Unaambiwa Pep Guardiola 'hapatikani' na hatumii simu yake ya mkononi, ajificha kuokoa Jahazi la Man City

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
2,069
5,679
Kocha mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, anadaiwa kuwa "hapatikani" na hatumii simu yake ya mkononi, huku muda mwingi akijifungia ofisini akijaribu kutafuta njia ya kutoka kwenye hali ya vipigo mfululizo vinavyoikumba timu yake.

Guardiola, ambaye anasifika kwa mbinu na Soka safi amekumbana na vipogo saba mfululizo bila kuonja ushindi na Man City, anapambana kutafuta suluhisho la haraka kwa hali mbaya ya timu hiyo.
IMG_1210.jpeg

Taarifa za ndani zinadai kuwa kocha huyo anajaribu kufikiria mikakati mipya ya kuirejesha timu hiyo kwenye ufanisi baada ya mfululizo wa matokeo mabaya.
 
Kwahiyo umeamua kututisha sisi Washika bunduki wa London eeh?

Hata hivyo akisubiri January, mbona atakuta mwana si wake
Hahahaa mwana Arsenal unakumbuka kilichotokea msimu uliopita Inatakiwa timu itakayokuwa kileleni kufikia mwezi wa tatu iwe imeizidi Man City si chini ya point 18 kwa kuanzia zaidi ya hapo ubingwa utarudi mikononi mwa kipara..... Jurgen Klopp na Mikael Arteta wanaelewa vizuri hili
 
Back
Top Bottom