black-tz
Senior Member
- Jul 20, 2021
- 115
- 164
IFAHAMU eSIM | LAINI YA KIDIGITALI!
Wengi huenda Mmesikia Mahali au wengine mmeona Neno “eSIM” na hamjaelewa nini Maana yake, Karibuni tuifahamu vyema Huduma ya eSIM na maana yake.
🔎 eSIM NI NINI?
☑️ eSIM ni Laini ya Kidigitali ambayo hupachikwa katika Simu kutoka Kiwandani. Ni laini ambayo haiwezi Kutolewa kama zilivyo laini nyingine zilizozoeleka Nchini Tanzania.
🔎 NINI FAIDA YA eSIM?
☑️ eSIM hurahisisha Kununua Vifurushi katika Mtandao wowote ule haraka zaidi (hata Mtandao wa Nje ya Nchi Uishio).
☑️ Kama ilivyo kwa laini za Kawaida, eSIM inakuwezesha Kutumia Mitandao mingi ya Simu na kuwa na Namba nyingi. Hivyo utaweza Kucontrol shughuli zako kirahisi.
☑️ Laini za eSIM ni Rahisi Kuunganishwa katika Mtandao kuliko Laini za Kawaisa, kwani utascan QR Code pekee ili Kujiunga na Mtandao husika ili Kupata Huduma lakini laini za Kawaida utahitajika Kuziweka katika Simu ndio Ujiunge, na Baadhi huhitaji PIN ili kuziruhusu kufanya kazi.
☑️ eSIM inarahisisha Kutumia Huduma na Kubadilisha Mtandao haraka zaidi kuliko Line za Kawaida. Ili Kupata Laini za Kawaida ni lazima uende Dukani au kwa Mawakala ili Kusajili.
🔎 KITU CHA KUFAHAMU KUHUSU eSIM
☑️ eSIM ni Embedded Hardware (Chip) au Kifaa Ambacho huwekwa katika Simu inapotoka Kiwandani, Hakiwezi tolewa na Hakiwezi Kubadilishwa isipokuwa Unaweza Kubadilisha aina ya Mtandao au Mitandao unayohitaji Kutumia uwapo Nchini au Nje ya Nchi. Simu isiyo support eSIM kamwe haiwezi kuwa na Huduma hii. Mhusika anapaswa Kununua Simu yenye Uwezo huo au Kuendelea Kutumia Laini za Kawaida.
🔎NAMNA YA KUJUA SIMU INA VIGEZO VYA KUTUMIA HUDUMA YA eSIM
☑️ Piga *#06#, Ikiwa Utaona Neno EID na ID zake, basi fahamu Simu yako ina uwezo wa Kutumia Huduma hii, ikiwa hutoona fahamu Simu yako Haina Uwezo wa Huduma hii.
😊Bila Shaka mpaka Hapa nimekupa Mwanga kidogo Kuhusu Huduma hii