Sikubaliani na Uteuzi wa Idd Simba kwa sababu moja nayo ni kuwa mwanawe Simba wa kike kwa jina Sauda ni mwajiriwa wa kampuni ya Barricks (officer) kwa hiyo kuna utata kidogo pamoja na kwamba nafahamu kuwa ni mjumbe mzuri sana ktk maslahi yetu na hasa ktk swala la Uzawa.
Sikubaliani na Uteuzi wa Idd Simba kwa sababu moja nayo ni kuwa mwanawe Simba wa kike kwa jina Sauda ni mwajiriwa wa kampuni ya Barricks (officer) kwa hiyo kuna utata kidogo pamoja na kwamba nafahamu kuwa ni mjumbe mzuri sana ktk maslahi yetu na hasa ktk swala la Uzawa.
Kithuku na Kada,
Niliyotoa ni mawazo yangu binafsi na sababu kubwa nayoweza kuisema ni kutokana na experience yangu ktk maswala kama haya hasa kwetu sisi Wadanganyika inapoingia swala la mahusiano kati ya mwanao na mwajiri wake. Hata uchaguzi wa Jury ktk mahakama zetu huangalia vitu kama hivi kwani sii lazima awe na hisa ila hata ajira ndio inayoendesha maisha ya mwanae - Yote yanahusiana na fedha.
Binafsi namuamini Simba kama nilivyowahi kuwaamini viongozi wengine lakini pamoja na yote haya nimejifunza kitu kimoja kuwa family interest comes first before anything!
Dr. Slaa amezungumza mengi yenye maana zaidi kuhusiana na kamati hii kama utasoma hotuba yake kwa makini na katoa solution nzuri sana kuwa kamati ichaguliwe toka bungeni kuepuka yale yaliyokwisha tokea huko nyuma. Nitarudia kusema ni mawazo yangu binafsi na sii lazima yawe na ukweli ama yafuatwe..
Bi. Sauda kafanya kazi ITV na hiyo kampuni ya bia lakini sidhani kama maswala ya kampuni hizi yapo mezani leo hii wala hazihusiani kabisa na mashaka yangu.
huyu slaa sasa anajifungafunga kamba mwenyewe na alivyokuwa jeuri hataki hata kuomba msaada wa kufunguliwa hiyo kamba maana anajizunguka tu mwenyewe na kivuli chake. leo anasema hivi kesho vile keshokutwa vileee yaani tabu kweli !
mwaka huu mambo yamewakwama kooni nje hayatoki ndani hayaendi.
na tumewashtukizia muongo muongoze. na tuna msemo mchawi mpe mwana kulea.
sasa tunawaangalia watasemaje