Mkuu nakutahadharisha tena nakuomba sana, ujenzi wa ghorofa (gorofa) maswala ya nondo mwachie Engineer si suala la kukisikia au kuulizia mitaani au kwa fundi mzoefu. Nasema hakuna kitu kama hicho, utakuja juta baadae!! Mahesabu ya nondo yanafanywa kwa utaalamu (calculations) kutumia fomula sio kukisia, ukubwa wa eneo/unene wa zege (floor thickness), matumizi ya jengo na pia ratio (vipimo) vya zege. "Foundation" ndio inabeba kila kilicho juu ya ghorofa, kwa hiyo huwezi kubadili juu bila kurekebisha chini au kujua chini kuna uwezo gani.
* Tuache njia za mkato, mme sahau mara hii kilichotokea Changombe/Kariakoo/Kisutu na kwengineko?