Mwanafunzi aacha shule kutoa dozi ya ‘kikombe’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi aacha shule kutoa dozi ya ‘kikombe’

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MAFILILI, May 15, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  WIMBI la tiba ya kienyeji maarufu kama ‘Kikombe’ linaendelea kugubika nchi na safari hii mwanafunzi wa kidato cha tano wa sekondari ya Buluba, wilayani hapa, amelazimika kuacha shule na kujikita katika kutibu kwa ‘Kikombe.’

  Akiwa na umri wa miaka 24, Sanagu Onesmo, ambaye ni miongoni mwa vijana wenye umri mdogo kati ya matabibu wa vikombe walioanza kuibuka Tanzania mwaka huu, anatoa huduma yake hiyo katika kijiji cha Mwambegwa kata ya Mwanuhuzi.

  Vijana wengine waliowahi kuibuka na vikombe ni pamoja na binti mwenye umri wa miaka 19 aliyekatisha masomo kidato cha tatu Singida na mwingine wa Mbeya.

  Onesmo ni mtoto wa Onesmo Mwigulu, Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Mwambegwa ambaye anadai kushangazwa na mwanawe kuanza kutoa dawa hiyo ya ‘miujiza’ kwani katika ukoo wao hakuna historia ya waganga wa kienyeji.

  “Onesmo alilazimika kuacha masomo akiwa kidato cha tano Buluba, baada ya walimu wake kugundua kuwa alikuwa akitumia muda mwingi darasani kulala, tena usingizi mzito,” alisema Mwigulu.

  “Ilibidi niache shule maana kila nilipokuwa darasani, nilijikuwa nimepitiwa na usingizi na ni katika hatua hiyo ndipo ghafla nilioteshwa dawa za mitishamba,” alisema Onesmo akiongeza kuwa katika ndoto hizo, aliletewa picha za miti na mimea ambayo hakuifahamu mara moja isipokuwa mmoja uliofanana na miti iliyokuwa katika eneo la nyumba ya marehemu babu yake.

  “Huu mti unaitwa ‘nditima’ kwa Kisukuma na ni kweli babu alikuwa ameipanda kwa wingi kwenye nyumba yetu ya zamani na nilishangaa, maana yeye hakuwahi hata siku moja kuitumia kwa dawa,” alisema Mwigulu.

  Hivi sasa Onesmo hupata wateja kati ya 100 na 200 kwa siku na anadai dawa yake, kama ile ya ‘Babu wa Loliondo’ –Ambilikile Mwasapile - pia inatibu Ukimwi na magonjwa mengine sugu, lakini kijana huyo ‘alitoa mpya’ alipodai kuwa tiba yake pia ina uwezo wa kurefusha maisha.

  Dawa hiyo mpya inatolewa kwa Sh 2,000 na mgonjwa ni lazima anywe vikombe viwili ikiwa ni kwa Sh 1000 kwa kikombe.

  Onesmo anasema kila kikombe kina dawa iliyotokana na miti tofauti.

  Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Abihudi Saideya, alikiri kuwa uongozi wa wilaya umeshatoa kibali kwa Onesmo, aendelee kutoa tiba yake baada ya kuridhishwa kuwa mazingira ya eneo lake ni safi na dawa haina madhara ila kuhusu suala la uwezo wake wa kutibu, bado linafanyiwa kazi.

  “Nimemtuma Ofisa wa Afya wa Wilaya kuichunguza kwa makini dawa hiyo ya Meatu,” alisema Saideya.

  Tayari mwanamke (jina limehifadhiwa) ambaye ni mfanya biashara wa hapa, na anayedaiwa kuwa na Ukimwi, ametangaza kujisikia vizuri baada ya kupata ‘kikombe’ cha Onesmo.

  Wimbi la vikombe limeshika kasi karibu katika kila pembe ya nchini, tangu kuibuka kwa Mchungaji Mwasapila wa kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro ambaye pamoja na wengi kujitokeza `kuiiga’ tiba yake, bado umaarufu wake uko juu na ameendelea kupokea umati mkubwa wa wagonjwa, wakiwamo viongozi, watu mashuhuri wa kada za siasa na utumishi wa umma wa ndani na nje ya nchi.

  Source: Gazeti la Habari Leo, Mei 15, 2011

  Nchi inaenda wapi na vikombe kila sehemu!!!!!!
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Dah!! Sijui tunaelekea wapi? Mwisho kila mtaa utakuwa na mtoa kikombe!
   
 3. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Haya sasa kazi kwenu wabongo. Soon tutasikia waziri na so ajabu Rais naye ameanza kutoa tiba ya Babu ikulu
   
 4. mtemiwaWandamba

  mtemiwaWandamba JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 536
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Unashangaa Rais au Waziri kuwa tabibu wa kienyeji?
  Kwa taarifa yako Rais wa GAMBIA Nchi iliyoko Africa Magharibi
  Shekhe Captain Jahya Jamme ni tabibu wa kienyeji.
   
 5. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  inaonekana kikombe ni soln au shortcut ya maisha!!
   
 6. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hujataja jina la hiyo wilaya ndugu, au ume assume tunaijua?
   
 7. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wilaya ya Meatu, mkoani Shinyanga
   
 8. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  kwenye kuongeza maisha hapo mmmh!!!!!
   
 9. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Safari hii upele umepata mkunaji, kwani kila kona ya nchi ni kikombe kwenda mbele halafu hakuna hata sehemu moja kikombe hicho kimekuwa scientificaly proved. Sijui tunaelekea wapi sisi kama nchi?
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duu.. nasikia na Babu nae kaoteshwa tena apandishe bei 1500:spit:
   
Loading...