SoC01 Ifahamu OSINT - Open Source Intelligence na umuhimu wake kwa sekta binafsi Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Environmental Security

Senior Member
May 21, 2020
181
261
Kila siku zaidi ya tweets milioni 500 zinaandikwa na watu mtandaoni duniani ambazo ni sawa na tweet bilioni 200 kwa mwaka duniani. Ongeza na picha zinazokadiriwa kufika milioni 350 ambazo huwekwa facebook na watumiaji, jumlisha na zaidi ya masaa 720,000 ya maudhui ya video mpya zinazowekwa YouTube ndani ya kila saa 24 duniani, pia inadhaniwa kuna zaidi ya comment zaidi ya 500,000 kila siku duniani. Hapo utaanza kuelewa kwanini hizi zinaitwa zama za taarifa, “The Information Age”.

Katika zama hizi tunazoishi sasa, taarifa ndio kila kitu katika uendeshaji wa serikali, mashirika, makampuni na taasisi mbalimbali binafsi na za uma, ili kuwezesha kitu kinaitwa "informed decisions"

Mara baada ya utangulizi huo, nipende kujikita ktk kueleza juu ya mbinu mojawapo muhimu sana ktk kukusanya taarifa ijulikanayo kama OSINT - Open Source Intelligence, iwe ni kwa matumizi ya taasisi muhimu za uma au binafsi. Lakini leo nitajikita ktk kuielezea OSINT kwa upande wa sekta binafsi na mtu mmoja mmoja.

OSINT ni nini?
Open Source Intelligence (OSINT) ni mbinu ya ukusanyaji wa taarifa (intelligence) ambazo vyanzo vyake ni vya wazi na vinaruhusiwa kufikiwa na jamii kwa ujumla wake.

Ni zile taarifa ambazo zimeruhusiwa kwa matumizi ya uma na hazihitaji mtu kuwa na ujuzi fulani wa hali ya juu, au matumizi ya vifaa maalum sana ili kupata taarifa hizo.

OSINT inahusisha ukusanyaji wa taarifa zote kutoka katika vyanzo vya wazi kama internet/kugoogle, magazeti, maandiko ya kitaaluma (journals), majukwaa ya uma kama jamii forum, magroup ya WhatsApp, facebook, (social media), ripoti za serikali, kutazama video mitandaoni, matangazo, picha, kuangalia televisheni, kusikiliza redio, tafiti (research), taarifa za kijiografia pia inahusisha kuangalia profile za watu au taasisi walizoweka mtandaoni, lakini haihusishi kuiba password zao na kuingia au kuhack au kutumia mbinu nyinginezo za kijasusi.

Nani hasa wanaweza kutumia OSINT?
Mbinu za OSINT hutumiwa na watu mbalimbali kama wapelelezi, wachunguzi, wachambuzi, waandishi wa habari za kiuchunguzi, watafiti, wasimamia sheria, wanausalama wa mtandaoni (cyber security), pia zanaweza kutumiwa na watubinafsi. Lakini leo nataka nijikite juu ya umuhimu wa OSINT kwa sekta binafsi hasa wafanyabiashara, makampuni na mashirika.

Wafanyabiashara, makampuni na mashirika kwa nyakati tofauti wamejikuta katika kuhitaji kufanya maamuzi muhimu lakini wakajikuta hawana taarifa za kutosha kujiridhisha juu ya maeneo fulani ya kuyafanyia maamuzi kwaajili ya taasisi zao. Hapa ndipo OSINT inakuja kuwa mbinu muhimu kuleta majawabu au taarifa muhimu kwa wakati unaofaa ili zitendewe kazi kwa manufaa ya taasisi husika.

Mf. Kwa kutumia chanzo kikubwa sana cha taarifa kwasasa ambacho ni mitandao ya kijamii, taasisi mbalimbali za kibiashara zinaweza kuweka namna bora ya kupata taarifa muhimu (intelligence) kuhusu mtazamo wa jamii juu ya biashara yao, kujua mwenendo wa kibiashara wa washindani wao, kujua uhitaji wa soko, kujua hatari ambazo zinaweza kuathiri biashara, kuweka mkakati wa kushawishi jamii au kutoa elimu na matangazo yanayowahusu, kupata masoko mapya, na ubunifu mwingine.

Ni wakati sasa sekta binafsi kwa mmoja mmoja kuanza kufikiria ktk kuwekeza vyakutosha ktk eneo la ukusanyaji taarifa nyeti (intelligence) zinazowagusa kwa namna moja au nyingine, na mbinu rahisi kutumia kwa kuanzia ni OSINT ambapo haitoi nafasi kwa mikwaruzano na washindani au taasisi nyingine sababu chanzo cha taarifa ni OPEN.

Ukifanikiwa ktk ulingo wa taarifa (intelligence) kwamaana ya utafutaji, ukusanyaji, uchambuzi/analysis na kufanya maamuzi sahihi (informed decision) unakuwa umefanikiwa sana katika kudhibiti na kusimamia mwenendo wa shughuli zako lakini pia kuwadhibiti washindani.

Nataka nipate nafasi niandike vizuri sana juu ya OSINT na tools zake ili iwe rahisi mtu kuamua kuanza kutumia.

Ni wakati sasa sekta binafsi ijikite ktk intelligence, iwe na skilled personnel, iwe na vitengo hivyo, ili kuweza kuwa na uwezo wa kuhimili ushindani na kujifanya zaidi kwa kupunguza kabisa viwango vya risk.
Serikali pia iweke dirisha la kufacilitate intelligence kwaajili ya kuibeba sekta binafsi kimkakati hasa ya viwanda vya waTanzania na maeneo mengine ya kimkakati kama kilimo na uchumi wa bluu.

OSINT ni hatua nzuri, rahisi na muhimu kuanzia.

Na-pause kwa leo.
Nitaendelea.
 
Wewe umesoma Cyber security laazima
its not a must that he leant abaut cybersecurity, hii ni kitu kila mtu anaweza fanya, yaani this days without data collection and proper analysis of the said data, you as a company, as an individual of you as a gorverment your failure is CERTAIN, and this is the main reason our country tz will lag behind, will remain in abject poverty coz our gava is not capable of doind such things, data collection and proper analysis is a multi billion dollar bussiness today, be blessed
 
OSINT nimeisoma kwa Dave Majumdar na naendelea kuitumia itanisaidia. Wengi wanaitumia bila kuijua mfano utakutana na kina Rrondo na Extrovert wanayajua magari, hiyo ni OSINT wanatumia
 
Voted, hivi hata serikali si ingekua na means ya ku collect data kujua public opinion kabla ya ku finalise mambo? Si ingekua hivyo kwa kitu ulichoandika au nimekwenda off point?😊😊
 
its not a must that he leant abaut cybersecurity, hii ni kitu kila mtu anaweza fanya, yaani this days without data collection and proper analysis of the said data, you as a company, as an individual of you as a gorverment your failure is CERTAIN, and this is the main reason our country tz will lag behind, will remain in abject poverty coz our gava is not capable of doind such things, data collection and proper analysis is a multi billion dollar bussiness today, be blessed
Umeongea vema sana comrade
Tz tuongeze bidii ktk kudeal na info maana dunia ipo huko. Tena sisi vijana ndio muhimu sana kuanza na hii mindset
 
Voted, hivi hata serikali si ingekua na means ya ku collect data kujua public opinion kabla ya ku finalise mambo? Si ingekua hivyo kwa kitu ulichoandika au nimekwenda off point?😊😊
Upo right sana senior, nadhani serikali hii kitu huwa inafanya japo sidhani kama huwa ni ktk angles zote inawezekana huwa inalenga zinazohusu mambo flan flan tu ambayo inayahitaji kwa wakati huo. Ila bado ni muhimu serikali kuendelea kuwekeza vyakutosha ktk eneo hili
 
Safi... Tembelea na kwangu.. support ni muhimu Mkuu
 
Umeongea vema sana comrade
Tz tuongeze bidii ktk kudeal na info maana dunia ipo huko. Tena sisi vijana ndio muhimu sana kuanza na hii mindset
kweli kabisa, lakini angalia wale ambao wanastahili kuwa katika mustari wa mbere yaani serikali, kazi ni kubadikia watu makesi fake, this is a must in todays world, bila hii data collection na kuifanyia kazi vizuri tutakuwa tunajaribu maisha, yaani kwa ufupi we will remain in guess work, data ni kaa users manual, na unajua vile users manual ya kitu au chombo chochote ni muhimu, fail to study it at your own risk, tunasubili sahemu ya pili mkuu
 
Taratibu tukiendelea kama vijana na mawazo mapya yenye mwelekeo usiofungwa na itikadi za kisiasa tutafika mahali one day japo safari ndefu na ngumu
 
Back
Top Bottom