Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 549
- 785
Tuma timu yako kwa namna inayofaa leo tarehe 01.10.2023 wakajiridhishe namna Trafic wanavyokomoa Madereva hasa wa Bajaji katika eneo hilo.
Leo nimepita Mandela Road Dar es Salaam nimeona operesheni kali madereva wa Gari wanakamatwa na wengine watu wazima wanafokewa na kujibiwa vibaya kwa kiburi, Dharau na udhalilishaji kama watoto wadogo katika kituo cha Polisi Tabata Relini, usimamizi wa sheria umegeuka Vita pale.
Makosa yenyewe nimeyaangalia mengi yanahitaji Elimu tu lakini watu wanakomolewa wanaandikiwa tu notification kama watu wametumwa kufikia Target flani ya Makusanyo bila kuangalia chochote.
Upokeaji wa Rushwa eneo lile ni wa kiwango cha kutisha,Trafic anaongea waziwazi kwa Dereva kwamba chini ya Elfu 10 hapokei hata kabla Dereva hajamwambia habari za Rushwa hii ni hatari.
Kuna Trafic mmoja mwanamke namba zake zina 88 mbili mkononi kavaa Smart Watch na Bracelet ni hatari kwa Rushwa,kukomoa na Majibu ya hovyo kwa Madereva, anafanya kazi kwa vitisho na vurugu kama mtu ambaye ameshatumia kilevi au kisaikolojia ana matatizo makubwa.
Naona huyu Dada anatumia sana Sticker ya Nenda kwa Usalama kama kosa kubwa sana,kwanini Polisi wasiweke Sheria vizuri kama hilo ni kosa kubwa kiasi hicho zikapatikana palepale kituoni gari ikakaguliwa hapohapo mtu akalipia akapewa badala ya kutumia Rungu la Faini tu kwa kila kitu,rungu la Elimu na Uhamasishaji liko wapi?
Ieleweke hali ya Maisha ni ngumu kumlipisha Dereva wa Bajaji Faini makosa mawili au matatu kwa pamoja asubuhiasubuhi ambayo ukiyaangalia ni makosa ambayo yanahitaji tu Elimu, tukumbuke kumfanyia hivyo umefanya siku nzima afanye kazi bure umemuumiza yeye umeumiza hadi Familia yake ,hii siyo nzuri inazidisha sana Chuki ya Raia kwa Jeshi la Polisi.
Kwa nia njema IGP liangalie hili.