TFF na Bodi ya ligi jifunzeni kutoka CAF kuhusu hao makomandoo wa Simba sc na Yanga SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,288
12,789
Katika mchezo wa Simba sc vs Al ahly siku tatu kabla Kuna kikosi kinachojiita Makomandoo wa Simba sc kilikwenda kuweka kambi kwa dhumuni la kulinda uwanja wa Mkapa.

Juhudi ziligonga mwamba baada ya Maofisa wa CAF kuwazuia hao makomandoo kulinda uwanja.

Hii siyo kwa Simba sc tu hata kwa Yanga sc Hawa huwa wanautamaduni huo wa kulinda uwanja haswa kipindi Cha Dabi ya Kariakoo na mechi za kimataifa.

Swali la kujiuliza Hawa makomandoo huwa wanalinda Nini? Na wakati uwanja una security guards ambao wanalipwa kwa mwezi Sasa hao makomandoo wanakua hawana Imani na hao walinzi kuwa uwanja utaibiwa na timu zao zisicheze?

Jibu ni hakuna Bali kinachoendelea hapo kwenye ulinzi wa makomandoo ni Imani za kishirikina na uchimbaji wa uwanja (uharibifu) hakuna kingine zaidi ya hilo tukubali tukatae.

Maoni Yangu : TFF&,Meneja wa uwanja ipige marufuku timu kuingiza makomandoo wao kabla ya mechi kuanza kwani wanaharibu uwanja mbona CAF walizuia huo UPUUZI (ushuzi) wa makomandoo na wakafanikiwa.
 
UHARO,non sense
 
Hizi pigo zipo sana kwa Simba, hawa si ndo walipigwa faini ya ushirikina kule South Africa? Hovyo sana management ya hii timu.
 
TFF walishazuia hayo mambo kitambo sana, sasahivi timu ikileta makomandoo wanaishia nje tu, hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia uwanjani kama sio mfanyakazi wa uwanja
MAKOMANDOO WA SIMBA NA YANGA HUWA HAWAZUILIKI.
 
Back
Top Bottom