Idadi ya vifo vya mafuruko Ulaya yapindukia 150

Idadi ya vifo vya mafuruko Ulaya yapindukia 150

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Zaidi ya watu 150 wamekufa kufuatia mafuriko makubwa katika maeneo ya magharibi mwa Ujerumani na Ubelgiji. Operesheni zinaendelea za kuwatafuta na kuwaokoa mamia ya watu ambao bado hawajulikani waliko au wako hatarini.

Maafisa katika jimbo la Ujerumani la Rhineland-Palatinate wamesema watu 60 wamefariki dunia, wakiwemo watu 12 katika makazi ya watu wanaoishi na ulemavu katika mji wa Sinzig.

Katika jimbo jirani la North Rhine-Westphalia maafisa wamesema idadi ya vifo ni 43 lakini wameonya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema ameshtushwa na uharibifu uliosababishwa na mafuriko na akaahidi kuzisaidia familia za waliopoteza maisha na miji na vijiji vinavyokumbwa na uharibifu.

Katika nchi jirani Ubelgiji, maafisa wamethibitisha kuwa watu 20 wamekufa na 1,000 hawajulikani waliko
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu kwa sasa anaishi Ubelgiji nchi ambayo imekumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya takribani watu 20 kwa mujibu wa BBC.

Tumuombee Tundu Lisu na familia yake Mungu awalinde.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Mimi nikadhani tayari ameshaenda na mafuriko.
Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu kwa sasa anaishi Ubelgiji nchi ambayo imekumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya takribani watu 20 kwa mujibu wa BBC.

Tumuombee Tundu Lisu na familia yake Mungu awalinde.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Kwani akifa mtapata hasara gani nyie CCM?

Acha unafiki kijana wangu.
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu kwa sasa anaishi Ubelgiji nchi ambayo imekumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya takribani watu 20 kwa mujibu wa BBC.

Tumuombee Tundu Lisu na familia yake Mungu awalinde.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Mnafique Jo!
 
Back
Top Bottom