Igunga: Mbunge kunywa sumu CCM ikishindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Mbunge kunywa sumu CCM ikishindwa

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by raffiki, Sep 19, 2011.

 1. r

  raffiki Senior Member

  #1
  Sep 19, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ndugu zangu CCM huyu mbunge anaongeza kura za CCM au anapunguza?jiulize anawambia hivyo watu wa uelewa gani...!kwa akili zangu ndogo tena sie watu wa vijijini tunajiju, mtu akisema kitu fulani kikitokea atafanya hv, kwa desturi zetu sie wenye uelewa mdogo ndio tunafanya hivyo ili tuone atakunywa sumu kweli au..???CCM inahitaji watu makini kwa mwendo huu haaa sijuii

  Source:Tanzania daima.
   
 2. jambo1

  jambo1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani Living stone Lusinde Babo ana fikra za zamani..!

  KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

  Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.

  “Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu,” alisema na kuongeza:

  “Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia Mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa,” alisema Lusinde.

  “Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita,” alisema Lusinde Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

  Kwa upande wake mratibu wa kampeni hizo, Mwigulu Mchemba, aliwataka wananchi hao kumchagua Dk. Kafumu na kusema wanasiasa wa upinzani wanasema tangu uhuru serikali ya CCM haijafanya kitu kabisa, Igunga haijapata maendeleo wakati si kweli.

  “Wenzetu wanapandikiza chuki kwa vijana wa vyuo vikuu nao wanakubali kupotoshwa na wanasema serikali ya CCM haijafanya kitu si kweli. Kwanza idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu imeongezeka halafu wanasema Rais huyu hajafanya kitu, kama si kulaaniwa ni nini?” alihoji.

  Alisema wapinzani wanatumia umaskini wa wananchi kama mtaji wa kisiasa, wamelalamikia kupandishwa kwa bei ya pamba ili watu wakasirike na kutoichagua CCM.

  “Wacha niwaambie wakati wa ukame serikali ya CCM iligawa chakula jimbo lilipokuwa wazi wakasema tusigawe chakula eti hiyo ni rushwa sasa tusipogawa chakula mtatuchagua? Hivi njaa ina likizo? Kwa nini serikali ipeleke chakula mpaka Somalia lakini Igunga ibaki na njaa hivi mtapiga kura mkiwa na njaa?” alihoji Mwigulu.
   
 3. HT

  HT JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  khaa! CCM wameishiwa hadi kumkodi huyu Lusinde? Angalia aliyoyasema sasa. Kwa wenye akili timamu watajua hafai na hivyo anapunguza kura za dr. Kafumu badala ya kuziongeza.
  Poleni CCM
   
 4. j

  jigoku JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Jamani Lusinde nae ni wa kumjadili?huyo dogo ni Empty magazine!
   
 5. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  ...........
  You dont need to be a rocket scientist to see the conflict in the statements.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Nna wasiwasi Lusinde kama hata ametahiriwa maana lugha zake huwa hazina punje hata ya heshima na uelewa wa mambo. Lugha nyingine alitakiwa aziongee akiwa na watu wa kwao ugogoni sio za kusikika na watanzania wote. Hovyooooooooooooooooo!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Si ameshapewa taarifa ya kiasi cha vitambulisho vya mpiga kura vilivyonunuliwa mpaka sasa na vilivyoorodheshwa na wenyewe kutishwa mkiwapigia upinzani tutajua namba zenu tunazo ?
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  Lusinde anajadiliwa hapa???oooooooooooohhh poor boy kunywa sumu ufanyike uchaguzi mwingine then CDM wachukue jimbo lako nalo
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Huyu Mbunge Lusinde kwa tafsiri yangu aliwakasirisha watu kwa matusi haya yafuatayo na baada ya hapo ndo akakumbana na joto ya jiwe kwe wenye uchungu na nchi hii.

  KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

  Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.

  "Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu," alisema na kuongeza:

  "Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia Mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa," alisema Lusinde.

  "Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita," alisema Lusinde Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.
  [​IMG]

  Hali Tete Uchaguzi Mdogo Igunga; Magari Ya CCM Yapigwa Mawe


  Mbuge wa Mtera, Livingstone Lusinde, akiwaonesha maafisa wa polisi sehemu ya kioo cha gari lake kilichopasuka baada ya kurushiwa mawe na watu waiojulikana wakati masfara wa magari ya kampeni ya CCM, kurushiwa mawe katika kijiji cha Nkinga.
  Picha na Victor Makinda
   
 10. n

  ngoka New Member

  #10
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwenye akili timamu anajua mvuta bangi ni nani kati ya ccm na chadema,maendeleo hayatangazwiwau hujionea wenyewe,mkishashiba na kuongeza vitambi vyenu kama anavyoonekana huyo lusinde ndio miropoko inakuwa mingi!shibe ndio inakufanya uropoke!
   
 11. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Kauli aliyotoa plus size of his stomach angekuwa mwanamke ningesema tumsamehe ujauzito unamsumbua.

  Huyu Lusinde hajui kama hiyo mikutano inaudhuriwa na watoto pia na yeye kama mbunge ni role model?

  Hajui kwamba ana waambia younger generation is okay to commit suicide?
   
 12. bi mkora

  bi mkora JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 262
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahaha Uyu mbunge anacheza, inabidi tummalizie asipojiua coz lazima CCM ishindwe.
   
 13. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bora afe na kitumbo chake ilitufanye uchaguzi mwingine tena!
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,334
  Trophy Points: 280
  Mhe. Lusinde sio tuu ni mpayukaji mwenye mdomo mchafu, jamaa ni debe tupu kabisa!. Kabla ya kuukwaa ubunge, jamaa alikuwq MC maarufu kule Dodoma. Nadhani ni umaarufu wa uMC ndio uliomsaidia kumuangusha yule Mzee na busara zake. Ndiye mpuuzi huyu huyu aliyetamka bungeni kuwa "tufunge milango tuzichape!".

  Tuwashukuru waandishi na wahariri wa habari kuzistahi hizi kampeni kwenye kinachoandikwa na magazeti yao, vinginevyo kila kinachotamkwa kingeandikwa, sio tuu ni vichekesho vingejaa magazetini bali na visivyosomeka vingeandikwa.

  Kwa wale wenzangu na mimi, baadhi ya wabunge ambao ni majuha kabisa, utawatambua kwa kuwaona machoni tuu hata kabla hawajatoa hayo maupupu yao, huyu Mhe. Lusinde ni mmoja wa watu hawa!.

  Meya wa jiji was not right alipodai kuwa baadhi ya wabunge wa Dar es Salaam wanafikiri kupitia makalio!, the fact ni kuwa sio wabunge wa DSM pekee bali hata wa sehemu nyingine na mfano hai ndio huu wa mbunge wa Mtera!. I doubt if he has even a tiny little brain to help him think!.
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Kilaza tu huyu
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo bado siku chache afe
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wala simshangai Lusinde. Alishawahi kusema bungeni kwanba akinamama wa Mtera waliona gari ndogo ya Padri wakasema ni mtoto wa gari kubwa walioiona awali. Na walipoo na exaust wakasema ni mtoto wa kiume. Haya ni maneno aliyaongea bungeni. Unaweza kupata picha ya mtu tunayemzungumzia hapa. Sio tu ni mpuuzì lakini hajui ni nini hasa anachokifanya kwenye siasa. Kama sio minyukano ya kimakundi ndani ya chama, leo angekuwa anaendelea na kazi yake ya ufundi wa bomba (plumber)
   
 18. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hiv huyu lusinde, huwa anafikiri kwa kutumia nini? Coz anaongea pumba mpaka anakera
   
 19. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Angetaja na aina ya sumu atayotumia.......
   
 20. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Fikiria mamilioni ya kodi zetu anayovuta kila mwezi mpuuzi kama huyu!
   
Loading...