Idd Simba, Salum Mwakinginda wafikishwa mahakamani

Ni lini report ya kamati teule itasomwa bungeni ili watanzania na hasa watu wa DSM wajue ukweli kuhusu UDA?
 
NIMEIKUMBUKA HII YA MANYERERE JACKTON

Dar es Salaam na ukame wa wazee!

Na Manyerere Jackton

Ukiwasikia watu wanaovyokikosoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) au Serikali inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, unaweza kudhani kwamba wakipewa nafasi wanaweza kufanya mambo ya maana tofauti na hao walioshika madaraka sasa.

Ukiwasikia baadhi ya wazee unaweza kuamini kuwa hawa wakirejeshwa kuliongoza taifa hili, wanaweza kurekebisha makosa waliyofanya wakati wakiwa madarakani, au wanaweza kurekebisha kabisa hizi kasoro tunazoziona sasa.
Mara kadhaa wazee kwa vijana wamesikika wakitoa ushauri wa namna ya kuijenga CCM au kuifanya Serikali itekeleze wajibu wake barabara. Kwa ufupi ni kwamba katika taifa letu sasa kila mmoja ni mtaalamu wa “nasaha”. Lakini juu ya yote, bado tumeamini kuwa Tanzania itajengwa na “wao”, na si kwamba itajengwa na “mimi”. Tuna maneno na nadharia nyingi za kufikirika.
Tujitazame wenyewe. Hatukosi kulalamika kwamba miji yetu ni michafu. Hatukosi kulalamika kuwa ajali za barabarani zimekuwa nyingi. Hatukosi kulalamika kuwa vijana wa vijiweni na vibaka wanaongezeka. Lakini hatujiulizi ni nani ataifanya miji yetu iwe misafi, nani mwenye wajibu wa kupunguza ajali barabarani, au ni nani mwenye dhima ya kuhakikisha vijiwe vinapungua na vibaka wanakoma. Hakuna. Mara zote tumeamini kuwa kila jambo jema au jambo kubwa la maana ni lazima, ama lifanywe na kiongozi, au serikali iliyo madarakani. Tunakosea.
Haya mambo yananifanya niende moja kwa moja kwenya mada yangu ya leo. Iddi Simba ni mtu ambaye unaweza kusema kwa kimombo kuwa ni “controversial”.
Simba anakabiliwa na kashfa kadhaa, kubwa ikiwa ile ya vibali vya sukari iliyomlazimu auachie uwaziri wa viwanda na biashara. Alijiuzulu. Mbunge wa Kwela kwa wakati huo, Dk. Chrisant Mzindakaya, alifanya kazi yake.
Simba huyu huyu akaibuka na “sera ya uzawa”. Wapo waliompinga kwa namna alivyoiwasilisha, lakini wapo waliomuunga mkono. Inawezekana dhamira ilikuwa njema, lakini namna ya kuiweka ndiyo ilikuwa mbaya. Alitaka tuamini kuwa Mtanzania mzawa ni mtu mweusi mithili yetu kina Manyerere. Kuwa mweusi, pua pana na mengine ya aina hiyo, yalionekana kuwa ndivyo vigezo vya mtu kuwa mzawa. Nadhani tafsiri ya mzawa kwa maana hiyo haikuwa sahihi. Inawezekana ni yeye, au waliodakia mjadala huo ndiyo waliopotosha jambo hilo. Uzawa kwa wenzetu ni uzalendo unaoonyeshwa na mwana wa nchi husika-bila kujali rangi au asili.
Tunao watu wasio weusi katika taifa letu, lakini ni wazawa wa kuzaliwa na wa kimatendo kuliko weusi wengi waliozaliwa au kuhamia hapa. Kwa mfano, mtu kama Mustafa Sabodo ambaye si mweusi, amethibitisha uzawa wake kwa kutoa misaada mingi katika jamii. Ameshachimba visima virefu zaidi ya 400 nchini kote. Ametumia mabilioni ya shilingi. Huyu anaweza asiwe na tofauti sana na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye ametumia mabilioni ya fedha zake kuwapa maendeleo wananchi katika jimbo na taifa lake. Ingawa hawa wawili ni tofauti kwa rangi, ni wazawa wa kweli. Tunao weusi wengi wasiotaka kuwasaidia Watanzania wenzao. Hao hatuwezi kulazimishwa kuamini kuwa ni wazawa kwa maana ile ya tafsiri ya Iddi Simba. Tuna wazawa weusi ambao ni mawakala wa majizi yanayopora rasilimalin za nchi yetu. Wapo serikalini, katika benki na kila mahali.
Pengine Simba kwake uzawa ilikuwa rangi, maana kama ni kuzaliwa, kuna minong’ono kwamba naye alizaliwa huko kwa majirani zetu. Hilo si la maana sana hasa kwetu tunaoamini kuwa, “Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja”.
Utata wa Simba umeendelea kuwapo katika mambo kadha wa kadha. Jipya kabisa ni sakata la yeye akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya UDA kuamua kuwekewa Sh zaidi ya milioni 250 kwenye akaunti yake. Fikiria, fedha binafsi za shirika la umma, Mwenyekiti anaamuru ziwekwe kwenye akaunti yake. Fedha zote hizo zimeshatafunwa. Kwa kuwa uchunguzi wa suala hilo unaendelea, pengine tuishie hapa kwa sasa.
Simba huyu huyu anayekabiliwa na kashfa mbalimbali, yeye ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam! Nilidhani kuwa baada ya kashfa hii ya UDA, ukijumulisha na zilizopita, wazee wangeibuka na kuonyesha mfano wa uwajibishaji!
Hapo juu nimesema kwamba nchi hii sasa kila mmoja ni mtaalamu wa “nasaha”. Ukiwatafakari hawa wazee wa Dar es Salaam, unabaini kuwa nao wameishia kwenye nasaha tu za kufikirika, wakiamini kuwa yupo malaika atakayekuja kumaliza kero zinazolikabili taifa letu.
Siku ile Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akiwahutubia wazee hao katika Ukumbi wa Karimjee, Simba alikuwa pembeni akijaribu kujitutumua kuonyesha kuwa ni Mwenyekiti wa ukweli wa wazee wa Dar es Salaam. Nikajiuliza swali, “Hivi Dar es Salaam imekosa wazee hadi waone anayestahili kuendelea kushika nafasi hiyo ni Iddi Simba?”
Nilijiuliza swali hilo si kwa sababu namchukia Simba, bali kwa kuwa huyu mzee tayari ana kashfa zinazomtosha. Kashfa alizonazo hazistahili kabisa yeye kuendelea kuwa kiongozi wa wazee tunaoamini kuwa wana busara na maono ya kulipeleka mbele taifa letu. Kijana gani anaweza kumsikiliza na kumheshimu mzee anayetuhumiwa kwa utapeli? Hakuna. Kama yupo, basi naye lazima awe na vimelea vya tabia hiyo.
Kitu gani alichokuwa akizungumza Rais Kikwete siku hiyo? Rais wetu alikuwa akizungumzia madai ya madaktari. Miongoni mwa madai hayo ni mishahara, marupurupu duni, vitendea kazi na mazingira magumu ya kazi zao. Kwa kifupi ni kwamba madai mengi yalijikita kwenye fedha. Rais akatoa maelezo marefu mno ya namna fedha zisivyotosheleza. Yapo tuliyoweza kukubaliana naye, lakini mengine yalikuwa ya kupamba tu. Kwa mfano, matumizi ya fedha za umma ni makubwa sana. Hakusema atapunguza nini kwenye matumizi ya Serikali.
Vyanzo vya fedha ni baadhi ya mashirika ya umma kama UDA. Sasa kama Mwenyekiti wa Wazee pekee amelamba Sh milioni zaidi ya 250 na anamsikia Rais wa nchi anavyolia kwa ukata unaofanya ashindwe kuwalipa vema madaktari, nani mwenye akili anaweza kumsamehe mzee huyu? Rais alijisikiaje kuwa meza moja na mzee anayetuhumiwa kulamba mamilioni ya fedha anazosaka kuwalipa madaktari?
Shilingi milioni 250 zinawalipa madaktari wangapi na kwa miezi mingapi? Matarajio yangu siku hiyo yalikuwa kumwona mzee mmoja shujaa akisimama na kumtaka mzee mwenzao aachie madaraka kwa sababu anatuhumiwa kulamba fedha ambazo pengine zingewasaidia hao vijana madaktari ili mgomo ukome.
Hata kama fedha anazodaiwa Simba kuzitafuta haziwezi kubadili hali ya madaktari nchini, nadhani kauli ya kumtaka ajiuzulu ingekuwa na thamani kubwa zaidi kwa sababu wazee wangeonyesha kuwa wamedhamiria kupambana na mafisadi wanaosababisha vilio kwa madaktari, walimu na kada nyingi nchini. Lakini wazee wale wakawa kama wamepigwa ganzi. Wakawa Wamethibitisha kuwa wanamwogopa mwenyekiti wao. Hakuna aliyethubutu kusimama na kusema, “Mzee mwenzetu rejesha fedha za UDA ili zipoze makali ya mgomo wa madaktari”.
Ndiyo maana nasema uwajibikaji katika nchi hii ni zigo la kufikirika. Kila mtu anadhani kuwa wakombozi wa taifa letu ni watu wengine kabisa tofauti na sisi wenyewe. Wazee wanafikiri wakombozi ni vijana. Vijana nao wanadhani wakombozi ni wazee. Tunakosea. Sote tuna dhima hiyo.
Kama wazee wanashindwa kumhoji au hata kumng’oa mzee mwezao anayekabiliwa na kashfa ya kutafuna mamilioni ya fedha za umma, watakuwa na ushujaa gani wa kuwakemea au kuwaadhibu watuhumiwa wa ufisadi ndani ya vyama vya siasa na serikalini?
Kama wazee wanageuka mabubu kwa mwenzao anayetuhumiwa kula fedha za umma, vijana watatoa wapi ushujaa wa kupambana na wazee au vijana wenzao walioifilisi nchi?
Nilichojifunza kutoka kwa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam ni kwamba ili katika taifa hili mtu uweze kupata heshima, ni lazima uwe na kashfa nyingi, zikiwamo za ukwapuaji fedha za umma! Kama hivyo sivyo, bila shaka leo ingekuwa ni aibu kubwa kuwaona watu aina ya Iddi Simba wakiwa wameketi na Rais katika meza kuu ilhali wakiwa wamezingirwa na kashfa mbaya ya upokaji fedha za umma.
Mwisho niulize swali, “Hivi ni kweli kwamba miongoni mwa wazee woooote wa Mkoa wa Dar es Salaam hakuna anayeweza kuwa mwenyekiti wao wa muda kupisha uchunguzi dhidi ya Iddi Simba? Bila shaka wapo wengi wanaofaa wasiokuwa na kashfa za wazi kama za huyu mzee mwenzao. Wazee wasipokemeana, watakuwa wakijenga taswira na kuwapa vijana urithi mbaya; urithi wa kuwavumilia wala fedha za umma.

..tamati….

…tamati….
 
Gharama ya kesi ni milioni 800 ambazo kisheria anatakiwa alipwe Idd Simba, na Serikali imetakiwa kumuomba radhi.

Wakati mwingine huwa mna mawazo mazuri sana....unajua Ritz huwa nawashangaa ninyi mnaoitetea CCM na serekali yake. Nadhani ni kazi ngumu kuliko kubebe gunia la misumari...Hivi huwa mnawatetea hawa jamaa kiukweli kabisa kwa dhati yenu au na ninyi mnauona usanii wao na unawauma kama siye wengine??
 
Tz nchi ya ajabu sana, naamini siku akitokea mwenye akili timama tu na akaamuru sheria za Chini ziwepo tz,tutanyonga mpaka maiti zilizozikwa tu!
 
Aliyekuwa diwani wa sinza salum mwakinginda pamoja na aliyekuwa mbunge wa ilala idd simba wamefikishwa mahakama ya kisutu hivi sasa kwa makosa ya ufisadi wa uda.

picha? ameka kwenye benchi au kasimama kizimbani?
 
Gharama ya kesi ni milioni 800 ambazo kisheria anatakiwa alipwe Idd Simba, na Serikali imetakiwa kumuomba radhi.
Bro naona umekomaa kifikra,bado nashindwa kuunganisha unachoandika hapa jamvini na unachokiamini kwenye mfumo wa magamba,anyway nakuombea uwe delivered na virus wa magamba teh!
 
...Na Mkapa atapandishwa lini Kizimbani kuhusiana na wizi wa Kiwira, ununuzi wa rada, ndege ya Rais, ukwapuaji wa nyumba za serikali na ufisadi mwingine.
 
Wazazi --- Puu:lock1:, Uwaziri --- Puu:lock1:, Board chair -- Puu:lock1:

What a failure and still expected to lead Dar elders?:yell:
 
Tz nchi ya ajabu sana, naamini siku akitokea mwenye akili timama tu na akaamuru sheria za Chini ziwepo tz,tutanyonga mpaka maiti zilizozikwa tu!
Kwa Tanzania, kisichowezekana ndio kinawezekana na kinachowezekana hakiwezekani (angalau kwa sasa ndivyo ilivyo).
 
Gharama ya kesi ni milioni 800 ambazo kisheria anatakiwa alipwe Idd Simba, na Serikali imetakiwa kumuomba radhi.
Wakati huo serikali ya magamba haitakuwepo, na bahati mbaya zaidi dingi huyo atakuwa amezeeka ile mbaya!
 
Binafsi naona hii ni hatua nzuri kuelekea haki kupatikana!
Ila shida kubwa ni mahakama zetu kuwa kangaroo;sijui kama haki itapatikana!!!!
 
Huyu miezi michache iliyopita alijifanya mwenyekiti wa wazee wa Dar es Salaam na kumkaribisha JK Ukumbi wa PTA wakati alipowananga madaktari waliogoma. Ajabu JK alikubali kukaribishwa na jamaa huyu huku akijuwa fika anabeba tuhuma nzito za ufisadi wa UDA.

CCM na uongozi wote wa juu is really f***** up!!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom