If I had my druthers....

If I had my druthers....

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,079
Reaction score
136,519
In this Information Age, almost everybody is an ‘expert’ in ‘everything’.

So, if I had my druthers, this is what I would do:

Wale wote ambao kwao Rais Magufuli hana jema lolote lile, ningewapa fursa ya wao kuunda serikali nzima ya kuiongoza Tanzania halafu tuone kile ambacho wao wangekifanya kilicho bora zaidi na kilicho tofauti kabisa na afanyacho Rais kwa sasa.

Manake sasa naona na sisi kwenye hii Tanzania yetu tuna watu wanaosumbuliwa na Magufuli Derangement Syndrome.

Chochote afanyacho Rais, kuna watu hawatapenda tu, hata kama na wao ni wanufaika.

Chochote asemacho Rais, watu hawa wenye huu ugonjwa wa Magufuli Derangement Syndrome, watasema ni kibaya tu kwa vile kimesemwa na yeye. Lakini kitu hicho hicho kikisemwa na mwingine, watashangilia kwa kupiga makofi na vigeregere.

Watu hawa natamani sana wao ndo waunde serikali ili hatimaye tuone kama kweli wanaweza kufanya kinyume na vile ufanyavyo huu utawala wa sasa.

Manake isije tu kuwa ni kelele za kupitia kwenye keyboards zisizoambatana na substance yoyote ile kwenye uhalisia.

Anyway, that’s just a hope. And a hope without a plan is nothing more than a wish.....
 
Kwani wakipinga tatizo liko wapi?
Ni serikali gani duniani ambayo ni opposition free?
Kusema za ukweli, mawazo yako ni ya muhimu kuyazingatia. Hizo ni kelele za mpango ambazo hazikatazi mwenye nyumba kuingia
 
Hahaha hakukubalika chamani alipitishwa kwa nguvu, hakushinda uchaguzi akatangazwa kwa nguvu. Haya unayoyaona ni matokeo ya kulazimisha kutawala watu.
Sasa anajitahidi kutafuta legitimacy ndio hapo anapingwa kwa kila kitu. Hata akimleta Yesu bado atapingwa, ingawa wanaweza kumpokea Yesu lakini yeye huyu Magufuli watampinga tu maana watu hawamtaki kwa lolote na chochote.
 
Mzani huelekeza namna ya kuhukumu/amua,sio kwa wingi tu bali pia kwa kuzingatia uzito wa vihusikavyo.Vivyo basi iwapo kama kuna mema lakini yazidiwa na mabaya kwa namna iwayo yote ile au kinyume chake basi hakuna budi kuegemea kunakozidi penzie.

Sintofahamu ni pale wapingao/walalamishi(hata kama hawana maana) wanapo adhibiwa achilia mbali kudhihakiwa maana hata wapongezao juhudi nao wanadhihakiwa.....iweje akosoae/apingaye aadhibiwe??!!!!
 
Sidhani kama kuna mtu anapinga kila kitu anachofanya, yapo mazuri anayofanya mengi sana, ila mabaya anayofanya yanaweza kua ni machache ila makubwa mno.

Wapo wanaopinga kila kitu!
 
Mzani huelekeza namna ya kuhukumu/amua,sio kwa wingi tu bali pia kwa kuzingatia uzito wa vihusikavyo.Vivyo basi iwapo kama kuna mema lakini yazidiwa na mabaya kwa namna iwayo yote ile au kinyume chake basi hakuna budi kuegemea kunakozidi penzie.

Sintofahamu ni pale wapingao/walalamishi(hata kama hawana maana) wanapo adhibiwa achilia mbali kudhihakiwa maana hata wapongezao juhudi nao wanadhihakiwa.....iweje akosoae/apingaye aadhibiwe??!!!!

Kila apingaye ameadhibiwa?
 
Wapingaji wa Magufuli wengi wanasumbuliwa na njaa ukifatilia wengi either maslahi yao yameminywa au wanapata mkate wa kila siku kwa kumpinga JPM.
 
Wewe ndio huelewi...hatutaki Rais afanye chochote...tunamtaka atengeneze mazingira mazuri ya biashara,ajira,etc ili tufanye WENYEWE..peke yake hatoweza
 
Nyani Ngabu you look so smart, lakini cha ajabu kwanini huoni kilicho nyuma ya pazia? Je ni kweli huoni? au huoni kimkakati?

Sisi wakristo tuna maandiko yanasema "shetani huwa anakuja kwa sura ya malaika" anafanya hivi ili kuwahadaa watu wa Mungu, sasa wewe endelea kuhadaika na huyo shetani mwenye sura ya malaika.
 
I’m not smart at all. I’m the dumbest MFer in here.
 
Back
Top Bottom