IGP Kumshauri Rais kuna ubaya?

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,440
Hili jambo linamsikitisha kila Mtanzania mwenye akili timamu.Kuna kamatakamata kila kona ya nchi hii. Nyingi ni za kisiasa, na hii inatokana na Tamko la Raisi la kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa.

Sasa kwa kuwa Nina imani IGP ni mtu anayeijua sheria vizuri, kwanini asimshauri Rais atengue hilo Tamko kwa sababu kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania Raisi tayari amevunja katiba.

Kitendo cha Rais kwenda kinyume na katiba aliyoapa kuilinda, kinatoa taswira mbaya sana. Matokeo yake yameanza kuonekana ni usumbufu usio na lazima kwa Jeshi la polisi.

Nina imani polisi na wao wanajua kuwa wanachokifanya ni makosa na ni kupoteza muda wao ambao wangeutumia kwa mambo ya maana zaidi, ni dhahiri pasi na Shaka kuwa polisi wanajua hizi kesi zikifika mahakamani serikali utashindwa.

Nina imani Rais ni mtu msikivu, nami pia Kama raia mwema namshauri, Aongoze nchi kwa mujibu wa katiba aliyoapa kuilinda.Vinginevyo atajikuta anapambana na wanasiasa badala ya kupambana kuletea wananchi maendeleo.

Mwaka wa kwanza ndiyo huo unakatika. Kuna mengi umeahidi wananchi.sasa hivi hali za wananchi ni mbaya Mara 2 zaidi ya tulikotoka. Watu wameanza kuchoka utawala huu mpya.

Kila siku ni matamko tu. Hakuna hata moja linalotekelezeka, viongozi wasipokuwa makini, watashangaa miaka mitano waliyopewa inakatika na hakuna walichokifanya zaidi ya kamata kamata.

God bless us.
 
Wana create Bomu la kimya kimya LA uasi bila wao kujua, hekima na busara inabidi itume na sio kukaribisha mianya ya kuanza uovu, lazima jamii iachwe ipumue, since last year nchi inapitia wakati mgumu mno Mungu asaidie tu aisee, ubabe wa kijinga ukae pembeni busara itawale.
 
Anafikiri neno mtawala ni kutumia mabavu na polisi! Tatua kero za wananchi sio kukamata wapinzani wasio na kosa ili kuwatisha!! Hataweza! Kizazi hiki sio kile! Nchi sio yake pekeyake kwa nini anatuchezea akili? Kila tamko halina mantiki wal faida kwa Taifa! Nchi hii haina wazee , anapotea! Tunahitaji ajira madawa pembejeo mikopo ya wakulima na vijana...sio kutishana kwa mkono wa dola! Saa ngapi hizo dola zitafanya kazi yake??
 
Wajumbe ndiyoo hao ataanzia wapi labda kwa mfano?
Mkuu, hakuna kauli iliynishangaza Kama ile aliyotoa kwamba kila mwanasiasa aliyechaguliwa afanye siasa ktk jimbo lake tu. Sasa nikajiuliza, akina Kinana na Ole Sendeka ni Kama hawana tena kazi ya kufanya.kauli nyingine kwa kweli! Mhh!
 
Kuna jamaa aliandika kwenye ukurasa wake wa fb wiki iliyopita kwamba kuna mwenyekiti wa chama kimoja wapo cha siasa hataki kushauriwa, yaani inafika wakati yeye (mwenyekiti) ndo anawashauri washauri wake, teh! teh!
 
Tunaposema Magufuli mkurupukaji watu hawaelewi, nilishangaa aliposema siasa hadi 2020 then anabadilika anasema wafanye kwenye majimbo waliposhinda dah... Mwenyewe anajua afanyacho anakurupuka sana ngoja tusubiri ndio shida urais wa kupewa na Lubuva
 
Hahahaa, mkuu wakati naandika huu uzi kuna habari zimenifikia punde. Kuwa kuna kamata kamata inaendelea muda huu hapo hapo mahakamani. Hii ni kuwapa watu umaarufu wa bure bila sababu
Mkuu poa, nami nimesoma hapa kuwa kiongozi wa Bavicha Mwita kakamatwa. Kuna wengine? Lete updates za kamanda Lissu.
 
Cjui kwa nini rais wetu kaingia/kajiingiza ktk huu mtego wa kutaka kujibu kila kitu!
 
lipo alilolitekeleza si amehamasisha upatikanaji wa madawati...nadhani ivi sasa wadogo zetu wanakaa kwenye madawati ila hawana vitabu wala walimu.
 
Mkuu poa, nami nimesoma hapa kuwa kiongozi wa Bavicha Mwita kakamatwa. Kuna wengine? Lete updates za kamanda Lissu.
Mkuu mpaka sasa hivi hakuna dalili ya kiwanda hata kimoja, na vinavyozalisha vimepunguza uzalishaji for 50% demand ipo chini kabisa, sasa la viwanda limesahaulika limeibuka jipya la kuhamia Dodoma. Wataalam wa hesabu wanakwambia garama za kumhamisha mtumishi mmoja wa wizara siyo chini ya mil.14.hizo pesa zitatoka ktk bajeti gani, hakuna ajuae. Ila wenye akili tumeshagundua mkwamo mkubwa mbeleni.
 
Mkuu, hakuna kauli iliynishangaza Kama ile aliyotoa kwamba kila mwanasiasa aliyechaguliwa afanye siasa ktk jimbo lake tu. Sasa nikajiuliza, akina Kinana na Ole Sendeka ni Kama hawana tena kazi ya kufanya.kauli nyingine kwa kweli! Mhh!
JF ni raha maana kuna majibu hadi anaingia mitini.
 
Mimi sina sababu ya kuMlaumu magu; amewekwa madarakani na waliomuweka. Iwe sisi wananchi, CCM au TISS magu ndiye mtawala hastahili lawama. Ni kama waliomuweka madarakani waliamua kutuingiza kwenye hili janga. Waswahili tunasema KILA MCHUMA JANGA HULA NA WAKWAO. TUNALO SUALA LILILOPO NI MAPAMBANO HADI JANGA LITOKOMEE
 
Ngosha, wananchi wako tunataka maendeleo achana na kina T. Lissu unawapa umaarufu bure! mbona ulianza vizuri,lakini kwa sasa unakoelekea sipo!Nahisi kuna kundi linakupa ushauri ili ualibikiwe.
 
Back
Top Bottom