idd ninga:NAHISI NIPO PEPONI(shairi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,207
4,405
>>Nahisi nipo peponi,nikiona sura yako.
Penzi lako la thamani,hakuna mfano wako.
Napata hamu moyoni,kushika kiganja chako.
Kilichokuwa laini,nalainika mwenzako.
Nikuonapo usoni,ni nyororo ngozi yako.
Sikuachi asilani,milele mimi ni wako.
Wewe ni wangu mwandani,nifanye chaguo lako.
Nitie ndani moyoni,nisije kufa mwenzako.
Kwani kwangu u moyoni,kukuacha mimi mwiko.
Sebuleni na chumbani,kwangu uje kuwa jiko.
Ni shuka langu la ndani,kwako sina hangaiko.
Nitatulia kitini,nije pata pumziko.
Nisemeze sikioni,linitoke sikitiko.
Mrembo hadi gizani,hata hujapakwa piko.
Ungelikuwa angani,malaika peke yako.
Utamu wako mezani,nilizuri pishi lako.
Oho malaika wangu,ipooze roho yangu.
Kwako sipati uchungu,upo kwenye moyo wangu.
Nishike mkono wangu,utazame mboni yangu.
Utajiona mwenzangu,wewe ulo chungu changu.
Ivisha chakula changu,kitamu kiso kichungu.
Zawadi toka kwa mungu,ilofika hapa kwangu.
Naapa haki ya mungu,paka kifo wewe wangu.
Niseme nini mwenzako,nahisi nipo peponi.
Mazuri mahaba yako,yasiyouzwa sokoni.
Mazuri mahaba yako, hayapo hata dukani.
Shairi:NAHISI NIPO PEPONI.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0655519736.
 
Back
Top Bottom