IGP Mangu: Sina taarifa juu ya agizo la Rais kumpandisha cheo askari

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,682
239,222
Amesema hajapewa taarifa za Rais Magufuli kuagiza koplo Deogratius Mbango kupandishwa cheo baada ya kumdhibiti mke wa mmoja wa mawaziri wa serikali yake kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani.

" Bado hajapandishwa cheo kwa sababu sijapewa taarifa hizo na nitakapopewa taarifa atalazimika kwenda kwenye mafunzo kwanza, sisi jeshi la polisi tuna taratibu zetu" alisema IGP Mangu .

Chanzo: Nipashe

MyTake - ng'ombe wa masikini hazai .
 
Nafikiri kabla ya rais kutoa le tamkooooz ni vizuri akawa anawasiliana na taasisi husika,kila taasisi ina taratibu zake za upandaji cheo,kuna vyeo vya ujaji wa mahakama kuu kuna taratibu,kuna kupanda ngazi uwakili wa serikali kuna taratibu,jeshi la wananchi pia,ifikie ajifunze kwamba taratibu na sheria zipo miaka mingi sana,hii nchi haijaanza juzi, sasa kama huyo askari akishindwa mafunzo?si lazima akikose cheo? Sheria,sheria,sheria,kuna siku mtu Mwenye V moja atapewa u-IGP,nafikiri pia polisi watakuwa wanawavizia watu wenye vyeo wawadhalilishe huku wanawarekodi wakitazamia kupanda cheo,mapolisi ni mabingwa wa kubambika kesi
 
Amesema hajapewa taarifa za Rais Magufuri kuagiza koplo Deogratius Mbango kupandishwa cheo baada ya kumdhibiti mke wa mmoja wa mawaziri wa serikali yake kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani .

" Bado hajapandishwa cheo kwa sababu sijapewa taarifa hizo , na nitakapopewa taarifa atalazimika kwenda kwenye mafunzo kwanza , sisi jeshi la polisi tuna taratibu zetu " alisema IGP Mangu .

Chanzo - nipashe

MyTake - ng'ombe wa masikini hazai .
kumbe chanzo cha habari chenyewe ni gazeti la nipashe.
 
Mbona wengi wanapandishwa humu hawaendi mafunzo? Uwaziri ubunge ukuu wa wilaya au mkoa mbona hauna vyuo? Yye ampe huyo jamaa haki yake basi
Jamani, we vipi? Kuna vyuo vya mawaziri? Polisi hawapandishwi kiholela ni lazima upitie mafunzo ya ngazi hiyo. Ukifaulu ndo unapandishwa na wala siyo kwa maagizo. Angeagiza apewe kiasi fulani cha pesa kwa ujasiri wa kupambana na mke wa diplomat.
 
Back
Top Bottom