Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,898
- 828,493
Kamandi ya Jeshi la Anga ni moja ya Kamandi muhimu zinazounda Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kiutendaji, kivita na kiutawala. Kamandi ya Jeshi la Anga inayo majukumu ya ziada ya msingi katika kutimiza wajibu wake wa ulinzi wa Anga la Tanzania. Kamandi hiyo inao uzoefu wa kusafirisha maafisa na askari wakati wa amani na dharura, pia husaidia mamlaka za kiraia katika kutimiza wajibu wake na kusafirisha mizigo.
Juhudi za awali za kuunda nguvu za Jeshi la Anga ndani ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania zilianza mapema mwaka 1964 pale ambapo kikundi cha maafisa kadhaa walipelekwa nchini Israeli na Ujerumani ya Magharibi wakati huo kusomea urubani.
Hata hivyo, wanafunzi waliokwenda kujifunza urubani katika nchi ya Ujerumani ya Magharibi hawakuweza kumaliza mafunzo ya urubani kutokana na kuvunjika kwa uhusiano wa kibalozi baina ya Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi mwaka 1965.
Baada ya jitihada za muda, hatimae kikosi cha usafirishaji wa anga kilianza operesheni mwaka 1969 kikiwa na ndege mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ndege nne aina ya OTTER na zilizosalia za CARRIBOU. Wakati wote wa chimbuko la nguvu za anga shughuli zote za kioperesheni zilizohusu vikosi na vitengo vya ulinzi wa anga viliongozwa na Tawi la Operesheni na Mafunzo (COT) la Makao Makuu ya Jeshi.
Mwaka 1971 kilianzishwa kikosi maalum cha mizinga ya kutungulia ndege kikiongozwa na Kapteni Abdallah, makao yake yakiwepo Mgulani. Maafisa wa mwanzo walipelekwa Pakistan na India kwa mafunzo ya mizinga hiyo. Mwaka huohuo Rais na Amiri Jeshi Mkuu (mstaafu) Mwl. Julius K. Nyerere aliagiza Jeshi lipatiwe ndegevita.
Mwaka 1973 timu ya marubani wanafunzi 48 wakiongozwa na Meja JE Luhanga(alistaafu akiwa Meja Jenerali) walihitimu mafunzo yao nchini China na wakaanzisha kikosi cha kwanza cha ndegevita
Maendeleo makubwa yalifanyika katika kipindi cha miaka mitano ambapo idadi ya vikosi na zana za Ulinzi wa Anga viliongezeka. Mwaka 1975 vikosi vya Rada vilianzishwa na kugawiwa kanda za uchunguzi wa Anga, kipindi hichohicho vikosi vya makombora matiifu ya kutungulia ndege (SAM) vilianzishwa katika miji mbalimbali.
Utaratibu wa utendaji kivita na mafunzo wa vikosi vyote vya ulinzi wa anga toka 1974 hadi 1982 ulifanywa na Tawi la Makao Makuu ya Jeshi (MMJ) la Chief of Air Defence (CAD) chini ya Kanali SA Hemedi, ambaye baadae alipandishwa cheo kuwa Brigedia Jenerali.
Majukumu ya Kamandi ya Anga.
a. Kutoa ulinzi wa Anga kwa maeneo muhimu ya kitaifa, kisiasa, kiuchumi na kwa Wananchi,
b. Kutoa ulinzi wa Anga kwa maeneo na vituo muhimu vya kijeshi na mkusanyiko wa Majeshi,
c. Kutoa msaada wa kimapigano kwa operesheni za Majeshi ya Nchi Kavu na Wanamaji,
d. Kutoa msaada kwa mamlaka za kiraia hasa nyakati za maafa ya kitaifa na kusindikiza ndege za viongozi pia hukusanya taarifa za kiusalama,
e. Kuendeleza juhudi za mahusiano ya kijeshi na nchi nyingine kwa njia ya mazoezi ya pamoja.
f. Kushiriki katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.
Chanzo: TPDF