Ifikie hatua uwanja wa taifa upewe jina

Ifikie hatua uwanja wa taifa upewe jina

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,710
Reaction score
4,044
Ukiwa unauingia uwanja huu wa kisasa na mkubwa kuliko ata viwanja vingi barani ulaya na Africa, unakutana na bango kubwa mbele yake linaloutambulisha uwanja huo kwa majina ya 'Tanzania National Main Stadium' kwa tafsiri isiyo rasmi sana 'uwanja mkuu wa Taifa', na hili ndio jina lake, jina lilobuniwa na watu ambao uenda ni wasomi kabisa na wana exposure kubwa tu ya kuzunguka huku na huko.

Asee kituko iki kinachekesha sanaa maana ni sawa na kumtaja mnyama kwa wajihi wake, na kusema tu huyu ni mbwa, sasa nani asiejua kua uyo ni mbwa? Wewe sema Jina lake nani?

Duniani kote kila nchi ina uwanja wa taifa lakini vyote vina majina yake na yenye kuleta maana tu, majina yapo mengi sana ambayo yangekua kama utambulisho wa taifa kwa namna yake, sasa uwanja mzuri kama huu wetu wa taifa si ungeitwa tu ata 'Mwalimu Nyerere Stadium' au 'the Serengeti Arena' au ata Tanzanite Stadium na majina mengi tu yenye maana kubwa hapa nchini.

Sasa et uwanja unaitwa Tanzania National Main stadium? Sasa si kituko hiki au? Ni hatujui kiingereza au tunajua national main stadium ni bonge la jina la kimataifa? Tunatia aibu bhana hasa nyie TFF, acheni zenu uwanja upewe jina ilo, kama uko vijijini tu Ng'ombe wanapewa majina mazuri tu na hawaitwi 'Cow' kama nyie mlivyofanya, sasa mnashindwa wapi nyie? Muuite ata Chief Mkwawa Stadium.
 
Kutokana na kazi nzuri anazopiga mh Rais tuuite Maguful National Stadium (MNS) ili kuendeleza heshima na uchapakazi wake ambao sasa umekua gumzo duniani kote kias cha watu kufanya kampen za uchaguzi kwa kumtumia km rol modo wao...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uwanja ukipewa hili jina hakuna mechi tutakayo shinda ndani ya uwanja huo.
 
Timu ya taifa tu inaitwa "taifa stars". Unategemea uwanja uwe na jina???
 
Kwaio kila shule, barabara na mavyuo yote yenye jina lake yeye ndio alivijenga? Kwaio uitwe kwa jina alieujenga sio? Haya wachina ndio wameujenga so what? Wauite Jack Chen stadium?
Au wauite Ching yu lu ho
 
Ukiwa unauingia uwanja huu wa kisasa na mkubwa kuliko ata viwanja vingi barani ulaya na Africa, unakutana na bango kubwa mbele yake linaloutambulisha uwanja huo kwa majina ya 'Tanzania National Main Stadium' kwa tafsiri isiyo rasmi sana 'uwanja mkuu wa Taifa', na hili ndio jina lake, jina lilobuniwa na watu ambao uenda ni wasomi kabisa na wana exposure kubwa tu ya kuzunguka huku na huko.

Asee kituko iki kinachekesha sanaa maana ni sawa na kumtaja mnyama kwa wajihi wake, na kusema tu huyu ni mbwa, sasa nani asiejua kua uyo ni mbwa? Wewe sema Jina lake nani?

Duniani kote kila nchi ina uwanja wa taifa lakini vyote vina majina yake na yenye kuleta maana tu, majina yapo mengi sana ambayo yangekua kama utambulisho wa taifa kwa namna yake, sasa uwanja mzuri kama huu wetu wa taifa si ungeitwa tu ata 'Mwalimu Nyerere Stadium' au 'the Serengeti Arena' au ata Tanzanite Stadium na majina mengi tu yenye maana kubwa hapa nchini.

Sasa et uwanja unaitwa Tanzania National Main stadium? Sasa si kituko hiki au? Ni hatujui kiingereza au tunajua national main stadium ni bonge la jina la kimataifa? Tunatia aibu bhana hasa nyie TFF, acheni zenu uwanja upewe jina ilo, kama uko vijijini tu Ng'ombe wanapewa majina mazuri tu na hawaitwi 'Cow' kama nyie mlivyofanya, sasa mnashindwa wapi nyie? Muuite ata Chief Mkwawa Stadium.
Jina lipo kitambo, ni KIKWETE STADIUM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umewaza mbali mkuu, ila ni vyema ungeitwa Nyerere stadium

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kila kitu tutakiita kwa jina la nyerere?? Hapana kuna majina mengi yakujivunia zaidi ya hilo..wanasema tanzanite ipo Tanzania pekee lakini kuna nchi nyingi zimetengeneza bidhaa na kuziita tanzanite huku wenye tanzanite zetu tumekaa tu bila lolote..bora uwanja Wa taifa upewe jina tanzanite stadium

young kilimanjaro
 
Kutokana na kazi nzuri anazopiga mh Rais tuuite Maguful National Stadium (MNS) ili kuendeleza heshima na uchapakazi wake ambao sasa umekua gumzo duniani kote kias cha watu kufanya kampen za uchaguzi kwa kumtumia km rol modo wao...

Sent using Jamii Forums mobile app
ukiitwa hivo tujiandae kushika mkia kwenye viwango vya fifa
 
Back
Top Bottom