DOKEZO Idara ya Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kuna uonevu wa kutolipa watoa huduma fedha za on-call miezi minane sasa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na changamoto kwa watumishi wa idara ya afya Korogwe kulipwa fedha za on-call allowances; huu ni mwezi wa nane tangu February wakiuliza wanagombezwa na viongozi (ofisi ya mganga mkuu wilaya ya Korogwe) hasa watumishi kituo cha afya Mombo.

Pili, kumekuwa na changamoto ya kuwalipisha malipo wajawazito wakati wa kufanya vipimo kwenye Kliniki za ujauzito na wakati wa upasuaji wa uzazi kama mama atatakiwa kujifungua kwa upasuaji anaambiwa alipie vifaa zaidi ya elfu 60 na kuendelea; wakiuliza wanaambiwa ni utaratibu wa Wilaya wakati ni kinyume na maagizo ya Serikali kwenye kituo cha afya Mombo.

Tatu, mganga mfawidhi katika kituo hicho ni mkorofi, hana ushirikiano na watumishi wenzake hasa kwenye kutatua changamoto za mahitaji ya watumishi hao kufanyia kazi jambo linaloshusha ari ya kufanya kazi kwa kuwa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu ya kutolipwa madai yao ya muda wa ziada.

Nne, labor ward vitoto vichanga vinakufa Vingi kwa sababu ya huduma mbovu ya uzazi; hakuna vifaa vya kuzalishia, utakasaji wa vifaa haufuatwi kiasi cha sisi tunaopata huduma tunaogopa kuambukizwa magonjwa wakati wa kujifungua kwenye kituo hicho.

Labor ward na theatre kuna rushwa tunaombwa fedha wakati wa kupata huduma , mimi mwenyewe wakati wa upasuaji wa kujifungua nilitoa fedha kama elfu 65 nikaambiwa na madaktari wa theatre ni za vifaa vya dharura.

Mdogo wangu mwenyewe huko labor ward pamoja na mtoto kufariki kwa sababu ya uzembe wao wa kutokuwa na vifaa salama bado tuliombwa fedha 20000 ya kujifungua eti masona.
  • Hospitali vitanda na magodoro vina kunguni na wana magodoro mapya hawabadilishi.
  • Nyakati za usiku duka la dawa wanafunga na hivyo huduma ya dawa tunalazimika kwenda kununua nje ya hospitali na ni mbali. Hii imekuwa changamoto ya siku nyingi tumeulizia kwenye mikutano ya kijamii mganga mfawidhi anatujibu wanashughulikia lakini tunasikia ametumia fedha nyingi kukarabati duka la nje kwa ubadhirifu kwa hiyo lipo ni chumba tu. Sisi tunapata shida usiku tukija kupata huduma.
Tunaomba mtusaidie kupaza sauti.
 
We mgonjwa au muuguzi mbona unasema kuna kunguni tena kwenye vitanda.
 
Ccm ni walaghai sana.

Hawana uwezo wa kutoa huduma Bure ya afya ikawa na ubora wowote.

Sana sana ni kuwagombanisha watoa huduma na wapokea huduma ambao ni wananchi.

Aga Khan kuna huduma nzuri ulishawahi kuwa ni huduma ya bure?

Muhimbili ni ya serikali na inatoa huduma bora je ulishawahi kusikia ni Bure?
 
Hospitali vitanda na magodoro vina kunguni na wana magodoro mapya hawabadilishi.
Ndio stahili yenu.

Bila watanzania wotw kuungana tukawaondosha hawa watawala dhalim hakuna mabadiliko yoyote.

Wao hawatiwi kwenye viwango hivyo.
 
Kwa sababu ya mazingira yasiyo bora ya kujifungulia labor ward kuna Vifo vingi vya watoto wachanga kitu kinachofanya mpaka sisi tunaopata huduma kuogopa ...nakumbuka mdogo wangu alipoteza mtoto nikiwa naona baada ya kuzaliwa mtoto alitolewa uchafu mdomoni na kifaa kimetolewa kwenye ndoo ya maji machafu ya kusafishia vifaa.
Kama huko anakotoka Waziri wa Afya hali ni hiyo, vipi huko kwingine
 
Wale wanaosimamia stand ya kilole Kwanini wanakataza watu wasichome mahindi Na kuuzia wananchi?

Waelekezeni wao home kwa usafi wasimwage jivu chini lakini sio kuwapiga marifuku.

Hivi Kwani mnakuwaga na ulimbukeni wa nini?

 
Bure ina gharama, ukitaka huduma bora lipia, serikali ya CCM ni ya waongo nawahuni huduma za afya zimezorota rushwa imetamalaki. Kwasababu watumishi wa afya hawajaliwi.
 
Kwenye kufanya cs sidhani kama umeongozwa na uhalisia zaidi ya hisia.

Hakuna pahala cs ikafanywa bure. Mind you; vipimo alivyo-request daktari ndio bure, mfano mama kaja anataka kufanya USS unampimaje bure?

Embu fuatilia kwa i/c wako kujua hizo on-call allowances yeye ni member wa HMT kituoni kwako.

Kuhusu vifo vya watoto wachanga. Huwa mna morning reports siku 5 kila wiki plus maternal/perinatal discussions kila inapotokea hizo changamoto. Je, mnashiriki na mnakuja na maazimio na mnayatekeleza?

Pole sana
 
Wale wanaosimamia stand ya kilole Kwanini wanakataza watu wasichome mahindi Na kuuzia wananchi?

Waelekezeni wao home kwa usafi wasimwage jivu chini lakini sio kuwapiga marifuku.

Hivi Kwani mnakuwaga na ulimbukeni wa nini?

Hili swala sio korogwe dc tu hata koogwe tc lifuatiliwe
 
Acheni uchochezi..huo nchi inautaratibu na kila leo tunaambiwa kama umeonewa nenda takukuru na hata viongozi wa ccm wapo mbona hamupeleki hayo malalamiko..haya sasa humu mtandaoni utasaidiwa nn..ndoa maana nasema huu ni uwongo na uchochezi na nyingi ninao publish hizi taarifa bila ushahidi hamuko alama sana..ukionewa na kiongozi yeyote toa taarifa haraka.
Bila shaka mumeona mara kadha viongozi wakichukua hatua kali kwa watumishi wazembe..sasa na hilo vp
 
Back
Top Bottom