Mwanza: Bodaboda walalamikia uwepo wa kituo bubu cha polisi ambapo hutozwa Tsh. 10,000 kwa kila kosa la barabarani bila kupewa stakabadhi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,611
Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda jijiji Mwanza wamelalamikia uwepo wa kituo bubu cha Polisi kinachotumiwa na askari Polisi wasio waaminifu kwa ajili ya kujipatia fedha kinyume cha sheria huku wakiwabambikia faini na kuwalazimisha bodaboda hao kulipa bila kuwapa stakabadhi

Wakizungumza kwenye kongamano la elimu kuhusu usalama barabarani pamoja na madhara dhidi ya wanawake na watoto wamesema kituo bubu hicho cha polisi kipo Jirani na bandari ya Mwanza Kaskazini, Askari Polisi hao huwatoza faini ya shilingi elfu kumi kwa kila kosa la usalama barabarani bila kuwapa stakabadhi

"Hata sasa hivi ukienda pikipiki utazikuta pembeni kule karibu na meli ndiko mapatano yanakofanyikia ninasema hivyo sababu ni za kwetu tunapelekwa kule hazipelekwi huko ndani na malipo yanafanyikia kule nje sasa hili je RTO hajui kama kuna kituo kingine huwa kinatoza faini? Muhakikishe ukitoka hata leo utakuta pikipiki kule nje na siyo ndani na malipo yanafanyikia kule nje"

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoa wa Mwanza Dustan Kombe akawataka bodaboda hao kuhakikisha faini wanazolipa ngazi za juu zinafahamu na kuahidi kufikisha sula ahilo sehemu husika ili hatua zichukuliwe

"Hata kama una makosa ushaambiwa una makosa sawa saba mara kumi ngapi? Kumi mara saba? Kwahiyo elfu sabini natakiwa nilipe lakini nataka RPC ajue OCS, OCD, RTO ajue ili kituo kilichopo kifutwe na uzuri sisi tunachukuliana hatua tumeelewa vizuri?

Akiwa kwenye kongamano hilo mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wanawake na Watoto la KIVULINI Yassin Ally akawataka bodaboda hao kuja na mfumo utakaowaongoza kujiwekea kanuni na taratibu zinazotokomeza ukatili kwa wanawake na Watoto

"Tuje na mfumo utakaoongoza bodaboda nchi nzima kupitia vitu vyao kujiwekea kanuni na taratibu zinazolinda usalama wa watu na abiria zinazozingatia mafunzo lakini pia zinazotokomeza ukatili dhidi ya wanawake"

"Basi twende tukawe na tabia ya aina moja ya kusaidia watu wetu na watu wetu ambao tunawasaidia nao ni kundi maalum kama mlivyo nyinyi sisi kwa sisis ni lazima tuhakikishe tunasaidiana"


Chanzo: EastAfrica Tv
 
Hawa wakuda njaa zao zitawapeleka motoni..polisi siwapendi kwa kweli ni bora mtu akutane na jambazi kuliko polisi
 
Nchi hii kunq uhuni San

Tunazidi kutengeneza taifa la majambaz

Ova
 
Back
Top Bottom