IGP Said Mwema aongezewa mkataba

Hii kwangu sio habari; habari ingekuwa: "IGP Mwema agoma kuongezewa mkataba", au "Serikali yagoma kumwongezea mkataba IGP Mwema", au.....
 
Ni karata mbaya ambayo mwema ameicheza kama habari hizo ni kweli. Ni bora angeamua kupumzika na kula maisha yake kwani tukiwa tunaelekea 2015, lolote linaweza kutokea litakalomfanya awepo katika watu wanaotakiwa kwenda the Hague kwani mara nyingi wakuu wa polisi huwa hawachomoki na matuko ya uvunjifu wa haki za binaadam. Time will tell
 

mambo kama yataendelea kila mahali ni kuongezewa mikataba hivi damu mpya zitashika uongozi kweli .tatizo la ajiri halitakwisha .kutoka kwenye madaraka ni hadi kifo kikutenganishe.ni boro serikari ikabadili sera zake.mtu akistaafu aondoke jamani vijana wako tene wazuri tu.
 
Inaonekana siku hizi Tanzania tuna uhaba wa wasomi wa kukava nafasi za wastaafu kwenye taasisi mbalimbali..

Maana mara nyingi wanaongezewa mikataba, na hata ikiisha wanatafutiwa nafasi kwenye vitengo vingine.!!

hii kasumba ya kung'ang'ania viongozi waliochoka haileti tija kwenye nchi yetu zaidi ya kuendekekaza kulindana tu.!!
 
Yaani Polisi wote tulionao hakuna wa kuziba nafasi ya IGP.

Aliyeruhusu kuongezwa mkataba huu ...atutake radhi.
 
Mwema ni wakala wa ccm, amefanya kazi nzuri ya kuiwakilisha chama vizuri

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 

Hii huwa naiona kama ni tusi kwa wafanyakazi wa taasisi husika, inatoa ujumbe kuwa wengine mlio katika taasisi husika hamna uwezo wa kushika nafasi ya mtu aliyeongezewa mkataba ilhali umri wake wa kustaafu ushawadia.
 
amepewa bonus ya kazi nzuri anayoifanya ya kulinda vitumbua vya wala nchi....
 

ni jambo jema sana kafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…