Idea hii mnaionaje?

Mnyenz

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
1,420
4,306
Huko Duniani hata hapa Tz tumekua tukishuhudia mastaa wengi wakiwa na REALITY TV SHOW, mfano mkubwa kwa mbele ni ile show ya kina KIM KADASHIAN na familia yake.

Huku bongo nadhani ile MAISHA PLUS ilikua ndio the best(big up kwa mwanzilishi)

Sasa baada ya kuanza kushuhudia nyuzi nyingi za kulalamika ukosefu wa ubunifu wa vipindi vizuri katika TV, nikaamua kuleta wazo hili kwenu wadau ili tuone kama linaweza kufaa.

Kuwe na REALITY TV SHOW ambayo badala ya kuwa ya watu au familia maarufu iwe ni ya kutoka katika familia hizi za kwetu za USWAHILINI.

Familia husika iwe na binti MJANJA MJANJA/CHAKARAMU wa mambo ya kiswazi, binti huyu ndio awe muhusika mkuu wa hiyo reality tv show.

Kigezo cha binti ni akubali kuyaishi maisha yake halisi na familia yake kwa ujumla mbele ya camera.(na kusisitiza hilo ni kukubaliana kumlipa baada ya msimu kumalizika na sio kabla ili tuyaone maisha yake halisi/asifeki)

Nadhani kama ikipewa promo ya kutosha itakua show nzuri sana.
 
Una wazo zuri sana. Moja ya makosa makubwa kabisa kwenye fani ya uigizaji au reality kwenye TV za Tanzania ni kufanya mambo yasiyoakisi maisha halisi ya mitaani. Watu wanaigiza uzungu, wanaigiza mambo yanayohitaji uelewa kuliko waigizaji wenyewe walio nao.
 
Naomba mimi niwe mpenzi wa huyo binti chakaramu chakaramu.

The best Medicine of Corona is to Stay Home.
 
Hii content itauza sana kwenye tv hizi maana hawana content za maana siku hizi. Ila angalia wasiibe hii idea tu maana ukishakua na hela idea unazikosa
 
Shida yetu wabongo huyo binti akianza msimu tu akanza kuwa maarufu anabadilika anaanza kufake maisha
ata fake vipi wakati kutakua na mikataba inayombana kuhusu kupata pesa kutokana na umaarufu wake?, yani kama alikua muuza nyanya mkataba utataka aendelee na dili hiyo hiyo
 
Back
Top Bottom