Ijue Ajenda ya Siri juu ya Yanga SC 'Kutishia' kutocheza Mechi yao na Simba SC 03 July, 2021

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,752
109,374
Juhudi zangu za Kuchimba kutoka Jikoni nimeambiwa na Mmoja wao kuwa si Kweli kuwa Yanga SC hawataleta Timu Siku hiyo ila Kutishia kwao huku mara kwa mara kutoitambua au kutocheza 'Derby' ni kutaka 'Kuidhoofisha' Klabu ya Simba Kimapato kwakuwa Mechi hii ijayo Simba SC ndiyo Mwenyeji.

Hivyo basi nauomba Uongozi wa Simba SC ulishtukie hili mapema na sasa Msemaji wa Simba SC Haji Manara aanze Kuhimiza wana Simba SC wowote popote pale walipo kuwa muda wa Kununua Tiketi ukifika ( japo nimeambiwa walionunua Kipindi kile watarejeshewa Pesa zao) basi wakate kwa Wingi na 'Waujaze' Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Msidanganywe Yanga SC wataleta Timu.
 
Mapato si yashapatikana tokea ile tarehe ya mwanzo, labda ambao walikuwa bado ambao wataongezea mapato sio kupunguza
 
Mengine yanasema eti janja yao ni kuidhoofisha kambi ya mnyama. Eti wanataka wamfunge mnyama kisaikolojia. Simba wasijiandae wakiamini mechi haitakuwepo.

Wanachokisahau, kikosi cha Simba kinaweza kutokea bar wakiwa wamelewa na bado Utopolo akachezea kichapo hata akiwa kafanya mazoezi ya miezi sita.
 
Nakubaliana nawe kwa hili 100% Mkuu.
 
Leo kuu ni kuidhohofisha simba ktk maandalizi nje ya uwanja, yaani mechi hiyo ni muhimu sana kwa Yanga wakishinda watatamba "sisi hatuna haja na ubingwa, lengo ni kuifunga simba"
 
Stori gani unaleta ,tff na serikali ,waje najibu kwann ilemechi iliahirishwa .kelele zenu acheni.
 
Nakwambia waziwazi yanga hawataleta timu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…