Idara ya Uhamiaji isisahau watanzania tunaongoza kwa kutoa wahamiaji haramu

lusaka city

Senior Member
Mar 17, 2015
146
116
Watanzania tumekuwa na midomo kuwasema wakenya na wageni wengine kuwa hawatakiwi nchini mwetu tusisahau pia watanzania tunaongoza kwa idadi kubwa kuvamia nchi za watu.

Mfano mzuri soko la Comesa nchini Zambia asilimia 90% ya watu wanaofanya biashara pale ni watanzania na kwa asilimia zaidi ya 70 hawana work permit ukiacha apo nenda mitaani wako wakumwaga.

Nenda Malawi Lilongwe na Blantyre, nenda Zimbabwe Afrika Kusini usiseme Johanesberg ni shida, tusisahahau tunandugu wanaoishi nje ya nchi ni wengi sana idara ya uhamiaji kamata kamata yenu isije kuwaponza watanzania hawa.
 
Wanasema two wrongs don't make it right. Hivyo lazima ifike wakati sheria ifuatwe.
 
Hoja yako haina mashiko kwahiyo unataka kutuambia tusifuate sheria za nchi kwasababu kuna watanzania ambao hawafuati sheria ?.
 
Watanzania tumekuwa na midomo kuwasema wakenya na wageni wengine kuwa hawatakiwi nchini mwetu tusisahau pia watanzania tunaongoza kwa idadi kubwa kuvamia nchi za watu.

Mfano mzuri soko la Comesa nchini Zambia asilimia 90% ya watu wanaofanya biashara pale ni watanzania na kwa asilimia zaidi ya 70 hawana work permit ukiacha apo nenda mitaani wako wakumwaga.

Nenda Malawi Lilongwe na Blantyre, nenda Zimbabwe Afrika Kusini usiseme Johanesberg ni shida, tusisahahau tunandugu wanaoishi nje ya nchi ni wengi sana idara ya uhamiaji kamata kamata yenu isije kuwaponza watanzania hawa.
Aisee umepotoka mbaya hizo nchi unazozisema kwanza ni noma kuliko hata Tanzania ambako unaweza kukaribishwa na kusaidiwa na wenyeji lakini sio huko ulikotaja hasa Malawi Kenya Uganda na South Africa, nimetaja hizo kwakuwa nilishawahi kuishi na kufanya kazi huko
Between hatuwezi kuiacha nchi isisimamie sheria zake kisa eti kuna raia wake wengi wanakikuka taratibu na nchi nyingine huko waliko
 
Vyovyote saw a ila unapaswa kuishi kwenye mchi yatu kwa kufuata taratibu zao
 
Tunachotakiwa kufanya turahisishe taratibu ya vibali kwa wageni hasa kwa nchi zenye mahusiano mema nasi, na uhamiaji waondoe upokeaji wa Rushwa ndilo tatizo kubwa.
 
Mzee lusaka city umenena na husiende mbali.Nenda Congo ndo utajua wapo watanzania tena watu wanatafuta maisha ni balaa.
 
Hiki kimbunga cha uhamiaji kitawavuruga sana wahamiaji haramu siyo Tanzania tu bali ni ukanda wote wa Afrika mashariki na kati.
 
Mombasa,Nairobi,kisumu na hata ktk miji midogo wamejaa wa Tz.Ukizunguka mtu,ndipo unaelewa.
 
Back
Top Bottom