Igunga: Mgombea ubunge wa TLP ajitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Mgombea ubunge wa TLP ajitoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Sep 1, 2011.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,685
  Trophy Points: 280
  WAKATI vuguvugu la siasa jimboni Igunga mkoani Tabora likiendelea kushika kasi, mgombea ubunge mteule wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Dk. Moses Edward, amejitoa kuwania nafasi hiyo ya ubunge kupitia chama hicho.

  Akizungumuza na waandishi wa habari jana katika ofisi za chama hicho jimboni humo alisema ameamua kujitoa kutokana na kukabiliwa na ukata huku zoezi hilo likihitaji nguvu kubwa.

  Alisema hata makao makuu ya chama hicho yameshindwa kuonyesha msaada wowote hadi sasa huku mbio za kampeni zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.

  “Nimefikia maamuzi haya hasa baada ya makao makuu ya chama changu kushindwa kunipa msaada wowote huku kukiwa hakuna mwelekeo wa kuniunga mkono,” alisema.

  Alisema alipitishwa na chama hicho bila kupingwa na kufanya idadi ya wagombea wanaowania nafasi hiyo kufikia wagombea saba.

  Alitoa wito kwa wanachama wa chama hicho kuhakikisha wanaunga mkono chama watakachoona kinafaa kulingana na hoja za mchakato huo utakavyokwenda.

  Mpaka sasa katika Jimbo la Igunga hali ya kisiasa inazidi kuchukua sura mpya, hasa mji huo kukusanya wanasiasa mbalimbali ambao wanahakikisha wanaibuka na ushindi.

  Hadi sasa ni wagombea sita wamejitokeza na kuchukua fomu ya serikali ya kuwania ubunge kupitia vyama vyao.

  Vyama hivyo ni CHADEMA inayowakilishwa na Joseph Mwandu, Chama cha Wananchi (CUF), Leopard Mahona, huku Chama cha Sauti (SAU), kikimteua John Maguma, Said Makeni (DP), Lazalo Ndegaya (UMD) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwakilishwa na Dk. Peter Kafumu.

  source: http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=34036

  MY TAKE. Hivi vyama vya DP, UMD na SAU vinanipa maswali mengi kuliko majibu. Ni vyama shindani kweli au vya msimu?
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  vyama vya misimu ni matatizo ndio maana mrema wafuasi wake wanasema ajihuzuru ili wapatiakane vijana wenye akili mpya na endelevu ndani ya chama
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Vyama vingine vinashiriki ili kurushiwa makombo yatakayodondoshwa na baba lao magamba TLP imenusa hakuna makapi safari hii, hata mbwa anajua jalala lipi lina unafuu.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,139
  Trophy Points: 280
  Nnawapongea TLP kwa kuona kuwa huko ni maji marefu yaliyowazidi kimo. Haya hao wana TLP wachache wapeni kura zenu CCM kwani magwanda si mmeshawaona siasa zao ni kufata na kuongelea watu badili ya kufata na kuo ngelea maendeleo.
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Sep 1, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu hivyo vyama vimesimamishwa na CCM kwa mawazo kwamba watapunguza kura za CHADEMA, kumbe wanajidanganya. wagombea wa hivyo vyama hata hela ya gharama za kampeni hawana, wanalipiwa na magamba
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Sep 1, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  sijajua kama wewe ni bonge la mwanamke. juzi nimekuona vizuri
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  mazingaombwe yashaanza! naye alipojiingiza alikuwa anategemea msaada wa aina gani kwa mfano?
  ff,angekua kajtoa wa chama mwenza hapo labda ila tlp sijui kama wanaunga mkono sana magamba. ila usiwe na wasiwasi, sera ya magamba ni kupindua daima (whatever..)
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wachache wepi wakati alikuwa peke yake.
   
 9. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  Una ushahidi?? Thibitisha.
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Maendeleo yepi hayo Faiza Fox??????????Unaota nini au unaishi nchi gani??????
   
 11. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,680
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  tujadili hoja ya msingi! hivi hicho chama hakina ruzuku, kuna haja ya kupitisha sheria ya kupunguza idadi ya vyama vya siasa maana vingine vipo kama havipo!
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  TLP INA MBUNGE 1 AGUSTINOR LYATONGER MREMER NAYE NI ZAID YA HASARA ACHILIA MBALI KUMPIGIA KURA NANI ATATHUBUTU HT KURUSHA MGUU KWNYE MKUTANO WA MGOMBEA WA TLP? mi nampongeza sbb amesoma alama za nyakati bd ccm.
   
Loading...