Ifikie mahali Sir Pep Guardiola apewe tu heshima yake

Tipstipstor

JF-Expert Member
Nov 29, 2021
1,531
3,331
Ahlan wa sahlan

Wakati ulimwengu ukifurahia kuwaona wachezaji magwiji wawili walioitikisa dunia ,namaanisha Mreno Sir Cristiano Ronaldo na Sir Lionel Messi, tunasahau kuwa hakuna kocha aliyewahi kufundisha mpira wa burudani na wa ushindi kama Mhispania Sir Pep Guardiola.

Sir Guardiola hapewi heshima inayostahili kutokana na umahiri wake ,kila timu anayohamia huwa anahama na mpira wake, wakati anaondoka Barcelona,wengi walimbeza kuwa alikuwa akibebwa na umahiri wa kina messi,iniesta na xavi. Aliwathibitishia kuwa si kama wanavyodhani wakosoaji wake, alikwenda kuibadilisha bayern Munich kutoka ktk mpira wao wa kupiga mashuti mpk kutandaza pasi safi. Vivyo hivyo alipofika Man city aliweza kuvunja utawala wa klabu pinzani kama watani wao wa jadi Man utd ambao hivi punde wametoka kubugizwa na kushindiliwa bakora nne, chelsea na liverpool.

Itoshe kusema kuwa unaweza kumdhibiti Sir Guardiola katika mechi moja ila huwezi kumzuia katika ligi. Licha ya ushindi wanaoupata Man city bado wanapata na burudani safi ya kushuhudia timu yao ikiwadhalilisha wapinzani mpira huu naufananisha na mpira wanaoucheza mabingwa wa soka la Tanzania Simba Sc ambao wanafundishwa na mrithi wa Guardiola , Sir Pablo Franco Martin ambae pia anatokea Hispania.

Naamini Sir Pep hatakama utampeleka katika klabu ya wanalizombe,Maji maji ya Songea bado ataweza kuibadilisha na kuwa tishio sio tu Tanzania bali Africa nzima.

Sir Guardiola umezidi kuwaonea Manchester United, mechi ya kwanza msimu huu walicheza dk 25 za mwisho padi na kugusa mpira ,leo umeamua kuwachezesha dk 45 zote za kipindi cha pili pasi na kugusa mpira.
 
Mungu akinijaalia uhai nitakuja kuwasimulia wajukuu zangu juu ya umahiri wa huyu Mhispania.
 
Ifikie hatua utambue duniani hatufanani kwa kila kitu, kumpenda kwako Pep Kipara kunatosha sana kuliko kutuhamasisha sisi tusiomkubali tumpende.

Kwanini upendwe na Watu wote ilihali wewe mwenyewe huwezi kumpenda kila Mtu duniani

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
Utakuwa umepigwa na kitu kizito chenye ncha kali usiku wa leo. Hongera Sir Pep
 
Mpira wake huo akikutana na team yenye kasi inayopiga quick counter attack kama liverpool anapasuka nyingi tu kama leo kama man u wangekuwa makini ile mechi walikuwa wanamaliza mapema tu.
Huyo liverpool mwenyewe anapasuka mbele ya Sir Pep Guardiola
 
Sir Klopp ni miongoni mwa makocha bora kwa sasa hapa ulimwenguni, yeye na Sir Thomas Tuchel ni miongoni mwa makocha wachache sana wanaoweza kumsumbua Guardiola
 
mpira huu naufananisha na mpira wanaoucheza mabingwa wa soka la Tanzania Simba Sc ambao wanafundishwa na mrithi wa Guardiola , Sir Pablo Franco Martin ambae pia anatokea Hispania.
1646595898773.png

Makolo mnazingua sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom