Idadi ya watoa vikombe ninaowafahamu mimi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idadi ya watoa vikombe ninaowafahamu mimi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kituro, Apr 7, 2011.

 1. k

  kituro Senior Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  watoa vikombe ambao mimi nawafahamu mpaka sasa ni hawa
  1. pastor wa loliondo (muasisi wa tiba ya kikombe )
  2. kijana wa tarakea rombo kilimanjaro (wa pili)
  3. kijana wa mianzini mabatini mbeya
  4. bibi wa tabora
  5. pastor wa katumba rungwe mbeya
  6. mtowa kikombe wa ruvu (sifa yake anatoa dawa kwa wagonjwa bure)
  7. mtoa kikombe wa kichangani morogoro ( sifa anatoa dawa kwa sh.200)
  8. mtoa dawa wa ruvuma


  natarajia mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu kila kijiji kitakuwa na mtoa kikombe wake.
  ndugu zangu huko tuendako ni kubaya sana! nibora tukajisalimisha kwa yesu ili tuweze kuwa salama!.
   
 2. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Dr Mwandulami pia kule Njombe anatoa, nasikia ni sh 2000.
   
 3. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu wabongo tulivyo vijiwe hata na wewe ukitoa kikombe chako utakula vichwa kama kawa teheteheteheeee!!!lol
   
 4. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ugua Kwanza then utatoa maamuzi ya busara sawa.
   
 5. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Umeongea kama masihara. Lakini nina taarifa za kiintelijensia. Jamaa yangu anayefanya shughuli zake Kariakoo ameshuhudia njemba moja ikiwa na kapu kubwa. Ndani ya kapu hilo kulikuwa na chupa nyingi za maji ya uhai zilizojazwa dawa fulani. Alikuwa anatembeza kikombe akidai kinatibu magonjwa mbalimbali sugu. Amini usiamini watu walimzingira na kunywa dawa yote kwa bei ya shilingi 2000 kwa kikombe. Wengi sana walitaka dawa hiyo lakini walikosa. Hawa ndio watanzania wa leo. Wamechoka kufikiri. Inasikitisha sana.
  Nilipouliza waliokunywa walifahamu vipi kama ni dawa kweli jibu nililopata lilikuwa utata mtupu. Eti mtu alipokunywa alihisi koo linawaka moto na hivyo kuamini kuwa ni dawa ya kweli.

  Mungu atunusuru na pepo hili.
   
 6. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Shangazi wa Mwanza
  Bagamoyo
  Mchungaji wa KKKT huko Sanya Juu (Leo - naye anatumia mti wa babu)
   
 7. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ugua Kwanza then utatoa maamuzi ya busara sawa.
   
 8. b

  binti ashura Senior Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  KKKT kuna mchungaji tena, mie nilifikili ni yule babu tu sasa bado askofu wa KKKT utasikia askofu mmoja kaanza nae kutua, haya sie yetu masikio!
   
 9. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza kuna watu wawili wanatoa vikombe mmoja yuko Tarafa ya Ng'wamashimba Kijiji KIKUBIJI huyu ni bibi na mwingine Tarafa ya Nyamilama kijiji NG'WAKILYAMBITI huyu ni mkaka tu. Sijui wa Tanzania tunaelekea wapi the list keeps increasing!
   
 10. LivingBody

  LivingBody Senior Member

  #10
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kaazi kwelikweli,,, baada ya mwaka itakuwaje?
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  tatizo ni idadi yao au tiba wanayotoa? Sijakuelewa mkuu
   
 12. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Mchungaji huyu anaitwa Japhet Laizer. Anadai alikuwa na mpango wa kuanzisha tiba hii tangu siku nyingi zilizopita kwani alishaandika kitabu juu ya uwezo wa mti wa mgariga. Ameshaanza kuwanywesha wakazi wa arusha dawa hiyo tangu juzi. Huyu bwana anasema ameshaufanyia research mti huo, na kwamba kiutaalam mti wa mgariga una uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali sugu. Alipoulizwa kama ameoteshwa au la, alidai kuwa mti huo alirithishwa na babu yake ambaye alikuwa anaelewa miti mbalimbali ya tiba. Alisema dawa yake haina masharti yoyote, ni mtu kunywa kikombe na kuondoka. Bei ya kikombe 1000/=. Inaonekana kwamba amelazimika kujitangaza sasa baada ya babu kumpri-empty. Ni sawa na Mwandulami aliyedai kuwa alikuwa akitumia mti huohuo kwa kuchanganya na dawa nyingine kutibu magonjwa mbalimbali na sasa amegundua kuwa ukiutumia wenyewe bila kuchanganya na dawa nyingine unakuwa na nguvu zaidi kutibu magonjwa sugu.

  Alimaliza kwa kusema kama babu alioteshwa mti huu, basi alioteshwa mti ambao tayari yeye alikuwa anaujua.
  Suala hili linaanza kuleta mwanga kuhusu kile kipengele cha imani. Kwamba kinachotibu si dawa bali ni neno lililomo kwenye mzizi. Na kwamba dawa haihamishiki. Huu ni ubinafsi wa babu kutaka kumiliki soko. Pia kipengele cha kupona kwa imani ndicho kilichowafunga wengi na kumwacha babu akiwacheka kwani usipopona huna imani! Mpaka sasa mti wa mgariga unatumiwa kutibu na watu watatu ingawa babu alisema hauhamishiki; babu, Mwandulami na Laizer. Mwenye masikio na asikie.


  Acts 4:12 "Neither is there salvation in any other: for there is none other name under heaven given among men, whereby we must be saved."
   
Loading...