Fall Army Worm
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 19,331
- 14,259
Kwa jinsi nilivyochafukwa Naomba hata Salamu niachane nayo kabisa Wapendwa sana Wana JF wenzangu.
Naamini kuwa Uzi huu Unaweza kumfikia Mheshimiwa Siro, Aidha kwa yeye Mwenyewe kuusoma au Kufikishiwa na watu wake wa Karibu. Niende moja kwa Moja.
Mheshimiwa Ombi langu ni kuhusiana na Mauaji ya kikatili wanayofanyiwa watoto wetu wadogo huku Njombe, huku wakinyofolewa baadhi ya Viungo km vile Koromeo, Kadhia hii imewakumba pia Akina mama, ambao hutolewa Kizazi. Katika Matukio haya yote ukiyaangalia kwa haraka Nyuma ya pazia kuna kila dalili kuwa ni Mambo ya Kishirikina.
Hivyo basi, Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Njombe nikuombe sana Mkuu Utusaidie fanya Kama ulivyofanya Mwaka ule kule Kibiti, Yale majamaa uliyatia adabu hadi Leo hii Kibiti kupo Shwari Kabisa.
Nina IMANI na wewe kuwa Jeshi lako la Polisi lina weledi wa kutosha, kufanya Intelijensia ya hali ya juu hata kuwabaini Wajuaji hao.Binafsi ningependekeza hao jamaa wafanywe kama wenzao kule Kibiti Yaani mwendo wa Shaba. Japo sio vizuri kuhukumu lkn inatia uchungu mno kwa Mauaji wanayofanyiwa watoto na Akina mama kutolewa Kizazi.
Aidha kwa jambo hili lina kila dalili ya kuhusishwa na IMANI za Kishirikina,Intelijensia ijikite pia kuwachunguza Waganga wa Kienyeji wanaojihusisha na mambo haya.
Chonde sana mheshimiwa tusaidie, Hivi sasa muda wote tunakuwa tunawaza Watoto wetu yaani Matumbo moto, Ni km vile hatupo ktk Kisiwa cha Amani.Mkoa wetu wa Njombe Ulikuwa ni Mahali salama kwa Kuishi Lkn sasa imekuwa tishio.
Sent using Jamii Forums mobile app