Igunga: Kigogo wa CCM afumaniwa na mke wa mtu

Status
Not open for further replies.

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Oct 27, 2008
456
103
Mojawapo wa viongozi wakuu wa kampeni za CCM amefumaniwa na mke wa mtu gesti wakijivinjari. Mwanamke mwenye uhusiano na mratibu wa kampeni za ccm kapata kipigo cha uhakika imebidi alazwe hospitali. Mumewe aliyempa kipigo vilvile ni kada maarufu wa chama cha mapinduzi. Hata hivyo viongozi wa CCM walijazana polisi na kuweza kuipotezea hiyo issue kuzuia aibu.
Kutoka Tanzania Daima

TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeingia katika msukosuko mkubwa wa chini kwa chini baada ya kiongozi mmoja mwandamizi anayeongoza kampeni hizo (jina tunalihifadhi) kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu, Tanzania Daima limebaini.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu jijini Dar es Salaam na kutoka Igunga zinaeleza kuwa tukio hilo limesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mwanamke huyo.

Ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alisema sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo anayeongoza kampeni za chama hicho kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM wakiendelea kupambana.

Habari zinaeleza kwamba mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kililieleza gazeti hili kwamba kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).

Inaelezwa kwamba mara baada ya kufikishwa kituoni hapo na wasamaria wema, mwanamke huyo (jina tunalo) alitakiwa kwanza kulitaja jina la mtu aliyemsababishia majeraha hayo na akajikuta akipata wakati mgumu kumtaja mumewe.

Habari zinaeleza kwamba taarifa za tukio hilo zilipofika katika ofisi za CCM wilaya ya Igunga, maofisa wa chama hicho waliingilia kati na kuamua kulizima jambo hilo chini kwa chini ili kuepukana na hatari ya kuvuruga kampeni nzima za ubunge cha chama hicho.

"Ni kweli tumepokea habari za kusikitisha kuhusu kiongozi wetu mmoja wa juu katika kampeni kukumbwa na kashfa ya kufumaniwa na kusababisha mwanamke aliyadaiwa kuwa na uhusiano naye kupata kipigo kikali kutoka kwa mumewe ambaye pia ni kada maarufu wa chama chetu Igunga," alisema ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na gazeti hili.

Hata hivyo, ofisa huyo alisema uchunguzi walioufanya awali kuhusu tukio hilo umebaini taarifa za kigogo huyo wa CCM kuwa na uhusiano usiofaa na mke wa mtu zilivujishwa na kundi la vijana wengine wa kiume walio katika timu hiyohiyo ya kampeni ya CCM ambao ndiyo waliopenyeza taarifa hizo kwa mume wa mwanamke anayetuhumiwa.

Wakati chama hicho kikihaha kulifunika sakata hilo ili lisivuje, viongozi wake waandamizi walipata wakati mgumu kumnadi mgombea wao, Dk. Peter Kafumu, kwenye ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Kata ya Nyandekwa, katika jimbo la Igunga.
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,506
CCM ni balaa hiyo ilikuwa session ya kampeni ya usiku
kumbuka mama Salma alisema wao watafanya kampeni siyo nyumba kwa nyumba bali shuka kwa shuka.
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,442
2,470
unaweza kudanganya watu kila siku lakini ipo siku utaumbuka kwa matendo yako, adhabu yao bado kwani wanajua ni nn walichofanya 2010 kuiba haki ya watanzania. mengi yatajitokeza hayo madogo,tutarajie mengi na maafa pia kwa wale walioiba haki majimboni na pia tutarajie kuumbuka kwa wengi, huwezi kuiba haki ya mtanzania alafu Mungu akakuacha uendelee kuiba bila kukupa kichapo hapa hapa duniani.sala za wanyonge zitawafuata popote walipo.
 
Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,332
Kwa siasa hizi kuna kila dalili CDM IKASHINDA IGUNGA maana naona mnajitahidi, wapi ile video ya vijana wanaopewa mafunzo ya ugaidi?
 
pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,238
1,354
Sasa kama issue imeshapotezewa unaileta ya nini hapa?

mkuu,vp yale mavingereza yako magumu kama ya wapenda sifa kwenye debate enzi za o level mbona huyaandiki tena?.... poleni kwa kufumaniana,nawe uwe makini na mkeo mana inaonekana ni kamchezo kenu magambaz...
 
EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,080
• Kigogo afumaniwa na mke wa mtu

na Mwandishi wetu

TIMU ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeingia katika msukosuko mkubwa wa chini kwa chini baada ya kiongozi mmoja mwandamizi anayeongoza kampeni hizo (jina tunalihifadhi) kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu, Tanzania Daima limebaini.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi Ndogo za CCM Makao Makuu jijini Dar es Salaam na kutoka Igunga zinaeleza kuwa tukio hilo limesababisha kujeruhiwa vibaya kwa mwanamke huyo.

Ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini alisema sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo anayeongoza kampeni za chama hicho kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM wakiendelea kupambana.

Habari zinaeleza kwamba mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Chanzo kingine cha kuaminika cha habari kililieleza gazeti hili kwamba kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).

Inaelezwa kwamba mara baada ya kufikishwa kituoni hapo na wasamaria wema, mwanamke huyo (jina tunalo) alitakiwa kwanza kulitaja jina la mtu aliyemsababishia majeraha hayo na akajikuta akipata wakati mgumu kumtaja mumewe.

Habari zinaeleza kwamba taarifa za tukio hilo zilipofika katika ofisi za CCM wilaya ya Igunga, maofisa wa chama hicho waliingilia kati na kuamua kulizima jambo hilo chini kwa chini ili kuepukana na hatari ya kuvuruga kampeni nzima za ubunge cha chama hicho.

"Ni kweli tumepokea habari za kusikitisha kuhusu kiongozi wetu mmoja wa juu katika kampeni kukumbwa na kashfa ya kufumaniwa na kusababisha mwanamke aliyadaiwa kuwa na uhusiano naye kupata kipigo kikali kutoka kwa mumewe ambaye pia ni kada maarufu wa chama chetu Igunga," alisema ofisa mmoja wa juu wa CCM aliyezungumza na gazeti hili.

Hata hivyo, ofisa huyo alisema uchunguzi walioufanya awali kuhusu tukio hilo umebaini taarifa za kigogo huyo wa CCM kuwa na uhusiano usiofaa na mke wa mtu zilivujishwa na kundi la vijana wengine wa kiume walio katika timu hiyohiyo ya kampeni ya CCM ambao ndiyo waliopenyeza taarifa hizo kwa mume wa mwanamke anayetuhumiwa.

Wakati chama hicho kikihaha kulifunika sakata hilo ili lisivuje, viongozi wake waandamizi walipata wakati mgumu kumnadi mgombea wao, Dk. Peter Kafumu, kwenye ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Kata ya Nyandekwa, katika jimbo la Igunga.

Ilimlazimu Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fedha na Uchumi, Mwigulu Mchemba, ambaye pia ni Meneja Kampeni wa Dk. Kafumu, kuwaangukia wanakijiji wa Ussongo, katika kata hiyo, kuwaomba wapunguze jaziba.

CHADEMA ndiyo inaonekana kuwa na mashabiki wengi katika eneo hilo, lakini Mchemba aliwaomba wamchague mgombea wa CCM.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini hapa, Mchemba alidai kuwa kukichagua chama cha upinzani ni sawa na kuchoma moto nyumba yenye kunguni badala ya kumwagia maji kitanda.

"Nilipokuwa mdogo, kwa sababu nimezaliwa katika familia maskini, nilikuwa nalala kwenye kitanda chenye kunguni, sasa nikajifunza kwamba ili kuwaondoa kunguni lazima ukimwagie maji ya moto kitanda hicho. Hii ni busara tu, lakini mwingine anaichoma moto nyumba nzima," alisema.
Ili kujihami, CCM iliomba ulinzi wa polisi tofauti na mikutano yake mingine.

Mwigulu alisema wanaoibeza CCM hawapendi kuona maendeleo ya wakazi wa Igunga na vitongoji vyake, kwa kuwa baada ya uchaguzi wote wanarejea makwao.

Alisema, "Tunao madiwani 32 kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Igunga kati yao wawili wanatoka upinzani waliobaki ni CCM kwa nini tuchanganye punda na ng'ombe kwenye kilimo? Ni wanyama wenye sifa tofauti katika kufanya kazi."

Dk. Kafumu aliahidi kusimamia rasilimali za wakazi wa Igunga kwa kuhakikisha kila kinachopatikana kinatumika kwa faida yao na si vinginevyo. Aliahidi kushirikiana nao kwenye maendeleo ya shule, zahanati na kumaliza tatizo sugu la maji.
"Nimezaliwa hapa Igunga, mmenilea na kunisomesha ninyi wenyewe naowaomba mniruhusu niwatumikie kwa kuwa nazifahamu fika kero za wilaya yetu," alisisitiza.

Gazeti la Tanzania Daima
 
dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
252
CCM magamba>CCM kunguni,...................,...........................,........................
 
Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,416
1,554
magamba wamebanwa vilivyo ndo maana huyo kaamua kupunguza stress walau kwa kubanjua amri ya 6 na kada mwenzie.lakini ccm ndo walisema slaa kaoa mke wa mtu so what si waonyeshe mfano?
 
We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
797
363
Du kumbe haka katabia hakapo kwa wakulu tu ambao husafiri na vimada wao wanapokwenda huko nje ya nchi kwa kutumia kodi ya walala hoi watanzania, kumbe mpaka ktk ngazi ya Wilaya? ahaaaa Chama hiki jamani...! haya tusubiri, labda watakuja kukanusha......
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,208
8,683
Aibu yao!
Hii inatosha kabisa kuwanyima kura, maana wanaendeleza ufisadi wa ngono!
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom