IGP Sirro afanya mabadiliko: ACP Wankyo Nyigesa arudishwa Makao Makuu kupisha Uchunguzi, ACP Mwampakale awa RPC Kagera

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Taarifa zilizopo ni kwamba RPC KAGERA ambaye ametoka Pwani na kupelekwa mkoa Kagera ndugu Wankyo nadhani kauli ya jana ya kuhitaji ukuu wa Jeshi la Polisi imemuungiza matatani hii imeonesha hana nidhamu ya hali ya juu ndani ya jeshi hivyo basi staff officer aliyepo mkoa wa Rukwa ameteuliwa kuwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera na Wankyo amepelekwa makao makuu ya jeshi mkoani DODOMA ambapo ni mji mkuu wa tanzania.

Ikumbukwe kuwa kauli aliyotoa jana kiutendaji ndani ya jeshi la polisi huku akijuwa mkuu wake wa kazi yupo na anafanya kazi hakustahili kusema kuwa mkuu wake wa kazi anafanya kazi ila yeye akipewa ukuu wa jeshi anaweza kufanya vizuri zaidi hii imeonesha kuwa nafasi aliyeteuliwa na amri jeshi mkuu hatoshi kuliongoza jeshi hivyo basi kwa kuwa jeshi huongozwa kwa nidhamu ya hali ya juu ndiyo maana mabadiliko hayo yamefanyika ili akae makao makuu ajifunze nidhamu pamoja na kuandika vipeperushi mabalimbali vinavyolihusu jeshi la polisi.

Pia soma: Wankyo Nyigesa RPC Kagera: Natamani kuwa IGP, aliyepo hajafanya makosa lakini mimi nitafanya mazuri zaidi


IMG-20220329-WA0010.jpg
 
Bangi siyo mboga Wakyo nahisi aliipuliza nyingi ikamshinda kuhimili, halafu ukizingatia ni homeboy wa Sirro wote wanatoka Kanda maalumu, na Bila Sirro Wakyo asingekuwa hapo alipo kiukweli alikosea sana Hana adabu hata angekuwa mtumishi au mfanyakazi wa sekta binafsi huo ni utovu wa nidhamu
 
Ingependeza ungetuwekea kauli ya huyo Bwn. Wankyo aliyoitoa hapo jana!

Kwa hisani ya uzi wa Replica
 
Huyu afande ana akili nyingi Sana, hakutaka kwenda Kagera. Alijua akim- provoc Mkuu wake, obviously atapelekwa makao makuu. Pale ndo atajijenga na Kisha ndoto zake zitatimia.

Hivi mnapajua Kagera?! Waache waende hao waliotoka Rukwa labda watapata nafuu.

Mawazo binafsi.
 
Back
Top Bottom