Ifahamike karibu nusu ya madini ya uraniamu yaliyorutubishwa yanatoka Urusi

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,976
Sitakosea kama nikimfananisha Marekani na mwanamke aliyeolewa, halafu ni malaya aliyekubuhu, ambapo akiwa katika udangaji wake hujitanabaisha kuwa hana mume ihali ni mke wa mtu.

Sasa unaambiwa Marekani pamoja na kujifanya kiranja wa dunia, tena akiwa mstari wa mbele kumuwekea vikwazo vya kiuchumi Urusi yeye pamoja na washirika wake wa jumuiya ya NATO, na huku akitamani nchi zote duniani ziungane naye kutofanya biashara na Urusi, kumbe kwa Siri yeye anaendelea kununua madini ya uraniamu tena kwa kasi kubwa.

Ifahamike karibu nusu ya madini ya uraniamu yaliyorutubishwa yanatoka Urusi, ambayo bei yake ni cheap zaidi kuliko uraniamu zinazotoka nchi nyingine.

Madini ya uraniamu yanatumika hasa kama chanzo cha nishati ya umeme, pamoja na matumzi mengine mengi.

Mpaka sasa unaambiwa Marekani ndio kwanza amezidisha kununua madini hayo kutoka Urusi.

Takwimu za nusu mwaka 2023 zinaonyesha US keshanunua tani 416 za uraniamu iliyorutubishwa, kiasi zaidi ya mara mbili kwa kipindi cha nusu mwaka wa 2022. Pia kiasi hiki ni cha juu zaidi miaka 18 iliyopita (tangu 2005).Kwa lugha rahisi, Marekani imeshalipa takribani dola milioni 696.5 kwa Mrusi mpaka sasa.

Cc. Mmarekani mweusi wa kibera MK254

Screenshot_2023-09-24-11-04-53-714_com.twitter.android.jpeg
IMG_20230924_104435.jpeg
 
Umeambiwa hapo ananunua kwa bei rahisi halafu unakuja hapa kusifia nini? Hujui ya kwamba kwa Marekani kipaumbele cha kwanza kwao ni Maslahi kwa Amerika? Kwanini wasinunue kama ni bei rahisi?
 
Duniani tuna vituko kwelikweli, ila WaTanzania tunaongoza kwa vituko...hatujui ata maana ya biashara ni nini.
Mtu hawezi kufikiria kwanini China na India wanagombania mipaka lakini wanakaa meza moja kujadili Sera za BRICS.
Au mtoa mada kwako kitu kinachoitwa SERA huwa hukijui? Kuna mikataba iliyokwisha fungwa za IGA na inayo utaratibu ya kuivunja, au wewe IGA yetu na DP WORLD wewe hukuiona kuwa hatutaivunja ata tukiingia vitani?
 
Duniani tuna vituko kwelikweli, ila WaTanzania tunaongoza kwa vituko...hatujui ata maana ya biashara ni nini.
Mtu hawezi kufikiria kwanini China na India wanagombania mipaka lakini wanakaa meza moja kujadili Sera za BRICS.
Au mtoa mada kwako kitu kinachoitwa SERA huwa hukijui? Kuna mikataba iliyokwisha fungwa za IGA na inayo utaratibu ya kuivunja, au wewe IGA yetu na DP WORLD wewe hukuiona kuwa hatutaivunja ata tukiingia vitani?
Hii biashara haimo kwenye orodha ya vikwazo?
Sisi watanzania wenye vituko tunaofanya tafiti tunataka TU kujua.
 
Marekani ana akili zake na mrus anabiashara yake.
Kwa hiyo vikwazo vinachagua?
Maana Nia ya vikwazo ni kuidhioofisha Urusi ili ishindwe kumudu gharama za vita na maisha,
Vita ishindwe
Halafu maisha yawe magumu uchumi uanguke kisha Warusi wampinge akili kubwa Putin.
Sasa ni kinyume chake,biashara hii inaipa Urusi Hela,hivyo inaweza kumudu gharama za vita na uchumi kutulia.
Matokeao yake Ukraine ndio inazidi kuumizwa.
Vikwazo vina faida Gani Sasa?
Sasa hapa nani mwenye akili?
 
Back
Top Bottom