Kama wasaidizi wa Kingai wamepandishwa vyeo, siku si nyingi mamlaka ya RAIS itampandisha cheo kuwa SACP/DCP/CP au IGP

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Siyo watu wote waliofanya uovu uadhibiwa na mamlaka za kibinadamu. Wengi wa wahalifu ufanya uhalifu baada ya kuingia mkataba wa uhalifu na wanapendezwa na huo uhalifu. Yawezekana kama wakina Kingai walifanya mateso waliyoeleza watuhumiwa kesi ya Mbowe basi walisaini mkataba wakuifanya kazi hii Kwa makubaliano flani ikiwemo promotion.

Ni vigumu mkataba huu kuvunjwa Kwa sababu una element za kiapo kwamba naahidi kufanya Kwa makubaliano flani. Kazi zilizofanywa nje ya mkataba zinapobainika hatua za kisheria uchukuliwe,rejea kesi ya Zombe. Naamini kwa Taarifa aliyotoa Jumanne mahakamani kwamba mashahidi wote wamepandishwa vyeo akiwemo mahita aliyepo kozi maana yake Kingai hajapandishwa kwa sababu mamlaka yake Kwa cheo kipya Kwa mujibu ya zinavyosoma kanuni zao ni Mhe. RAIS wakati akina Jumanne ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Taarifa hii inaamanisha jina la Kingai tayari limependekezwa kwa promotion likisubiri mkeka kutoka Ikulu.

Sitaki kuamini kwamba watendaji Hawa wa Polisi walifanya uhalifu unaoelezwa na watuhumiwa ila nataka kuamini kwamba walishiriki kwanamna Moja au nyingine kutekeleza Amri isiyo halali.

Hukumu Yao haiwezi kutolewa na mwanadamu wa cheo chochote maana viongozi wote wamefungwa na kifungo Cha mkataba kwamba tunafanya then mtatulipa na atutaadhibiwa.
 
Jinai ni jinai tu Wala haizeeki na malipo yake ni hapa hapa Duniani Wala siyo kwa mungu ni swala la muda tu, hao walio mtuma watakapo kuwa hawana hiyo dhamana ya uongozi Wala hawezi kumlinda Tena
 
Awamu iliyopita wenye tamaa haramu wengi walipanda vyeo ikiwemo kupata teuzi kwa kuwashughulikia au kuwatusi wapinzani Ili kumfurahisha bwana yule.

Mahakimu waliowafunga wapinzani walipewa ujaji.Ma rpc waligombea kuwashughulikia wapinzani kwa wimbo wa intelligencia.
Kihongosi alipewa udc baada ya kutishia kumuua Zito.Mwigulu alirudi jikoni baa6 ya kutumia dakika 4 kumsifia jiwe aliponangwa kajificha corona Chato.

List ni wengi walipewa vyeo teuzi sio kwa cv bali kuimba kwaya
 
Pamoja na afya njema, utajiri mkubwa kwa mwanadamu ni amani ya moyo na sio pesa, madaraka au umaarufu. Kwakifupi hawa wote kina Jumanne and his Co. Hawawezi kuwa na amani mioyoni mwao tena kwasababu ya matendo yao na hii ipo kwa Askari polisi wengi.

Kabendera amepost kumjua huyu afande Jumanne. Na mimi moja ya comments kutoka kwa wachangiaji nilizopenda ni hii hapa:

Alitumika Sana na shetani.Mungu Ni mwema moja kafa .moja yupo ndani miaka 30 na makesi kibao na moja kawa mzurulaji tu hata Kama Ana hela hayupo happy na kapoteza marafiki wengi .na lingine limepoteaza uspeaker kwa mikono yake tutawajuwa wengi tu
 
Siro, Kingai, Jumanne, Goodluck, Mahita na vizazi vyao vyote. Walaaniwe....waishi maisha marefu yenye mateso. Siyo kwa ukatili wanaoufanya
Hakika hawa watu ukiweza pata tap back record phone calls zao wamebeba Siri nyingi sana.
Wadukuzi wa call Wana Siri nyingi sana.
Hawa wanawajua wasiojulikana wote plus matukio yote ya uovu wa shetani.
Nature inakulipa ulivyotenda ile albadili inaendelea na Kazi juzi imekula ndugai hadi iwamalize wote waliowaumiza watz.
Ukoo mwingine damu zao huwa hazipotei bure kulingana na maagano yao.
 
Hivi kwa Nini utese na kuua watu ndipo update cheo? Uadilifu ni Bora kuliko utiifu. Miaka ya anko Magu upendo ulipotea na unafiki wa watu kwa rais uliyamalaki. How do you feel the guilty inside you? Kifo chenu kitakuwa kibaya kuliko Cha mbweha
Ukiua mtu umewasha bluetooth on maisha yako yote.
Na Sio KILA ukoo damu zao upotea bure,damu ikitoka urudi na damu,so wauaji mjiandae.
 
Back
Top Bottom