila sijawahi shuhudia ulioyasema
 
Hii kama ilivyokuwa ktk historia fupi hapo juu,ni kuwa wachaga na wapare wote ni wahamiaji kutoka sehemu za Kenya ila wote walihamia ktk vipindi tofauti.Wachaga walitangulia na kuchukua sehemu zote zilizokuwa na hali nzuri ya hewa na zenye rutuba hii ikiwa sehemu zote zinazunguka mlima kilimanjaro nk.Hivyo Wapare walivyofika walikuta sehemu zenye hali ya hewa na rutuba nzuri zilishachukuliwa na Wachaga wakajaribu kuchukua kwa mabavu wakashindwa hivyo wakakimbilia milimani na sehemu kame.

The hammer,

kabla hakujawa na wapare kulikuwa na koo ndogo ndogo za wahamiaji toka makabila mbalimbali yakiwemo wataita na wakamba ambazo zilikuwa haziko chini ya uongozi wowote ule unaoeleweka. sasa hao waliopigania ardhi na wachaga ni kati ya hizo koo ndogo ndogo kabla hazijaunganishwa kwa lugha, mila, na matambiko, na kuwa kabila moja, WAPARE.

katika muunganiko huu unaojulikana kama Wapare zipo koo ambazo zina asili ya Uchagani. Ushahidi wa hilo ni kuwepo kwa Wapare wenye majina ya Kichaga. sasa hapo suala zima la Wapare kupigana vita na Wachaga linakuwa ni utata mkubwa.

Mwisho, kuna mahali umeeleza kwamba chakula cha asili cha Wapare ni MAKANDE. Wapare wenyewe hupenda kukiita chakula hicho pure inatamkwa "MP-HURE." Kipo chakula kingine cha Wapare kinaitwa KISHUMBA.
 
Vava wetu weho uko wanga,
Izina lako ligimbikwe,
Vufumwa vwako vuze,
Kikundire chako kifunyanywe kunu he masanga,
sa vuntu chefunyanywa uko wanga,
Utuinke yoo kijo chetu,
Utushighie rando jetu,
Sa vuntu na uswi twevashighia varando vetu,
Usitugere he mighesho,
Mira utukije he ula mvivi,
Ambu vufumwa na nzinya na ngazo,
ni vyako kae na kae,
AMEN.

source: "Lughenjo Lwefuma Wanga"
 
Askofu Elinaza Sendoro, Balozi Ombeni Semfue.

Wapare wanapenda majina yao.

Kwa nini majina ya kike mengi yanaanza na Na- ? Is that some significant prefix?
Majina mengi yana maana na ili kuleta utofauti wa kike na kiume ndipo 'N'' inatangulia katika baadhi.
Sengondo mwanaume, Nankondo mwanamke. Nita edit hayo majina na kutoa maana zake.

Kwa kifupi ni kama vile Upendo na Pendael au labda Joseph na Josephina
 
m nauli za kwnn wapare n wabishi sana na n wabahili?
Sidhani kama ni wabishi, kinachotokea ni kuwa husimamia kile wanachoamini ni sahihi kwao. Mfano, waliungana na kumsimamia mkoloni kuhusu kodi ya mbiru hadi akasalim amri. Sasa huo kama ni ubishi nadhani ni mzuri tu.

Kuhusu ubahili, kuna utani wa wachaga na wapare lakini hasa ni mazingira yao. Wachaga waliwahi kufika na kuchukua maeneo yenye rutuba, wapare walilazimika kuishi maeneo ya milimani. Tofauti zao kimaisha zilichangia sana sehemu moja kuonekana wafujaji na nyingine mabahili.

Tamaduni pia, wakati wachaga wana take risk kama zile za wizi, ujambazi n.k. wapare hawana ujasiri huo.
Unaweza kuona tofauti ya matumizi kutokana na njia za mapato.
 
Ni historia nzuri sana, naamini kila mpare atampa na mwanae asome angalau aelewe asili yake.

Tafadhali kati ya viongozi wakuu ktk nchi hii kutoka kabila hili la wapare usimsahau mzee MSANGI NARUNDU ELANGWA SHAIDI yeye alikuwa ni Inspector General wa Police (IGP) wa kwanza Tanzania, akitokea Vudee na Chome kule Same. Pia kulikuwa na mzee Elifadhili Mchome, huyu alikuwa kati ya makamishna wa kwanza wa Magereza na alianzisha Chuo cha Magereza Kiwira 1980's.

Bless you.

Queen Esther

Queen Esther,

usimsahau Balozi.Daniel Lucas Mfinanga wa Ujerumani na Marekani, na Balozi.Akili Bernard Chaggi Danieli wa Umoja wa Mataifa.
 
Majina mengi yana maana na ili kuleta utofauti wa kike na kiume ndipo 'N'' inatangulia katika baadhi.
Sengondo mwanaume, Nankondo mwanamke. Nita edit hayo majina na kutoa maana zake.

Kwa kifupi ni kama vile Upendo na Pendael au labda Joseph na Josephina

Nguruvi3,

nadhani matamshi sahihi ni Senkhondo na Nankhonda.
 
Mifano ya majina ya watoto wakipare

Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)

Ingiahedi(ingia pazuri) Msianze usisimkwa au kutoa maana tofauti, Gaijin umenisikia!
Itikija(Kibwagizo)
Komkwavi(Mkwavi ni mmasai hapa akimaanisha binti Mkwavi, mwanaume ni Mkwavi)
Mchikirwa( Aliyesusiwa, hapa single mother ndipo hasa,kama mtu kasepa hakuna DNA wewe unaita Mchikirwa)
,Mshinwa( Mwenye haya au haiba), Naanjela(Asifiwaye), Naetwe( Aliyeletwa), Nahuja( Mkimya),
Nakadori( kadogoo), Nakiete( Wasokoni), Nakijwa(Alieyeponywa), Nakunda( Loveness), Nakundwa(Aliyependwa) ,Namkunda(Nimempenda) ,Nangasu( wa sherehe),Nanzano( wa kiangazi) , Narindwa( Nalindwa), Nasero, Nashumbwe, Natujwa( Nimefarijika) , Navuri( wa vuli) ,Nghuhia(Nipokee), Niendiwe( Niliyetafutwa), Nietiwe(Niliyeletewa), Ntevona(Nimeona) n.k

Majina ya kiume:
Bunija( Dumisha) Charema( Kilichoshindikana) , Chedieli( mungu mwema) ,Chuma, Eliesikia(Mungu msikivu) ,Elinighenja(Mungu nisaidie) ,Elibariki(Mungu bariki) ,Elitumaini(Amtumainiye mungu) ,Ghuheni(Chukueni), Gurisha(Aliyeshika hasa katika imani) , Ibwe(Jiwe), Kakore(Kigogo) , (Mbuzi), Mding'i, Mgheni, Mshigheni(Mwacheni), Ngasu(celebrity) , Nzao(Fahali la ng'ombe) , Nziajose(Njia zote), Nziamwe(njia moja), Senzia(Wa ,Twazihirwa(Tumefurahi) Zihirwa(Furaha), Zihirwani(Furahini) n.k.

Majina hayo mengine yametojana na maneno ya dini. Wapare waliandika Bibilia ya lugha yao wakati wa ukoloni na waliweza kwenda kanisani na kusali kwa kutumia biblia yao. Jambo moja la kushangaza, kama ilivyo katika vitabu vya dini, lugha ya kipare katika biblia ni ngumu sana kuielewa hadi apatikane mtu anayeweza kufafanua. Hilo pia lipo katika vitabu vyote vya dini zote vilivyotafsiriwa.

Wapare wana koo na koo zingine zina umaarufu wa aina fulani
Wasuya ni koo ya utawala
Washana ni wahunzi na kama ni kizungu hawa wanaitwa ''smith'' iwe iron smith, Gold smith etc.

Watu wakumbuke kuwa jina Smith kwa kizungu ni koo ya wahunzi.

Wambaga ni maarufu kwa kuleta mvua.

Majina hayo pia yametafsiriwa kiswahili. Kwa mfano Ziharwani kwa kiswahili ni Furahini na aghalabu ukiwa kule kwao utasikia sana jina la Furahini. Pia, Nkundiwe ni kama pendo na siku hizi utasikia sana Pendo au loveness.

Uzuri wa majina haya ya asili ni ile hali ya uasili na maana ya jina.
Hata siku moja hutasikia mtu anaitwa Msuya Mshana, au Mbwambo Mbaga, au Mziray Mdeme. Maana yake ni kuwa haya ni majina ya koo na huwezi kuwa na jina la ukoo kwa ubini wa ukoo.

Ikumbukwe kuwa ukisikia mtu anitwa Msuya, basi lazima anajina kwa wazungu Msuya ni Sir Name.

Kutokana na kuiga majina ya nje sikuhizi utasikia mtu anaitwa Martin Wallace Smith, hii ni sawa na kumuita mtu Msangi Mshana Msuya ambayo haina maana. Hili ni tatizo la waafrika. Tena lipo pande zote.
Kwa waislam mtu atajiita Said Abudulah Kharef, ukiangalia hayo ni majina ya koo.

Mimi napenda sana Majina kama ya akina Kokubanza, kokushubirwa, Navonaiwa, Nkundiwe, senzota, Mahiza( kule nyumbani Tanga), Semahonge, Mhina, Makame, Akida, Shetui, Mchili, Mwakifufule, Mwaigomole, Ng'abi, Odera, Onyango, Mwita, Wambura.

Kule kwetu Kicheba na mjasani Tanga majina ya asili yanatoweka sasa! Mwaka jana nilipofika Magoroto, Mkanyageni na Lusanga hadi Mtindiro nilishangaa majina yamekuwa imported yote.

Just to add spices, thank you mleta mada


.........
 
Nguruvi3,

Sala ya Baba Yetu kwa Kipare hii hapa:

Vava wetu weho uko wanga,
Izina lako ligimbikwe,
Vufumwa vwako vuze,
Kikundire chako kifunyanywe kunu he masanga,
sa vuntu chefunyanywa uko wanga,
Utuinke yoo kijo chetu,
Utushighie rando jetu,
Sa vuntu na uswi twevashighia varando vetu,
Usitugere he mighesho,
Mira utukije he ula mvivi,
Ambu vufumwa na nzinya na ngazo,
ni vyako kae na kae,
AMEN.

source: "Lughenjo Lwefuma Wanga"

Wapare pia walikuwa na gazeti lao linaitwa "Habari za Upare" ambalo lilianzishwa ili kukidhi kiu ya wananchi waliojifunza kusoma kupitia utaratibu wa elimu ya watu wazima.

Kuhusu majina kama Mbwambo, Msangi, Mmbaga, Mkheni, Mjema, hayo ni majina ya ukoo au clans kama vile Waarabu wanavyoitwa Al-Harith, au Al-Mazrui.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3, Wapare pia walikuwa na gazeti lao linaitwa "Habari za Upare" ambalo lilianzishwa ili kukidhi kiu ya wananchi waliojifunza kusoma kupitia utaratibu wa elimu ya watu wazima. Kuhusu majina kama Mbwambo, Msangi, Mmbaga, Mkheni, Mjema, hayo ni majina ya ukoo au clans kama vile Waarabu wanavyoitwa Al-Harith, au Al-Mazrui.
vip hilo gazeti badomlipo na lilianzishwa mwaka gani kama halipo je ni mwaka gani lilitoweka machoni mwa wasomaji wake. Pia ninavyokumbuka wapare ndio wanzilishi wa benk za wananchi
 
Last edited by a moderator:
Queen Esther,

usimsahau Balozi.Daniel Lucas Mfinanga wa Ujerumani na Marekani, na Balozi.Akili Bernard Chaggi Danieli wa Umoja wa Mataifa.

Asante sana Bangusule.
The Hammer ataweka kumbukumbu hizi vizuri pasipo shaka.
Mungu na akubariki.
Queen Esther
 
Du, hiyo aina ya adaptation uliyotoa ni kali (yaani wapare ni wafupi kwa sababu na miti iliyowazunguka ni mifupi?)
anyway ni historia nzuri sana(proud to be a pare)isisahaulike kuwa kwa sasa wapare ni mojawapo ya makabila makubwa hapa Tanzania(yenye watu zaidi ya 1,000,000) kuna makabila mengine ni makubwa kwa majina tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom