IGP ateua makamanda wapya wa mikoa, AHMED MSANGI AULA

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,195
2,000
Taarifa ya IGP ya uteuzi wa Makamanda wa Polisi wa Mwanza, Mbeya na Simiyu
08/12/20130 Comments

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amefanya uteuzi wa Makamanda wa Polisi kwa Mikoa mitatu Mwanza, Mbeya na Simiyu, ambapo amemteua Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Valentino Mlowola kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ahmed Msangi kuwa Kamanda wa Polisi mkoa
wa Mbeya na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Charles Mkumbo kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, SACP Salum Msangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.


Aidha, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Ibrahim amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Rogathe Mlasani kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.


Wengine ni Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Martin Otieno kutoka Kanda Maalum ya Dar es salaam amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi kuwa Mkuu wa kitengo cha Teknohama na Mrakibu wa Polisi (SP) Gidion Msuya ambaye alikuwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Tarime Rorya amehamishiwa Tunduru kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD).


Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Source: Taarifa ya IGP ya uteuzi wa Makamanda wa Polisi wa Mwanza, Mbeya na Simiyu - wavuti.com
 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
Msangi yule aliyemng'oa kucha Dr Ulimboka kapandishwa cheo na kali zaidi kapelekwa Mbeya?
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,636
2,000
Kumbe kuna Ahmed Msangi na Salum Msangi! Familia nyingine zinapenda kazi moja!
 

Mhonzuyadilu

Senior Member
Oct 28, 2012
156
0
Msangi yule aliyemng'oa kucha Dr Ulimboka kapandishwa cheo?

Tunaposema inchi ilishawekwa mfukoni na baadhi ya wahuni wachache watu wahaelewi ona tena haya majanga.jamani jamani basi tu kuishi inchi kama ni kuzidi kujiongezea presure tu.
 

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,774
2,000
Huyo msangi mng'a meno na kucha huko mbeya tayari muandike maumivu na muwe mnatembea na ganzi.
Viva home boy mkumbo.
 

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,113
2,000
Naona Kaka Yake Ahmed Msangi , Salum Msangi aliyekuwa RPC Simiyu kahamishiwa makao makuu.. kina Msangi wana bahati kweli Baba alkuwa RPC na watoti wawili MaRPC.... Anyway Diwani Athuman aliekuwa Mbeya kaenda wapi??
 

Vitaimana

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
3,542
2,000
Mbeya haitakuwa shamba la bibi amuulize Kova kabla hajawa promoted kuja Dar.
 

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,661
2,000
Mwema, Msuya, Mlasani, Msangi Chagonja.hawa watu ni makini na wanastahili utumishi uliotukuka.
 

Fede Masolwa

Verified Member
Oct 26, 2013
528
195
msangi mbeya ni pagumu sanaaaaaaa, sio dar kuna wanyia wana roho ngumu wanakata vichwa
 

kamanda wa kamanda

Senior Member
Oct 12, 2013
191
225
Naona Kaka Yake Ahmed Msangi , Salum Msangi aliyekuwa RPC Simiyu kahamishiwa makao makuu.. kina Msangi wana bahati kweli Baba alkuwa RPC na watoti wawili MaRPC.... Anyway Diwani Athuman aliekuwa Mbeya kaenda wapi??

Athuman diwani kimepanda ameamia makao makuu Dar
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom