IGP Mwema, pls pls pls niko chini ya miguu yako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Mwema, pls pls pls niko chini ya miguu yako!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by CHAI CHUNGU, Apr 26, 2012.

 1. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Walaka huu ukuendee ewe"IGP MWEMA"kisha uingiwe na moyo wa huruma.

  Mh IGP hivi karibuni nilitembelea mkoa wa morogoro ktk shughuri zangu binafsi.
  Nikiwa morogoro nilitembelea maeneo ya mtibwa,dumila,mzumbe,mgeta,matombo,bunduki,vinile,chenzema,kisaki na kisha nikamalizia ziara yangu pale maeneo ya Mlali wilaya ya MVOMERO.

  Kilichonishangaza ni mashamba ya bangi kule maeneo ya(Bunduki na vinile)ambapo imepelekea vijana wengi kuona bangi ndio sigara yao hasa maeneo ya Mlali,sasa kwa pale Mlali tu vijana takribani 70% hivi maeneo hayo wameathilika na uvutaji wa bangi na unywaji wa pombe za kienyeji huku wakiwa wameifanya kamari kama ndio shughuri yao ya kupatia riziki ya kila siku.

  Kamari inachezwa eneo hilo mpaka usiku wa manane, sasa sijui wale askari wako wa mgeta na mzumbe wanafanya kazi gani mh IGP,na 10% nyingine ya vijana ni vijana wanaojishugulisha na biashara ya kuendesha piki piki maarufu kama boda boda,cha kushangaza zaidi ni kwamba ktk waendesha bodaboda hao ni takribani 05% ndio wenye driving licence the rest of 95% hawana licence,hii ni hatari kubwa kwa nchi yetu mh IGP MWEMA,na 20% ya vijana ndio pekee wanaojishugulisha na kilimo.

  Ktk mahojiano yangu na baadhi ya vijana hao wakulima nao pia wana ndoto ya kumiliki piki piki ili waachane na tabu ya kulima.

  Mbaya zaidi nimeshuhudia watoto wengi wa kike wenye umri kati ya miaka 12-16 wakiwa na watoto pia.......gosh..inauma sana kamanda kuona watoto wako wanasoma vizuri wakati watoto wa vijijini wanapigwa mimba na kuvuta bangi kwa uzembe wa kiutendaji wa jeshi lako mkuu lol!

  Ninamachungu sana kiasi kwamba kama tungekua tunaongea uso kwa uso nadhani kesho ningepandishwa kizimbani kwa shambulio la makusudi kha!

  Lengo la kukuandikia walaka huu ndg mh IGP ni kukuomba ufatilie ili kulinusuru taifa la kesho,maana ukizembea basis jua kwamba miaka 10 ijayo hakutakua na nguvu kazi eneo hilo maana sasa hawaogopi hata kuvuta bangi hadhalani na pia wametumbukia tkt dibwi la ulevi uliopindukia wa pombe za kienyeji(GONGO NA MTAMA).

  Niko tayari kutoa msaada wa hali na mali kama kuna ntakachoweza kukusaidia mh " IGP MWEMA"

  Mh naomba kuwakilisha.
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Tanzania ya baadae itakua haina vijana lol!
   
 3. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,107
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Huko ni trailer,nenda TARIME ukaone ESTATES za Bangi! si kama hawaoni, ila wananufaika nazo! sasa mwisho wa siku tutatafuta mchawi! hao wenyewe askari wanatumia hiyo kitu! bado tuna safari ndefu!
   
 4. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  cha ajabu vijana wa mwema ndo watumiaji pia , isitoshe yawezekana pia ndo sehemu ya kuchukulia posho zao
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pengine nao wanamiliki mashamba/estates, c unaona maadili ya polisi yalivoporomoka these days? fuatilia idadi ya wanaofukuzwa kazi na aina ya makosa wanafukuzwa nayo
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,545
  Trophy Points: 280
  mashamba kama hayo yatakuwa ya watu wenye heshima zao,
  na wazee wameshajulishwa ili wayalinde.

  Kwa kweli vijana wetu wanaharibika vibaya sana,
  na hivi ajira hakuna starehe yao ndo hiyo hiyo mwisho.
   
 7. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  maadili yameshuka na pia heshima hakuna tena.. wizi na udhalilishaji ndo umechukua nafasi yake
   
 8. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Siku moja nilikuwa nasafiri kutoka Dar kwenda Mwanza,kufika Tinde kwenye check point ya polisi gari lilikaa kidogo,utingo wa basi nililokuwemo mara akasema amemuona mshikaji ngoja akabomu msuba,ghafla akamsogelea polisi mmoja pandikizi maji ya kunde ambaye nadhani kituo chake cha kazi ni Shinyanga wakateta,askari akaingiza mkono kwenye kombati yake akatoa msuba akampa konda,wakasogea karibu na gari bila aibu wakawasha kila mmoja na wake wakaanza kuvuta,kwa kweli roho iliniuma sana kuona askari na kombati zake anafanya kitu kama hicho,ilikuwa giza nilishindwa kuchukua namba zake
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  acheni wivu wakike huo mlitaka asikali na maisha yao magumu wale wapi??
  ninyi mnaiba na kuingiza madawa tena na vyeo vyenu mnataka askali wazuie nini?
  nani kakuambia askali hapendi kazi yake azuie mzigo afukuzwe kazi?
  MWISHONI WACHENI MAISHA YAENDE KAMA YALIVYO, NCHI IMEOZA KILA MAHALI!
   
 10. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Engare Nanyuki kisimiri juu wanalima kwa trakta
   
 11. papason

  papason JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  mbona nyie kila siku mnaburudika kwa mi beer, mi gin, mi wine, mi whisky etc waacheni vijana nao wasahau matatizo yao kwa kupata 'mmea wa kondeni' hayo mambo tangu enzi za mitume...IRE!!
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hii ni hatari kubwa sana kwa taifa!
  Inashangaza sana kuona every thing going wrong.......this country bwana dah!
   
 13. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280  Jamani tupeane pole tu. Matatizo haya yote yanatokana na uongozi mbovu wa mheshimiwa Mtukufu Dr. rais Kikwete. Nasema hivi kwa sababu huyu rais ana wakilishi wake hizi sehemu ulizozitaja kama vile wakuu wa wilaya na mikoa. Mkuu wa wilaya anawasilisha mada kwa mkuu wa mkoa, na mkuu wa mkoa anawasilisha kwa bosi wake ambaye ni waziri wa serikali/tawala za mikoa n.k. kama sijakosea na huyu waziri yuko chini ya Kikwete. Kutokana na malalamiko uliyoyatoa hapo juu, inadhihirisha moja kwa moja kwamba nobody cares. Cha kusikitisha ni kwamba hiki ni kizazi cha kesho, na pengine hawa viongozi wanafanya hivi makusudi tu kuwaachia wananchi wazuzuke na bangi ili waendelee kutuibia. Kwa mpangilio huu Tanzania tutazidi kuangamizwa na jirani zetu wa EAC wanaokuja kuchukia ardhi yetu na kutokuwa na viongozi wa kututetea, tutaenda wapi?
   
 14. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwa style hii basi miaka michache ijayo Tanzania itajaa wendawazimu!
   
Loading...