IGP Sirro nakuomba shughulika na wanaofanya mauaji huko Njombe kama ulivyoshughulikia wale wa Kibiti

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,322
14,244
Kwa jinsi nilivyochafukwa Naomba hata Salamu niachane nayo kabisa Wapendwa sana Wana JF wenzangu.

Naamini kuwa Uzi huu Unaweza kumfikia Mheshimiwa Siro, Aidha kwa yeye Mwenyewe kuusoma au Kufikishiwa na watu wake wa Karibu. Niende moja kwa Moja.

Mheshimiwa Ombi langu ni kuhusiana na Mauaji ya kikatili wanayofanyiwa watoto wetu wadogo huku Njombe, huku wakinyofolewa baadhi ya Viungo km vile Koromeo, Kadhia hii imewakumba pia Akina mama, ambao hutolewa Kizazi. Katika Matukio haya yote ukiyaangalia kwa haraka Nyuma ya pazia kuna kila dalili kuwa ni Mambo ya Kishirikina.

Hivyo basi, Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Njombe nikuombe sana Mkuu Utusaidie fanya Kama ulivyofanya Mwaka ule kule Kibiti, Yale majamaa uliyatia adabu hadi Leo hii Kibiti kupo Shwari Kabisa.

Nina IMANI na wewe kuwa Jeshi lako la Polisi lina weledi wa kutosha, kufanya Intelijensia ya hali ya juu hata kuwabaini Wajuaji hao.Binafsi ningependekeza hao jamaa wafanywe kama wenzao kule Kibiti Yaani mwendo wa Shaba. Japo sio vizuri kuhukumu lkn inatia uchungu mno kwa Mauaji wanayofanyiwa watoto na Akina mama kutolewa Kizazi.
Aidha kwa jambo hili lina kila dalili ya kuhusishwa na IMANI za Kishirikina,Intelijensia ijikite pia kuwachunguza Waganga wa Kienyeji wanaojihusisha na mambo haya.

Chonde sana mheshimiwa tusaidie, Hivi sasa muda wote tunakuwa tunawaza Watoto wetu yaani Matumbo moto, Ni km vile hatupo ktk Kisiwa cha Amani.Mkoa wetu wa Njombe Ulikuwa ni Mahali salama kwa Kuishi Lkn sasa imekuwa tishio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu hawa ndiyo wanao ituhumu mikoa ya pwani kwa ushirikina. Wanajisifu kwa elimu, elimu yao sasa inawasaidia nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bwana mkubwa wakati huu sio wa kuanza kuzodoana Bali ni kutiana Moyo na kuombeana, maana Watoto wetu wanaouawa kwasababu ya ujinga wa Mijitu michache Hawana hatia, Watoto ni Malaika. Nashangaa jinsi unavyowazodoa WanaNjombe bila hata kuwabaini na Chembe ya Huruma kwa watoto wanaokufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mauaji yangekuwa yanafanyika mikoa ya kusini dunia nzima ingesimama au mauji ya albino yangekuwa mikoa ya kusini sipati picha
 
Kila matukio ya kutisha hutokea nje ya mikoa ya pwani, ila wanajifanya hawaoni.
Huwezi sikia ujinga huu mikoa ya pwani, ingawa uchawi upo sio wananna hii, unauwa Binadamu mwenzio, na nguvu zake Damu ingali ya moto, eti akupe utajirili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi Kibiti ipo Mkoa wa Singida, eti?, Na vipi Kuhusu ile mili ya watu waliokuwa wakipatikana kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi??. Au huko sio Pwani??!!!. Ni Hayo tu Mkuu, Ngoja niendelee kuomboleza.

Mauaji huko njombe yanasababishwa na ushirikina,watu huko kutwa kuwaza utajiri wa ndumba
Serikali labda ianzishe operesheni kwa waganga wote huko

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Kibiti ipo Mkoa wa Singida, eti?, Na vipi Kuhusu ile mili ya watu waliokuwa wakipatikana kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi??. Au huko sio Pwani??!!!. Ni Hayo tu Mkuu, Ngoja niendelee kuomboleza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mauaji ya kibiti ukiaita ya kishirikina, basi kweli wewe utakuwa chaula, hapa tunaongelea ushirikina, huku mkijiita mmeendelea, na mna elimu, kuliko mikoa ya pwani, sisi wanyeji wa mikoa hii ya pwani, ambako ustaarabu ulikoanzia, tunawauliza Elimu yenu inawasaidiaje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana mkubwa wakati huu sio wa kuanza kuzodoana Bali ni kutiana Moyo na kuombeana, maana Watoto wetu wanaouawa kwasababu ya ujinga wa Mijitu michache Hawana hatia, Watoto ni Malaika. Nashangaa jinsi unavyowazodoa WanaNjombe bila hata kuwabaini na Chembe ya Huruma kwa watoto wanaokufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona mpaka nimeandika hapa, jua nimeguswa, lakini lazima tujue ubaguzi, ndiyo chanzo, cha kuondoa utu wa mtu mwingine, ubaguzi unamwondolea dhamani mwingine.

Tukae tujue wote ni Watanzania, na pale, mnapojiona mmeendelea, wakati sisi tunaona hamjaendelea kiasi, cha kumdharau mwingine, inabidi tukuonyeshe, kuwa hamjaendelea. Na ili kuweka ushahidi wa kuwa hamjaendelea, ndiyo maana tunakuonyesha kitendo kinachoendelea huko njombe, hakiweze fanywa na mtu aliesoma kamwe.

Lini na Nani Alisema Njombe tumeendelea kuzidi Pwani?, Leta Ushahidi hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom