Ifikie hatua uwanja wa taifa upewe jina

Ifikie hatua uwanja wa taifa upewe jina

Umewaza mbali mkuu, ila ni vyema ungeitwa Nyerere stadium

Sent using Jamii Forums mobile app
Aaaahg kila kitu Nyerere,sijui daraja kigamboni yeye,mara airport yeye,eeh vyuo navyo yeye,tufikie hatua tumwache mwalimu apumzike maana naona anajing'ata kila leo huko aliko.i like Tanzanite arena or Serengeti stadium au bora Estadio de Kilimanjaro.
 
Ukiwa unauingia uwanja huu wa kisasa na mkubwa kuliko ata viwanja vingi barani ulaya na Africa, unakutana na bango kubwa mbele yake linaloutambulisha uwanja huo kwa majina ya 'Tanzania National Main Stadium' kwa tafsiri isiyo rasmi sana 'uwanja mkuu wa Taifa', na hili ndio jina lake, jina lilobuniwa na watu ambao uenda ni wasomi kabisa na wana exposure kubwa tu ya kuzunguka huku na huko.

Asee kituko iki kinachekesha sanaa maana ni sawa na kumtaja mnyama kwa wajihi wake, na kusema tu huyu ni mbwa, sasa nani asiejua kua uyo ni mbwa? Wewe sema Jina lake nani?

Duniani kote kila nchi ina uwanja wa taifa lakini vyote vina majina yake na yenye kuleta maana tu, majina yapo mengi sana ambayo yangekua kama utambulisho wa taifa kwa namna yake, sasa uwanja mzuri kama huu wetu wa taifa si ungeitwa tu ata 'Mwalimu Nyerere Stadium' au 'the Serengeti Arena' au ata Tanzanite Stadium na majina mengi tu yenye maana kubwa hapa nchini.

Sasa et uwanja unaitwa Tanzania National Main stadium? Sasa si kituko hiki au? Ni hatujui kiingereza au tunajua national main stadium ni bonge la jina la kimataifa? Tunatia aibu bhana hasa nyie TFF, acheni zenu uwanja upewe jina ilo, kama uko vijijini tu Ng'ombe wanapewa majina mazuri tu na hawaitwi 'Cow' kama nyie mlivyofanya, sasa mnashindwa wapi nyie? Muuite ata Chief Mkwawa Stadium.
Kuna habari kwamba iliwahi kupendekezwa kwamba uitwe Benjamin William Mkapa Stadium, kama kumpa Heshima huyu mtu kwa kuujenga uwanja, lakini kwasababu finishingi ilifanyika kipindi cha JK, etiI kukawa na mvutano kwamba uitwe Jakaya Mrisho Kikwete Stadium hii ni kwa wale waliokuwa wanajipendekeza kwa utawala uliopo, na kwasasa kuna habari kwamba kuna watu eti Wanataka uitwe John Pombe Magufuli Satdium. Kwahiyo tusubiri jina laweza kutoka mda si mrefu
 
Aaaahg kila kitu Nyerere,sijui daraja kigamboni yeye,mara airport yeye,eeh vyuo navyo yeye,tufikie hatua tumwache mwalimu apumzike maana naona anajing'ata kila leo huko aliko.i like Tanzanite arena or Serengeti stadium au bora Estadio de Kilimanjaro.
Majina matamu kinyama. .....
Natamani yangekuwepo kipindi cha finali ya sportpesa alafu umkute mtangazaji mwenye mbwembwe anataja hilo jina la mwisho la kifaransa......wacha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom