Monstgala
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 1,079
- 1,037
Ningemwita Mgalanjuka, ila kwa namna ulivyouliza napata picha ya ufahamu wako na sidhani kama utamwelewa, tena kwa kiswahili hiki hiki.
Manake nondo zake huwa nasoma, sielewi, hadi namwita mtu mwengine anisomee kwa sauti lakini natoka mweupe.
Tafadhali Monstgala unahitajika huku.
Mkuu Mkiu nimeitikia wito,
Sayari katika mfumo wa Jua ziko nane. Baada ya kukua kwa teknolojia katika upande wa uchunguzi wa anga basi tukapata kuangalia vizuri mfumo huu na hapo ndipo Pluto ilipoonekana kuwa haikidhi vigezo vya kuwa Sayari. Ikaondolewa na kuwekwa kama mojawapo ya vidude vidogo kuliko zilivyo Sayari nyingine (Dwarf planet) kama alivyojibu mkuu apakak.
Mtoa mada kasema "sayari zilizopo Duniani", hakuna Sayari Duniani, ni kosa la muundo wa swali ambalo wadau wameliona lakini kichwa cha mada kimekaa vizuri na kinaeleweka. Hivyo katika mfumo wa Jua ni Sayari nane (8) lakini kama swali lako lililenga nje ya mfumo wa Jua basi yafuatayo ndio makadirio yake.
Sayari zinazoendelea kugunduliwa na kuhakikiwa ziko nje ya mfumo wa Jua. Kuiona sayari iliyo mbali si rahisi kabisa kutokana na ukweli kwamba sayari nyingi hazitoi mwanga kama zilivyo nyota. Hii inapelekea mwanga wa nyota kuzifanya zisionekane lakini kwa mbinu za kisasa sayari hizi zinafuatiliwa katika mifumo ya nyota nyingine na kuhakikiwa. Mpaka sasa zaidi ya sayari 1800 nje ya mfumo wa Jua zimehakikiwa na zimepewa majina.
Makadirio ya wingi wa sayari katika observable universe ni kwamba sayari ziko nyingi sawa na idadi ya nyota. Uwiano wa sayari na nyota ni kwa kila nyota moja kuna sayari moja. nyota 1:sayari 1 . Ni kwamba si rahisi kuziona ila nyota nyingi zinazungukwa na sayari na vitu vingine. Pia kuna baadhi ya sayari zisizozunguka nyota ziko kivyao-vyao. Katika ulimwengu unaoonekana kuna galaxi zaidi ya bilioni 100. Kila galaxi ina nyota kuanzia 10,000 (dwarf galaxies) mpaka trillioni 200( super massive galaxies) Sasa kama nyota katika ulimwengu tunaoweza kuuona ziko zaidi ya mchanga wa beach zote Duniani, ambao unakadiliwa kuwa Quintilion 7.5., basi sayari pia ni lukuki. Nyingi zaidi ya akili inavyoweza kuhesabu labda kukadiria.
Ukitaka majina ya Sayari katika solar system unaweza ku-google tu. Ukitaka kusoma zaidi pia google.
Cheers.