IGP Sirro, mulika Ofisi ya OCD Musoma

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,504
12,829
Kiongozi Wangu IGP Nyankoro Sirro, kuna malalamiko ambayo yamekuwepo miongoni mwa jamii za wavuvi katika wilaya ya Musoma Vijijini wakituhumu POLISI wako kuhusu masuala ya rushwa na uonevu.

Wananchi wengi wa Musoma Vijijini wanategemea Shughuli za uvuvi ndani ya Ziwa Victoria kuendesha maisha yao, kwa sasa lipo zoezi la ukamataji wa zana haramu za Uvuvi sambamba na kukamata wavuvi wenye zana husika.

Lkn kwa sasa kinachofanyika sicho hicho. Kinachofanyika ni unyang'anyi na Uonevu kwa kukamata na kupiga watu hovyo na kuwatoza kiasi kisichopungua Milioni 1 kwa kila Mvuvi aliyekamatwa na zana wanazoita haramu. Pesa Inakusanywaaaaaa, Huna Milioni au Laki 7 utaenda Central mpaka ndugu zako wajichange kupeleka pesa ndipo uachiwe.

Ukitaka uhakika fika Central uulize idadi ya Wananchi waliokamatwa kwenye hilo zoezi walikuwa wangapi sasa hivi wamebaki Central wangapi na hao wengine wametokaje Serro na kwanin hawapelekwi Mahakaman kama ni wahalifu. Fedha zooote hizo hakuna risiti wanayotoa bali ni fedha ya rushwa ili kuharalisha kwamba nyavu haramu zilikamatwa bila mvuvi!

UONEVU NA. 2
Wananchi wa kijiji cha bwai walishambulia gari la Polisi Toyota Land Cruiser Pickup LX wakati wa zoezi la ukamataji wa Mwalimu wa S/M aliyetuhumiwa kubaka mwanafunzi ofisini.

Baada ya Shambulizi hili ambalo siyo la kistaarabu la Gari, Polisi walikamata vijana wa kiume karbia kijiji kizima. Kwa kifupi waliwasomba.

Sadly wananchi hao walitakiwa kufidia matengenezo ya Gari hilo kadri ya uhalibifu, Zoezi la kuwatoa sero wananchi wote waliokamatwa pia liliendeshwa bila Milioni au Laki 8 aliyematwa hatolewi Cetral. Zilipigwa pessa ambazo wenyeji wanakadiria kufikia 70M.

Kwa sasa gari walilodai limeharibiwa na Wananchi linaendelea na kazi likiwa bovu vile vile na wakati pesa walishalipwa ya kufidia uhalibifu hivyo kuleta picha ya ubadhirifu.

Lakini yote haya yanafanyika chini ya utawala huu unaokataza vitendo vya Rushwa na Ufisadi kwa watumishi wa umma.

Kiongozi Sirro tunakuamini, mulika macho katika haya yanalipaka matope Jeshi la Polisi.
 
Back
Top Bottom