Simba SC ilibugi maeneo haya kiufundi katika kukabiliana na Yanga SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
1/ Aishi Manula hakupaswa kuanza/kucheza kabisa kwa sababu hakuwa na match fitness, japo kuwa benchi la ufundi lilikua na maono ya kumrudisha Aish Manula rasmi katika ligi kutokea Majeruhi lakini hesabu zimekua tofauti na vile benchi la ufundi lilivyoamini/kutegemea Aishi Manula angefanya vizuri katika Derby ya Kariakoo.

2/Ukuta wa YERIKO (Inonga na Che Malone) Hawa mabeki wote ni wacheza na jukwaa Bora hata Chemalone Fondoh anakua serious kidogo lakini Enonga utoto mwingi na kicheza na jukwaa ndiyo kitu anachoweza.

Simba sc waliposawazisha nilimuona Inonga alianza sifa anapokua na mpira anataka achezee mpira/apige chenga Mara amtishie Max Nzengeli kiufupi huo ni utoto.

Robertinho hapa angevunja mmoja angeanzia benchi na mmoja wapo angecheza na KENNEDY JUMA.

3/Viungo wakabaji Kati ya Ngoma na Kanuti mmoja wapo angeanza nje haswaa na Kanuti MZAMIRU angeanza, hii NI Derby na katika dabi ya karikoo huwa tunashuhudia dabi mbili Kati ya MZAMIRU na AUCHO.

Mzamiru huwa anamuweza sana AUCHO mpaka aucho anapaniki tofauti na Kanuti/Ngoma hapa Robertinho alibugi pakubwa sana Mchezaji mwandamizi Kama Mzamiru kuanzia benchi kwenye mechi Kama hii.

4/Chama na Saidoo ntibazonkiza hapa mmoja wao alipaswa kukaa benchi maana uchezaji Wa Yanga sc ni mpira wa speed ili uweze kupora mpira kwao unapaswa kuwakaba mawili wawili na msitegemee Viungo wakabaji.

Chama na Saidoo ntibazonkiza Hawa wote wakipoteza mpira siyo wakabaji Kama Viungo washambuliaji wa Yanga sc.

5/Uchoyo wa Kibu Denis kila anapopata mpira anataka afunge yeye sijui Kama Robertinho hakuliona hili kila anapopata mpira anataka apige golini tu hata Kama wenzie wamefungua nafasi wapasiwe mpira lakini hakufanya Hilo na kocha Robertinho hakumuambia mpaka anapata majeruhi.

6/Physical coach ajitafakari maana timu inacheza Kama imefungwa mawe miguuni wazito sana hakuna morali ndani ya kikosi kila mchezaji anacheza Kama anavyojua yeye.

7/Rotation ya wachezaji ni muhimu sana Shomari kapombe na Muhammed Hussein wanapaswa kupumnzika na vijana wadogo waanze kupata namba Israel mwenda na Duchu wapewe nafasi.

NB: Yanga sc ilikua Bora molari ya wachezaji na kupambana kwa Kasi ile ile mpaka mwisho ndiyo sababu ya KULETA matokeo Chanya kwao.
 
Umeongea ukweli kabisa, wenye Simba wao wanawaza nani wamgeuze mbuzi wa kafara badala ya kutatua matatizo ya msingi ambayo yalianza kuonekana tangu mwanzo wa msimu.

Timu ilikuwa inashinda ila washabiki hatukuwa na furaha kutokana na jinsi timu inavyocheza.
 
20231106_141006.jpg
 
Umeongea ukweli kabisa, wenye Simba wao wanawaza nani wamgeuze mbuzi wa kafara badala ya kutatua matatizo ya msingi ambayo yalianza kuonekana tangu mwanzo wa msimu.


Timu ilikuwa inashinda ila washabiki hatukuwa na furaha kutokana na jinsi timu inavyocheza.
HAPO HATA WAKIMFUKUZA KOCHA MAMBO NI YALE YALE TU.
 
HAPO HATA WAKIMFUKUZA KOCHA MAMBO NI YALE YALE TU.
Timu haina wachezaji wa kuendana na mahitaji ya Simba na kocha wa viungo hatoshi.

Pia kocha ana ujinga mwingi, kuna wachezaji wake kama Saido , Zimbwe na Kapombe wamebakiza majina tu lakini kila mechi wamo tu tena dakika 90.
 
1/ Aishi Manula hakupaswa kuanza/kucheza kabisa kwa sababu hakuwa na match fitness, japo kuwa benchi la ufundi lilikua na maono ya kumrudisha Aish Manula rasmi katika ligi kutokea Majeruhi...
Upo sahihi lakini ufa huo umeweza kuubaini kutokana na ubora walioonyesha Yanga. Kamajana Simba ingecheza na JKT Ruvu usingeona hayo mapungufu.

Hivyo basi kila durby team hata iwe nzuri kiasi gani kuna makosa madogo madogo sana huifanya team moja kupoteza. Tuendelee tusubiri mechi ijayo
 
Upo sahihi lakini ufa huo umeweza kuubaini kutokana na ubora walioonyesha Yanga. Kamajana Simba ingecheza na JKT Ruvu usingeona hayo mapungufu...
Haya mapungufu ya simba hayajaanza kuandikwa leo hapa jf, toka kipindi timu inashinda watu waliandika nyuzi hapa ila kwakua timu inashinda wengi wenu hamkuziona au kuzipuuza nyuzi za kuwakosoa.
 
Timu haina wachezaji wa kuendana na mahitaji ya Simba na kocha wa viungo hatoshi.

Pia kocha ana ujinga mwingi, kuna wachezaji wake kama Saido , Zimbwe na Kapombe wamebakiza majina tu lakini kila mechi wamo tu tena dakika 90.
Kweli kabisa.
 
hakika game ilikuwa ni ngumu mno kwa upande wa mnyama ni suala tu la kusema asante Mungu coz kuna nafasi zilikuwa zinakoswa nyingi mnooo lasivyo tungesema mengine leo


Political is just liKe a war always, BOOST YOUR CONFIDENCE
 
Kila nenonlitasemwa...

Wenye akili tuliwashauri sana wakatupuuza.

Nikawaambia mashabiki wa simba Wajiandae kisaikolojia.
Wewe ni muongo sana umesahau siku ya jumatano kwenye thread ya mo dewj kuteua kamati ya fitna na wewe uliweka matokeo ya simba kushinda 5 kwa Yanga O mwaka 2012 halafu ukasema ogopa sana wenye simba yao wakiungana? Halafu hapa unataka kujifanya eti ulishaonya
 
Aishi Manula hakupaswa kuanza/kucheza kabisa kwa sababu hakuwa na match fitness, japo kuwa benchi la ufundi lilikua na maono ya kumrudisha Aish Manula rasmi katika ligi kutokea Majeruhi lakini hesabu zimekua tofauti na vile benchi la ufundi lilivyoamini/kutegemea Aishi Manula angefanya vizuri katika Derby ya Kariakoo
Mkuu bora Manula ndio amepigwa zile 5 ingekua kapigwa Salim mtoto wa watu January angetafutiwa timu na ndio ungekua mwisho wake kusikika sikika tena.
 
Back
Top Bottom